Pages

KAPIPI TV

Monday, March 12, 2012

SERIKALI YAIPONGEZA KAMPUNI YA KISHEN ENTERPRISES KWA KUIBUA VIPAJI VYA WANARIADHA TABORA"Yatumia zaidi ya Milioni tatu katika mashindano ya TABORA MARATHON"

Mkuu wa mkoa wa Tabora Fatma Mwassa akizungumza wakati wa kufunga mashindano ya Tabora Marathon katika viwanja vya kumbukumbu ya Mwl.Nyerere Community Center Tabora na kutoa zawadi kwa washindi wa mashindano hayo.
Kutoka kushoto ni Mshindi wa kwanza wa Tabora Marathon Rose Seif,katikati ni mshindi wa pili Salima Mgazi,mwishoni ni Naomi Samwel mshindi wa tatu kwa wanawake.
Mshindi wa kwanza wa mashindano ya Tabora Marathon kwa upande wa wanaume,Dickson Mkami
Meneja Masoko Seraphine Baraka na mshauri wa ufundi  Tabora Marathon Tullo Chambo wakati wakishiriki mashindano ya Tabora Marathon.
Matukio yaliyojiri siku ya mashindano ya Tabora Marathon.

Serikali mkoani Tabora imeipongeza kampuni ya uuzaji wa pikipiki Kishen Enterprises kwa uamuzi wake wa kuanzisha mpango wa kuibua vipaji vya wanariadha kupitia mashindano yajulikanayo kama Tabora Marathon.

Mkuu wa mkoa wa Tabora Fatma Mwassa ametoa pongezi hizo wakati akifunga mashindano hayo ya marathon kwa wanaume na wanawake yenye urefu wa kilomita zaidi ishirini na moja ambayo yalianzia katika hotel ya Tabora Orion.

Pamoja na pongezi hizo kwa mashindano hayo yaliyofanyika kwa siku moja,mkuu huyo wa mkoa alikiri kuwepo kwa vipaji vingi mkoani Tabora licha ya kuwa hakuna taasisi yoyote inayojitokeza kusaidia michezo ikiwemo serikali yenyewe jambo ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa kurudisha nyuma au kudidimiza vipaji vya wanamichezo mkoani humo.

Aidha Fatma Mwassa aliweka bayana kuwa ni aibu kwa serikali kushindwa kutenga bajeti ya kusaidia michezo katika fani mbalimbali mkoani humo na kuacha sekta hiyo ikidumaa kwa kasi.

Kwaupande mwingine Mkuu huyo akayageukia makampuni yanayonunua zao la Tumbaku mkoani humo kuhakikisha yanajitokeza katika kuchangia michezo.

"Haya makampuni yamekuwa yakipata faida kubwa na kuwaacha wakulima wakiendelea kuwa masikini lakini hatuoni yakisaidia hata sekta ya michezo,kwahiyo mwakani tutayabana nayo yaweze kushiriki kuchangia kiasi katika michezo''alisema Fatma Mwassa kabla ya kutoa zawadi kwa washindi wa mashindano hayo ya Tabora Marathon.

Katka mashindano hayo Rose Seif alishika nafasi ya kwanza kwa wanawake na kujinyakulia kiasi cha shilingi laki moja,wakati Salima Mgazi alishika nafasi ya pili na kupata shilingi elfu sitini na huku Naomi Samwel akishika nafasi ya tatu na kupata shilingi elfu hamsini.

Kwaupande wa wanaume Dickson Mkami ambaye ni mwalimu wa Shule ya sekondari Lutende ya wilayani Uyui alishika nafasi ya kwanza na kufanikiwa kupata shilingi laki moja,mshindi wa pili Salum Majd ambaye ni askari wa jeshi la wananchi JWTZ alijinyakulia shilingi elfu sitini wakati mshindi wa tatu ni Kulwa Charles kutoka kijiji cha Masagala manispaa ya Tabora alijinyakulia shilingi elfu hamsini.  

Hata hivyo Kampuni ya Kishen Enterprises mbali na ufadhili kwa mwaka huu tayari imekwisha thibitisha kudhamini tena mashindano hayo kupitia kutangaza bidhaa za TOYO zikiwemo pikipiki.

No comments: