Pages

KAPIPI TV

Sunday, March 11, 2012

MWANAFUNZI CHUO CHA SAUT TABORA AJINYONGA"Wenzake wamlilia wasema alikuwa Mnyonge na anakunywa pombe kali"

 Mwili wa mwanafunzi wa chuo cha SAUT Tawi la Tabora aliyefahamika kwa jina la Qamunga Yandu(28) akiwa amejinyonga katika mlango wa kuingia chumbani kwake kwa kutumia shuka yake.

Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha SAUT wakiwa wanalia baada ya kuushuhudia mwili wa mwanachuo mwenzao ukiwa unaning'inia mlangoni  katika moja ya nyumba aliyokuwa amepanga na wenzake huko kata ya Ipuli Manispaa ya Tabora.
Mwanafunzi wa chuo cha SAUT tawi la Tabora Qamunga Yandu amejinyonga kwa kutumia shuka yake katika mlango wa kuingilia chumbani kwake kata ya Ipuli mjini Tabora.

Mwanafunzi huyo alibainika kufanya kitendo hicho muda mfupi mara baada wanafunzi wenzake ambao anaishi nao katika nyumba ya kupanga huko Ipuli barabara ya kazima.

Hata hivyo pamoja na kutopatikana kwa maelezo yanayohusu sababu ya kujinyonga kwa mwanafunzi huyo lakini katika chumba chake kumekutwa maganda ya pombe kali zilizotumika pamoja na vichungi vya sigara.

Baadhi ya wanafunzi wenzake waliokuwa katika eneo la tukio wameeleza kuwa marehemu alikuwa anakunywa pombe kupindukia na mara nyingi amekuwa akitembea peke yake.

Kwaupande mwingine huku wakionesha kutokuwa na uhakika wanafunzi hao ambao walimtaja Qamunga kuwa ni mkazi wa Babati walisema kuwa mwishoni mwa mwaka jana alifiwa na baba yake mzazi jambo ambalo lilionesha kuwa lilikuwa likimtia majonzi mara kwa mara wakati alipokuwa akiwasimulia wenzake wa karibu juu ya kifo cha mzazi wake huyo mpendwa.

Jeshi la Polisi mkoani Tabora bado linaendelea na uchunguzi kuhusiana na kifo cha kijana huyo ambaye alilazimika kupanga chumba kutokana na ukosefu wa mabweni katika chuo cha SAUT.
Post a Comment