Pages

KAPIPI TV

Tuesday, March 13, 2012

MBUNGE WA VITIMAALUM TABORA Mh.MUNDE JENGO ATOA MSAADA WA VITU VYENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI MIL.25"Walemavu nao wafaidika kwa viti 25 vya magurudumu matatu.Ameahidi mshahara wake kugawana na walala hoi"


Mbunge wa viti maalum mkoa wa Tabora Bi.Munde Jengo amesema kuanzia sasa atakuwa tayari mshahara wake anaoupata atakuwa akigawa  na  walalahoi ikiwa ni hatua ya kufikia lengo la kuwasaidia wananchi wenye maisha magumu wa mkoa wa Tabora katika kuwainua kiuchumi.

Kauli hiyo ameitoa katika mkutano wa hadhara wakati akizungumza na wananchi wa mjini Tabora,ambapo pamoja na mambo mengine  mbunge huyo akaidhihirisha kauli yake kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani zaidi ya shilingi milioni ishirini na tano katika makundi ya watu mbalimbali.

Misaada aliyoitoa mbunge huyo ni pamoja na mabati bandle 25,mifuko 90 ya saruji,mashine tatu za kufyatulia matofali,mchanga tani 210,vitabu kwa ajili ya shule za sekondari,viti 100 vya plastiki na viti 25 vya magurudumu matatu kwa ajili ya walemavu.

Aidha Bi.Munde alitoa mchanganuo katika msaada huo, ambapo mabati hayo bandle 25 yatatumika katika miradi ya ujenzi wa ofisi za ccm za kata mbalimbali mjini Tabora, wakati saruji mifuko 90,mchanga tani 210 na mashine za matofali  itasaidia mradi wa kufyatua matofali wa jumuiya ya umoja wa vijana.

Kwa upande mwingine Bi.Munde alisema mbele ya hadhara hiyo kuwa viti mia moja vya plastiki ni kwa ajili ya mradi wa jumuiya ya U.W.T ambavyo watakuwa wakivikodisha na kujiongezea kipato.

Aliongeza kusema kuwa hakuna jambo zuri linaloweza kuweka sawa maisha ya wananchi pasipo elimu hivyo ametoa msaada wa vitabu kwa shule za sekondari.

Hata hivyo aliweka wazi kwa kuwasaidia jamii ya watu wenye ulemavu ambao aliwapatia viti 25 vya magudumu matatu huku akieleza kuwa jamii ya watu hao wamekuwa wakisahalika mara kwa mara na hivyo kujikuta kuwa wanyonge wakati wote wa maisha yao.

Jitihada za mbunge huyo katika mkutano huo zikaungwa mkono baadhi ya wadau wa maendeleo ambapo Meya wa manispaa ya Tabora Bw.Ghulam Dewij aliwapatia walemavu hao kiasi cha shilingi elfu hamsini kila mmoja ili wafungue biashara ndogondogo sambamba na kutoa mifuko kumi  na tano ya saruji kwa ajili ya mradi wa kufyatua tofali.

Wadau wengine waliomuunga mkono mbunge huyo Bi.Munde Jengo,ni pamoja na Bw. Deo Kahumbi ambaye ni diwani mstaafu wa kata ya Ipuli manispaa ya Tabora kwa kutoa shilingi laki tatu kwa jumuiya ya U.W.T, wakati mfanyabiashara maarufu mkoani Tabora Bw.John Mchele akatoa mifuko kumi ya saruji.

Bi.Munde sambamba na hilo pia alitoa taarifa ya msaada mwingine wa shilingi laki moja uliotolewa na kada wa CCM aliyemuita kuwa mpiganaji Bw. Hussein Bashe.        













No comments: