Pages

KAPIPI TV

Tuesday, July 22, 2014

JESHI LA POLISI LAWASHIKILIA 25 KWA UCHUNGUZI TUKIO LA MLIPUKO WA MABOMU


mngulujuly152014
Kufuatia tukio la mlipuko wa bomu siku ya tarehe 7/7/2014 majira ya saa 22.15 usiku katika mgahawa wa VAMA, eneo la Uzunguni Jijini Arusha, ambapo watu wanane walijeruhiwa, Jeshi la Polisi limewakamata watuhumiwa 25 kwa uchunguzi. Kufuatia uchunguzi huo kati yao watu sita watafikishwa mahakamani mapema iwezakanavyo.
Watuhumiwa watakaofikishwa Mahakamani kwa tukio hilo ni:
 
1. SHAABAN MUSSA MMASA @ JAMAL, Umri miaka 26 Kabila, Msambaa. Mlinzi aliyekuwa zamu siku hiyo kwenye mgahawa huo.
 
2. ATHUMAN HUSSEIN MMASA, Umri miaka 38 kabila Msambaa, Mlinzi katika Mgahawa wa Chinese uliopo eneo la GYMKHANA jirani na eneo la tukio.
 
3. MOHAMED NURU @ MUHAKA, Umri miaka 30 Kabila Msambaa, Mlinzi katika mgahawa wa Chinese jirani na eneo la tukio.
 
4. JAFFAR HASHIM LEMA, Umri miaka 38 Mchaga Mwalimu wa Shule ya Msingi Olturmet Wilaya ya Arumeru. Pia alikuwa Imam wa Msikiti wa QUBA mjini Arusha. Huyu ametambuliwa kama mmoja wa viongozi walioratibu matukio ya milipuko ya mabomu maeneo mbalimbali nchini.
 
5. ABDUL MOHAMED HUMUD SALIM,@Wagoba; umri wa miaka 31, Mmanyema wa Ujiji Kigoma, wakala wa Mabasi Stendi Arusha.
 
6. SAIDI MICHAEL TEMBA; umri wa miaka 42, Mchaga, mfanyabiashara wa Arusha.
Aidha tarehe 21/07/2014 majira ya saa 20.00 usiku maeneo ya Sombetini walikamatwa YUSUFU HUSSEIN ALLY @ HUTA, kabila Mrangi, umri wa miaka 30 na mkewe SUMAIYA JUMA , kabila mwasi umri wa miaka 19 wakiwa nyumbani kwao baada ya kupekuliwa walikutwa na mabomu ya kutupwa kwa mkono saba, risasi sita za shortgun, mapanga mawili, unga wa baruti unaokadiriwa kufika nusu kilo na bisibisi moja. 

Mtuhumiwa YUSUFU HUSSEIN ni miongini mwa watuhumiwa waliokuwa wanatafutwa kwa ulipuaji wa mabomu maeneo yote jijini Arusha. Mahojiano yanaendelea dhidi yake.
 
Uchunguzi wa shauri hili pamoja na matukio mengine ya milipuko unaendelea, ikiwa ni pamoja na kuwahoji watuhumiwa walioko mikononi mwa Polisi na kuwakamata watakao bainika kuhusika na matukio hayo, mtajulishwa matokeo ya uchunguzi huo mara utakapokamilika.
 
Hata hivyo Jeshi la Polisi linatangaza kumtafuta YAHAYA HASSAN HELLA, kabila mrangi, umri wa miaka 33, mkazi wa Mianzini Arusha, mwenye asili ya eneo la Chemchemu Kondoa Dodoma kwa tuhuma za kuhusika na matukio ya ulipuaji mabomu nchini. Zawadi nono itatolewa kwa yeyote atakaye toa taarifa zitakazowezesha ukamatwaji wa mhalifu huyu. Jeshi la Polisi linawashukuru wananchi kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa. Asanteni.
…………………………….. ISAYA MNGULU-CP MKURUGENZI WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI TANZANIA

PINDA AZINDUA CHUO CHA VETA NA KUKABIDHIWA NYUMBA YA WALIMU SAME

PG4A5283
PG4A5427
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka jiwe la Msingi la  Chuo cha Ufundi ( VTC)   cha Maore wilayani Same Julai 21, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A5458
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikata utepe katika uzinduzi wa   Chuo cha Ufundi ( VTC)   cha Maore wilayani Same Julai 21, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A5682
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza na Jaji  Mstaafu, Amir Manento baada ya kukabidhiwa  nyumba iliyojengwa  na Jaji huyo kama mchango wake kwa Wananchi wa kijiji alichozaliwa cha Mtii.  Nyumba hiyo ilitolewa kwa  Halmashauri ya Wilaya ya Same ili ilitumike kama makazi ya Walimu. Julai 20, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A5714
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na watoto wa kijiji cha Mtii wilayani Same baada  ya kukabidhiwa nyimba ya walimu iliyojengwa katika kijiji hicho na Jaji Mstaafu Amir Manento, Julai 20, 2014. (Picha na Ofisi ya  Waziri Mkuu)
PG4A5782
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda  (kushoto) akipokea zawadi ya miwa kutoka kwa mkazi wa kijiji cha Mtii wilayani Same (jina Halikupatikana)
PG4A5395 1
Mke wa Waziri uu Mama Tunu Pinda akipanda mti chuoni hapo.

NHIF KIGOMA YAWAFUNDA WANDISHI WA HABARI

Na Magreth Magosso,Kigoma


CHAMA cha wandishi wa habari Mkoa wa Kigoma,wametakiwa watumie chama chao  kujiunga na mfuko wa Afya (Nhif)  kwa  lengo  la  kupunguza  changamoto ya kipato inayochangiwa na kutokuwa na mikataba ya ajira husika.


Hayo yalisema  na Meneja wa mfuko huo mkoani hapa Elias Odhiambo alipokuwa akizungumza na wanachama hao  kigoma Ujiji ,katika ofisi za  KGPC kwa tija ya kutaka watumie fursa ya huduma ya vikundi ili kunufaika na mafao ya matibabu yatolewayo na mfuko huo.


“ changamoto kubwa ni uhakika wa kipato,ambapo kupitia huduma mpya ya vikundi rasmi vya uzalishaji mali ni nafuu kwenu, kujiunga na bima ya afya na kila mwanachama atachangia sh.76,800 tu kwa mwaka” alibainisha Odhiambo.


Alianisha huduma ya vikundi ni chachu kwa kila mtanzania kuwa na uwezo wa kuchangia kiasi hicho kwa mwaka na endapo atahitaji kuongeza hitaji la mtegemezi anapaswa amchangie kiasi hichohicho,kwa dhati ya kuondoka na adha ya kulipa  matibabu ya papo kwa papo.

Alisema wananchi wote waliopo katika vikundi vidogo na vikubwa ambavyo vipo kihalali ni wakati wao kutumia fursa hiyo. ambayo inakidhi hali halisi ya maisha ya mtanzania na kusisitiza wananchi wathubutu hilo kwa faida ya leo na siku za usoni.


Mwenyekiti wa Kgpc Deogratius Nsokolo aliunga mkono huduma hiyo ,ambayo ni fursa kwa wanachama wake,ambao asilimia 99 hawana mikataba ya ajira ,hali inayochangia washindwe kwenda kupima afya zao kwa wakati .


Alisema  wataweka  utaratibu,kanuni na sheria  kwa kuhakiki  kila mchango wa  mwandishi kuingia katika mfuko huo kwa  wakati, ili kuwajengea uwezo wa kulipia huduma hiyo ambayo ni tija katika uwajibikaji wao.

MIILI INAYODAIWA NI YA BINADAMU ILIYOKUTWA JANA JIJINI DAR IKIWA NDANI YA MIFUKO IMETUPWA

63a4c18aba35870d3d4177324b654bae
Gari likiwa limebeba mifuko yenye viuongo hivyo, ambapo Jeshi la Polisi wilaya ya Kinondoni limesema kuwa limeanza uchunguzi wa kina baada ya kukakamata viungo mbalimbali vinavyodhaniwa kuwa ni vya binadamu katika mifuko ya plastiki katika machimbo ya kokoto sehemu za Mbweni Mpiji, Magohe, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam .http://daresalaam-yetu.blogspot.com
ad41c51ed504857ec7b80c1988a66e05
Sehemu ya mifuko ya plastiki iliyokutwa na viungo hivyo ambavyo inasemekana ni pamoja na mikono, miguu, ngozi na sehemu nyingine za miili

PPF YAFUTURISHA WAFANYAKAZI WAKE

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, akipakua chakula wakati  futari iliyoandaliwa na ofisi yake katika hoteli ya serena leo
Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakichukua chakula wakati wa futari iliyoandaliwa na Mfuko huo wa Pensheni wa PPF leo.
Afisa Mahusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Janeth Ezekiel akimuonyesha baadhi ya vyakula mjumbe wa bodi ya PPF, Mh Mbaruku Igangula wakati wa futari iliyoandaliwa na mfuko wa Pensheni wa PPF.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, akitoa hotuba kwa wafanyakazi wa Mfuko huo baada ya futari iliyoandaliwa na Ofisi yake kwa wafanyakazi wake kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Pembeni ni Msimamizi wa Masoko wa mfuko huo wa Pensheni wa PPF, Bw Alfred Elia
 Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakishiriki futari iliyoandaliwa na Mfuko huo kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Picha Zote na Josephat Lukaza - Lukaza Blog

MAUAJI YA VIKONGWE YASHIKA KASI MLELE- KATAVI

???????????????????????????????
(Picha zote na Kibada Kibada –Mlele Katavi)

Na Kibada Kibada –Mlele Katavi.
Wimbi la mauaji kwa watu wenye umri kuanzia  miaka 60 na kuendelea  Wilayani Mlele Mkoani Katavi linaonekana kushika kasi na kutishia hali ya ulinzi na usalama kama hatua za makusudi hazitachukuliwa.

Hii ni kwa Mujibu wa Taarifa ya Hali ya ulinzi na Usalama Wilayani humo  iliyotolewa na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa wilaya hiyo , Zabron Ibeganisa kwenye Mkutano Mkuu wa Baraza la Madiwani uliokuwa ukipokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali zilizotekelezwa kwa kipindi cha mwaka  wa 2013/2014.

Mkuu huyo wa upelelezi wa makosa ya jinai alieleza kuwa changamoto zitokanazo na matukio ya mauaji ni kubwa katika wilaya hiyo  na watu wanaolengwa na mauaji hayo ni wale wenye umri kuanzia miaka 60 na kuendelea ambapo kwa sehemu kubwa mauaji hufanyika nyakati za usiku kwa kuwavamia walengwa kwenye makazi yao.

Alisema katika matukio 24 yaliyotokea, watu 24 kwa kipindi cha januari hadi juni mwaka 2014   wameuwawa na waliolengwa hasa ni watu wa umri huo.

Alisema kuwa wauaji hao hutumia silaha zenye makali kama panga,shoka, na sime kuwakata waliowalenga na kisha kutoweka bila kuchukua kitu chochote.

Mauaji haya yanafanana sana na jinsi yanavyotokea katika mikoa ya Shinyanga kwa kuwaua vikongwe kwa imani kwamba ni wachawi.

Aidha akifafanua zaidi alieleza kuwa katika kipindi cha miezi sita iliyopita kuanzia mwezi januari hadi juni 2014 ,  yametokea mauaji 24 na watu 24 wameuwawa  ambapo kati ya mauaji hayo watuhumiwa sita walikamatwa.

Akibainisha hali ya uhalifu katika wilaya hiyo alieleza kuwa matukio mbalimbali ya makosa madogo ya kuwania mali yalikuwa 107 makosa makubwa dhidi ya binadamu kwa mauaji yalikuwa 24, kubaka 23,kulawiti mawili ,makosa madogo dhidi ya Binadamu yalikuwa 194, makosa madogo dhidi ya uvunjwaji wa maadili yalikuwa 108,  ajali zilizosababisha vifo ni mbili,ajali zilizosababisha majeruhi zilikuwa 39, ajali za kawada 17, makosa mengine 844.

Makosa makubwa dhidi ya maadili ya jamii kama kupatikana na bangi yalikuwa manane, kupatikana na pombe ya moshi 8, makosa ya kupatikana na nyara za serikali yalikuwa matatu na kupatikana na silaha moja
Ipo changamoto kutokana na ugumu uliopo wa kuwatambua wauaji ,hata hivyo jeshi la polisi linatoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo na kuwaasa  wana jamii  kuendeleza  ule utaratibu wa  daftari la wakazi kwa kuwaorodhesha wakazi kwenye maeneo kwa kuwa ni muhimu na litasaidia kuwatambau wageni wanaoingia kwenye maeneo na iwapo watakuwa na nia mbaya watabainika.

Monday, July 21, 2014

WANAWAKE WATWANGANA SOKONI HUKU WAKIWA NA SWAUMU-TABORA







Baadhi ya wanawake watatu katika soko la mkulima Tabora mjini wamejikuta wakipeana kipigo kikali mchana kweupe wakati walipokuwa wakifanya biashara za mbogamboga hatua ambao ilisababisha kuharibu sehemu ya bidhaa wanazouza ambapo muda mfupi baadae waliamuliwa ugomvi huo na askari polisi Fakih Abdul aliyekuwa akipita sokoni hapo,hata hivyo chanzo cha ugomvi huo kimetokana na mmoja wa wanawake hao kuwa mbabe kwa wenzake na hivyo kushindwa kumvumilia kutokana na vituko vyake. 

MWIGAMBA ATAKA ACT WATUMIE FURSA CHAGUZI SERIKALI ZA MITAA-KIGOMA

Na Magreth Magosso, Kigoma.

KATIBU mkuu wa chama cha Alliance for change and Transparency(ACT)  taifa  Samson Mwigamba amewataka viongozi wa chama hicho  kuanzia ngazi ya kata na majimbo kuhakiki viongozi  watakaogombea katika uchaguzi ujao 2014 wa serikali za mitaa kwa kuwasimika viongozi wenye upeo wa  mambo na wanaokubalika katika jamii.

Akitoa kauli hiyo  kigoma Ujiji jana katika kikao cha viongozi na wanachama wa chama hicho kutoka jimbo la Kigoma Kaskazini, Kusini na kigoma mjini alisema watumie fursa ya hiyo kuwapa nafasi viongozi wenye sifa na vigezo  kwa lengo la kuboresha mfumo wa utawala.

Alisema ili chama kiweze kupata nyadhifa mbalimbali za uongozi ni lazima kila kiongozi katika jimbo alilopo ahakikishe kunakuwa na uongozi kamili katika vijiji ,ili kunyakua majimbo katika nafasi za udiwani, ubunge na urais.

Hata hivyo aliwataka viongozi na wanachama kuacha siasa za matusi katika majukwaa na badala yake watumie lugha za hekima,busara na kizalendo kwa hoja zenye mashiko ya kuelimisha umma na kufanya kazi kwa uwazi na uwajibikaji.

Mwigamba alisema lengo la chama hicho kurekebisha siasa ya nchi kupitia vyama pinzani kwa kuondoa tofauti zilizopo pamoja na kuondoa utashi wa mwasisi wa chama katika vyama vilivyopo, kuwa na demokrasia ya kweli ambapo vyama vingine havizingatii hilo.

Naye katibu wa mawasiliano na habari Muhamedi Masaga alisema kuanzishwa kwa chama sio kwa lengo la kudhohofisha vyama vingine ni kuwa na chama chenye mshikamano, umoja na kulinda uzalendo wa   n chi ili kushika dola ya nchi katika chaguzi zijazo.

Alisema katika ziara walizozifanya katika mikoa mitatu, mkoa wa kigoma umekuwa kinara  wa wanachama waanzilishi ambao wamefikia 570 ikifuatiwa na Katavi 400 pamoja na Tabora 150 ambapo ni mwanzo unaoleta matumaini katika kukiendeleza chama.

TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) : NANI KUCHOMWA NA JUA LA UTOSI WIKI HII?

ILI KUWANUSURU AU KUMNUSURU MSHIRIKI UMPENDAE AENDELEE KUWEPO NDANI YA NYUMBA YA TMT UNACHOTAKIWA KUFANYA NI KUMPIGIA KURA KWA WINGI SANA.
JINSI YA KUPIGA KURA NI ANDIKA NENO "TMT" ikifuatiwa na namba yake ya ushiriki halafu tuma kwenda 15678. Mfano TMT00 tuma kwenda 15678.

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA ASHIRIKI MKUTANO WA TATU(03) WA UMOJA TAASISI ZA MAGEREZA BARANI AFRIKA, MAPUTO MSUMBIJI

image_3
image_1
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa Tatu(03) wa Umoja wa Taasisi za Urekebishaji(Magereza) Barani Afrika wakifuatilia Majadiliano ya Mkutano huo uliofanyika hivi karibuni Maputo, Msumbiji(wa kwanza kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja(wa kwanza kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Uganda, Dkt. Johnson Byabashaija(mstari wa nyuma) ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza Nchini Tanzania wakifuatilia mjadala katika Mkutano huo wa Kimataifa.
image_2
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Nchini Tanzania, Profesa Sifuni Mchome akiwasilisha Mada ihusuyo Urudiaji wa Vifungo Magerezani kwa Wahalifu(Recividism) katika Mkutano wa Tatu wa Umoja wa Taasisi za Urekebishaji(Magereza) Barani Afrika uliofanyika hivi karibuni Maputo, Msumbiji.
photo
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, John Casmir Minja akichangia Mada katika Mkutano wa Tatu(03) wa Umoja wa Taasisi za Urekebishaji(Magereza) Barani Afrika uliofanyika hivi karibuni kuanzia July 14 – 17, 2014 Maputo, Msumbiji.
image
Maafisa na Askari Magereza wa Msumbiji wakimsikiliza Mgeni rasmi, Rais wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji, Mhe. Dkt. Armando Guebuza(hayupo pichani) katika ufunguzi wa Mkutano wa Tatu(03) wa Umoja wa Taasisi za Urekebishaji(Magereza) Barani Afrika uliofanyika Maputo, Msumbiji.

NAPE : CCM HAIKATAZI MWANACHAMA WAKE KUTANGAZA NIA YA KUGOMBEA UONGOZI

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye amesema Chama Cha Mapinduzi hakimzuii mwanachama yeyote kutangaza nia ya kugombea Uongozi katika muhula unaofuata isipokuwa Chama kimezuia kampeni za mapema kwani ndio chanzo cha makundi ndani ya Chama akizungumza kwenye kipindi cha Baragumu kinachorushwa na Channel 10 ,Nape  alisema taratibu za kugombea Uongozi ndani ya chama zipo na kuna Kanuni mbili, moja ni ya Kanuni za Viongozi na Maadili na pili Kanuni zinazosimamia Uchaguzi ndani ya CCM, akinukuu kutoka kwenye kitabu cha Kanuni za Viongozi na Maadili ,Nape alisema “Wanachama wenye nia ya kugombea nafasi ya uongozi katika muhula unaofuata anaweza kutangaza nia ya kugombea lakini haruhusiwi kufanya kampeni kabla ya muda”.
   Akizungumzia juu ya adhabu wanazopewa waliokiuka alisema adhabu hizi zina shabaha ya kuwasaidia wanachama na Viongozi kujirekebisha.
Nape pia alizungumzia suala zima la upatikanaji wa Katiba Mpya,alisema CCM imeshikamana sana kiasi cha kuwachanganya Wapinzani, aliendelea kwa kusema Kanuni,Sheria zinazotumika ni makubaliano ya wote.(Wapinzani walishiriki katika kamati kutengeneza kanuni na sheria na zikapitishwa Bungeni wakiwemo na Rais akasaini).
Chanzo: kamerayangublog.com

MAMIA YA WANANCHI SOMANGA KILWA WAJITOKEZA KUPIMA AFYA BURE,KAYA 70 ZAJIUNGA NA CHF PAPO KWA PAPO WAKIPOKEA MWENGE WA UHURU.

822
Na. Paul Marenga-NHIF LINDI
841
Wananchi wa Kilwa wakiwa kwenye foleni ya kupata huduma za vipimo kwenye banda la Mfuko wa taifa wa bima ya afya ambapo huduma za upimajiwa kiwango cha sukari kwenye damu (RBG),shinikizo la damu (BP),uwiano wa uzito na urefu wa mwili (BMI) na ushauri wa kitaalamu ulitolewa na madaktari,wakati wa mapokezi ya mwenge wa uhuru kwenye viwanja vya shule ya msingi Somanga-Kilwa.
868
Meneja wa mfuko wa taifa wa bima ya afya mkoa wa Lindi Fortunata Kullaya akitoa taarifa ya utekelezaji wa zoezi la upimaji afya na mwitikio wa wananchi wa kilwa ambapo takribani wananchi 257 walijitokeza kupimwa afya na  kaya 73 zilijiunga papo kwa papo na CHF Kwenye banda la mfuko kwa kiongozi wa mwenge kitaifa kwa mwaka 2014 Rachel Kassanda,ambaye alikagua shughuli mbalimbali zilizokuwa zikitekelezwa kwenye viwanja vya shule ya msingi somanga ambapo mwenge wa uhuru ulipokelewa,kulia  ni mkuu wa wilaya ya Kilwa mhe. Abdallah Ulega.
882
Mnafanya kazi kubwa kuisaidia serikali katika kutoa elimu kwa jamii kuchangia huduma za afya ili ziboreke sambamba na upimaji wa afya bure kwa magonjwa yasiyoambukiza  unaomuwezesha mwananchi wa kawaida kupata huduma pasipo gharama..hongereni sana alisema kiongozi wa mwenge kitaifa Rachel Kassanda,huku akisisitiza wananchi kutambua CHF ni mali yao hivyo kujiunga kwao kwa wingi ndiyo msingi wa maboresho ya huduma za afya hususani upatikanaji wa dawa,kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe.Abdallah Ulega,kushoto anayemsikiliza ni Meneja wa NHIF Mkoa wa Lindi Fortunata Kullaya.
892
Kiongozi wa mwenge kitaifa mwaka 2014 Rachel Kassanda akiwataka wananchi wa kilwa kujiunga na CHF,kwani ndiyo mkombozi wa matibabu sasa kwa kuzingatia maboresho ya huduma za afya yanavyowezekana chini ya sera ya urasimishaji wa majukumu kwa jamii hususani ya uchangiaji baina ya wananchi na serikali,ambapo mfuko wa taifa wa bima ya afya unasimamia mfuko wa afya ya jamii kwa niaba ya serikali ,kulia ni mkuu wa wilaya ya Kilwa mhe.Abdalla Ulega ambaye ndiye mwenyeji wa mapokezi ya mwenge wa uhuru.

WANANCHI WAITOLEA MACHO MANISPAA-KIGOMA

Na Magreth Magosso,Kigoma
 
Mradi wa ujenzi wa Gati katika mwalo wa kibirizi katani humo mkoani hapa,upo mashakani  kuanza kwake ,kutokana na  wahanga wa eneo hilo wapatao 53 kuipa siku 30 Manispaa ya kigoma ujiji ili kuboreshewa  stahiki zao  kwa mujibu wa Sera  na Sheria ya Ardhi husika.
Hayo yalisemwa juzi na mwanasheria wa kujitegemea Daniel Rumenyela katika ofisi za chama cha wandishi wa habari mkoani hapa,akiwakilisha adha za wananachi hao, juu ya ufinyu wa fidia usiozingatia sheria ya ardhi ya mwaka 1999 .
“uthamini  ulifanyika 2012 na malipo 2014,kifungu cha( 5),( 4 )ya sheria ya ardhi  na sera ya ardhi inataka fidia itolewe kwa wakati na haraka kwa wahanga na ikichelewa  tathimini  ifanywe   kila baada ya miezi sita, ili fidia ilingane na hitaji la leo” alibainisha Rumenyela.
Alisema  wamempa siku 30 Mkurugenzi wa manispaa ya kigoma Ujiji ,ili aweze kuboresha  haki stahiki za wahusika kwa sheria husika kwa lengo la kuboresha ustawi wa jamii na maendeleo kwa ujumla.
 

Meneja wa Mamlaka ya Bandari TPA wa hapa Patrick Namahuta alipohojiwa juu ya hili alisema mchakato wa kufidiwa kwa walengwa ulifanywa na mthamini wa manispaa hiyo kwa mujibu wa sheria husika na wao walitenga bajeti zaidi  ya milioni 600 ili kukidhi hitaji la walengwa.
 

Alisema TPA taifa ilitoa fidia kwa wahanga hao pasipo mkoa kuhusishwa kikamilifu katika kuhakiki picha na akaunti za walengwa, ili anayelipwa  akiri ni sahihi na kusisitiza malipo yalifanywa makao makuu na akaunti za wahanga zilipelekwa na manispaa husika.
 Namahuta  alisema lengo la mradi huo ni kuboresha huduma kwa wadau,ambapo  mwalo wa kibirizi  ni chachu kibiashara kwa nchi jirani za Burundi na jamuhuri ya watu wa kongo(DRC)  na    ili kukidhi haja za walengwa kwa ukanda wa  ziwa Tanganyika  zinahitajika gati 19 ambayo  itaongeza ufanisi kwa mamlaka hiyo.
Mkuu wa wilaya ya hapa Ramadhan Maneno amekiri mchakato ulifanywa na manispaa husika kupitia mthamini wao na walicholipa TPA ni matokeo ya uthamini na kusisitiza wananchi walishirikishwa kwa kila hatua na kuwasihi walengwa wasitake malipo yalingane.
 Alisema mfumo mbovu wa  malipo  ya fidia hauko vyema, kutokana na  TPA mkoa kutoshirikishwa katika kila hatua  na endapo ingeshirikishwa  ni rahisi kubaini haki na batili kwa lengo la kuondoa utata wa fidia hizo kwa wananachi,ambao  wanamtazamo  hasi kwa  manispaa  katika uwajibikaji .
Kaimu  Mkurugenzi  wa  manispaa  hiyo Moses Weransari alisema mthamini alizingatia uhalisia wa thamani za wahanga  na kwa mara ya mwisho kufanya tathimini ilikuwa 2013 na  wahanga kulipwa rasmi kupitia akaunti zao ni  Juni,2014 .

KOMWETA HEMED MANETI A.K.A CHIRIKU WA VIJANA JAZZ AFUATA NYAYO ZA MAREHEMU BABA YAKE HEMED MANETI ULAYA

1970462_1454799778083088_1638018053_n
Komweta Hemed Maneti a.k.a Chiriku mwanamuziki wa bendiya Vijana Jazz
1486871_1427285270834539_2027172492_n
Marehemu Hemedi Maneti Ulaya Chiriku aliyekuwa mwamuziki wa bendi ya Vjana Jazz enzi hizo.
......................................................................................................
Komweta Hemed Maneti a.k.a Chiriku ni Mtoto wa mwanamuziki wa zamani marehemu Hemedi Maneti Ulaya Chiriku aliyekuwa akiimba katika bendi ya umoja wa vijana Vijana Jazz enzi hizo ambapo anasema amekuwa kwenye muziki kwa muda mrefu japokuwa kama ilikuwa kama kujifurahisha, Komweta Hemed Maneti alianza muziki kama kazi mwezi Agosti mwaka 2013 akiimba katika bendi ya Vijana Jazz ambayo marehemu baba yake Mzee Hemedi Maneti Ulaya aliitumikia kwa mafanikio enzi za uhai wake.

Komweta Hemed Maneti a.k.a Chiriku amekuwa akijizolea umaarufu mkubwa katika bendi hiyo kwani mashabiki wengi wamekuwa wakimkumbuka marehemu baba yake mara anapoimba jukwaani kwani kwa kiasi kikubwa sauti zinaendana na marehemu baba yake Hemed Maneti, Bendi ya Vijana Jazz imekuwa ikipata umaarufu siku hadi siku katika maonyesho yake yanayofanyika kwenye klabu ya Kilwa Road Pub Ijumaa, Jumamosi wanapiga Jet Lumo na Jumapili kwenye ukumbi wa Vijana Hall Kinondoni.

Komweta mpaka sasa ana Nyimbo mbili na zipo mbioni kutoka akiwa ameimba kwa kushirikiana na bendi ya Vijana Jazz mtunzi akiwa ni yeye mwenyewe nyimbo yake Inaitwa (Walimwengu) na nyingine inaitwa (Nitajuaje) ukiwa ni utunzi wa Shomary Ally lakini yeye akiwa mwimbaji kiongozi katika wimbo huo pamoja naye Julius Mwesiwa.

Wanamuziki wakongwe waliobaki kwenye bendi ya vijana Jazz ambao waliwahi kuimba na marehemu Hemed Maneti ni Shomary Ally,Abdallah Mgonahazeru na Roshy Mselela, Ndoto za Komweta Hemed ni kuwa mwanamuziki wa kimataifa na kuipepeprusha vema bendera ya Tanzania ndani na nje ya mipaka ya TANZANIA ameolewa na ana mtoto mmoja wa miaka 5 anayeitwa Fahad.

 Anaongeza kuwa Changamoto za kazi ya muziki na malezi ni nyingi lakini muhimu ni kujua jinsi gani utapanga ratiba zako vizuri na kuhakikisha unafanya maandalizi mazuri kwa ajili ya mtoto na hili halinishindi natimiza majukumu yangu vizuri kama mama
Ni kweli kwamba mara nyingi nakuwa nafanya kazi siku za wikiendi hivyo nakosa muda wa kutosha wa kukaa na mtoto ukizingatia ndiyo siku na yeye anakuwa anapumzika haendi shule, lakini kama mama unatakiwa kujua majukumu ya familia yako ninafurahia maisha na familia yangu na mtoto wangu ni mweye furaha sana ninamshukuru mungu kwa hilo,
hata hivyo siku za jumatatu zinakuwa zina changamoto kubwa sana hasa katika kumwandalia mahitaji yake kwa ajili ya kwenda shule kwakuwa nakuwa nimechoka na kazi.

Mwanamuziki huyo anasema mashabiki wa bendi ya vijana wamempokea vizuri sana kusema kweli anaongeza kuwa "Nashukuru Mungu sana kwa hilo
na hili linajidhihirisha ninapokuwa nafanya shoo zangu...watu hawakai chini mara nyingi wanakuwa wakicheza..."
Anamaliza kwa kusema "Umaarufu wa marehemu baba yake mzee Hemed Maneti upo na siwezi kuuepuka...lakini kubwa watu wananipima kutokana na utendaji na ufanisi wangu wa kazi yangu niwapo jukwaani".

MAAFISA BARAZA LA HABARI TANZANIA WATEMBELEA CHUO CHA MUSOMA UTALII NA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI TABORA

Baadhi ya maafisa kutoka Baraza la Habari Tanzania MCT,Bi.Pili Mtambalike,Bi.Alakok Mayombo na Bw.John Nguya walitembelea Ofisi ya Chama cha Waandishi wa habari Tabora ambapo waliambatana na wenyeji wao Mkurugenzi wa Chuo Cha Musoma Utalii  Tabora Bw.Shaaban Mrutu na Mkufunzi wa chuo hicho Bw.Marwa Robert.

CHADEMA YAZIDI KUTEKETEZWA NA MOTO WA CHAMA KIPYA CHA ACT, TABORA NAKO CHAWAKA


TABORA, Tanzania
WIMBI la viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kukikimbia zimeendea, kufuatia Katibu wa Chama hicho  mkoani Tabora, Othman Balozi na kundi la wanachama wengine kibao kutangaza leo kujiunga na chama kipya cha  ACT Tanzania, ambacho kinaaminika kuasisiwa na aliyekuwa Natibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe ambaye kwa sasa amebakia ni mbunge tu kwa tiketi ya chama hicho.

Mbali na Balozi aliyewaongoza wajumbe 78 wa baraza kuu la Chadema hivi karibuni kwenda kwa msajili wa vyama kulalamikia katiba ya Chadema kukiukwa, pia wamo viongozi mbali mbali wa mabaraza ya kimkoa kiwilaya na majimbo walioamua kujitoa na kujiunga na Chama kipya cha ACT-Tanzania

Viongozi hao ni mwenyekiti wa Bavicha mkoa wa  Tabora Hussein Kundecha,mratibu wa uhamasishaji Bavicha  wilaya ya Tabora mjini Nzuki Machibya na Ramadhan Simba Mwenyekiti wa Chadema jimbo la Bukene.

Wengine ni Suni Yohane aliyewahi kuwa katibu wa Chadema wilaya ya Nzega pamoja na mwenyekiti wa baraza la wanawake katika wilaya hiyo.

Wimbi hilo pia limewazoa wanachama wa kawaida kutoka Chadema na CUF pamoja na watu ambao 200 ambao  hawakuwahi kuwa wanachama wa chama chochote hapo awali.

Kuhama kwa viongozi hao kumekuja ikiwa ni siku moja baada ya waliokuwa viongozi wa Chama hicho mkoa wa Kigoma kubwaga Manyanga

Waliobwaga Manyanga kwa Mkoa wa Kigoma hiyo juzi ni Jafari Kasisiko Mwenyekiti, katibu Msafiri Wamalwa na iti wa Baraza la wanawake wa  mkoa wa Kigoma kubwaga Manyanga

Akizungumzia sababu ya kujiondoa Chadema Balozi alisema kabla ya kufikia uamuzi huo alimpa taarifa mwenyekiti wake wa mkoa Kansa Mbaruku juu ya uamuzi huo

Alisema akiwa miongoni mwa viongozi wa awali kukipokea Chadema katika mkoa wa Tabora,amechoshwa na chama hicho kuacha misingi yake ya  kidemokrasia na kukumbatia Ubabe na dharau huku wakiwanyooshea vidole  vya usaliti wale wanaohoji baadhi ya mambo wasiyoridhika nayo ndani ya Chama hicho.

“Leo mimi ni mtu huru na nimewasikiliza ACT na falsafa yao ya uwazi na kuamua kujinga kwa hiari yangu sasa huu uwazi waudhihirishe na sitasita kuhoji pale penye matatizo nawasihi katika hali hiyo wawe wavumilivu kwa tutakayohoji”alisema Balozi.