INADAIWA kuwa,Wachina wamechangia kufubaza Biashara ya
vitenge Mkoa wa kigoma na kupelekea kushuka kwa makusanyo ya kodi za Forodha na
hivyo Mamlaka ya Mapato Tawi la Kigoma kushindwa kufikia lengo la kukusanya kiasi cha milioni 643,300,000
kwa kipindi cha Julai-Septemba 2014.
Akifafanua hilo mbele
ya wandishi wa habari jana katika ofisi ya mamlaka hiyo Kaimu Meneja
wa tawi Patrice Mushi alisema serikali idhibiti uingizaji holela wa bidhaa kutoka nje
ya nchi ambapo, makampuni ya kichina hutumia
sera ya biashara huria hufoji bidhaa mbalimbali na hivyo kupunguza kasi ya
walaji kutumia bandari ya kigoma
kuchukua vitenge kutoka nchi za magharibi .
“wachina wameua soko la vitenge ,makusanyo halisi ya forordha ni milioni 1,062,806,736 bidhaa
hii ndio chachu ,bidhaa ya mafuta si tija kwetu haitabiriki sasa vitenge
vya wax feki za wachina wadau wanatumia bandari ya
Dar-es-salaam na wanauza hapo serikali isimamie kanuni,tratibu tunakwama
“alibainisha Mushi.
Pia alisema TRA kigoma imejiwekea mkakati wa kuimarisha
ukusanyaji wa kodi kupitia mfumo wa kisasa(EFD),vitalu(Block management system)
sanjari na kuendelea kuhamasisha wananchi wadai risiti wakati wanaponunua
bidhaa madukani,ili kuzuia ukwepaji wa kulipa kodi kwa walengwa.
Aidha alisema wafanyabiashara wenye mtaji wa kuanzia milioni
14 wanahitajika kutumia mfumo wa kisasa wa( EFD) na kuahidi kufuatilia
wasiotumia ipasavyo mashine hizo na adhabu kwa walaji wasiodai risiti za bidhaa
walizonunua kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2000 na kuzuia bidhaa haramu kwa
walaji.
Hivyo makusanyo ya kodi kwa mwaka 2013/14 wamekusanya kodi
za forodha kiasi cha sh.bilioni 2.9
ambapo lengo ilikuwa wakusanye bilioni 3.2 sawa na 91% ya ufanisi,huku kodi za
ndani wamefanikiwa kukusanya sh.bilioni 6.2 ambapo lengo likiuwa kiasi cha
sh.7.179,400,000 sawa na 87%.
Kwa upande wauza vitenge soko la kigoma mjini na mwanga Ally
Kisala na Tatu Amani kwa nyakati tofauti wakiri hali tete katika uzaji wa vitenge
kutoka nchi ya DRC-kongo ,kutokana na bidhaa hiyo kushikwa na wachina ambao
hutumia bandari ya Dar-es-salaam kwa bei
rahisi .
Awali walikuwa wakiuza vitenge pande tatu 500 kwa mwezi
,ambapo hivi sasa wanauza pande tatu 20 kwa mwezi,hali inayowalazimu washindwe
kuagiza kwa wingi bidhaa hiyo kutoka nchini Congo ,ambapo wax kupitia kongo huuzwa sh.27,000 cha Dar-es-salaam sh.19,000.
Walisema ugumu wa maisha unachangia walaji wengi kuvamia
vitenge kutoka china ambavyo vina bei rahisi ilihali havina viwango vya ubora
na kushauri walaji wathamini ubora wa
bidhaa ili kuepukana na bidhaa rahisi ambavyo ni gharama kwa badae (uimara
mdogo).
No comments:
Post a Comment