Pages

KAPIPI TV

Tuesday, July 10, 2012

TABORA YANUKA KWA MAUAJI YA RAIA WASIO NA HATIA"Mke na Mume wauawa kwa kukatwa mapanga,ni unyama uliofanyika mbele ya mtoto wao"

 Askari wa Jeshi la Polisi Tabora,Masesa (aliyevaa suti) akikagua mauaji hayo yaliyotokea katika kijiji cha Inala eneo la kata ya Ndevelwa manispaa ya Tabora.

 Mkuu wa wilaya ya Tabora Bw.Suleiman Kumchaya akizungumza na wakazi wa kijiji cha Inala wakati wa tukio la mauaji hayo.


 Mkuu wa wilaya ya Tabora mjini Bw.Kumchaya  akipata maelezo mafupi kutoka kwa mtoto wa marehemu hao Bi. Zainabu Khalid kuhusu tukio hilo lililofanyika mbele ya macho yake na kushuhudia unyama huo dhidi ya wazazi wake.


TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI 

Katika tukio lililokuwa si la kawaida watu wawili mke na mume wameuawa kwa kukatwa katwa mapanga hadi kufa katika kijiji cha Inala kata ya Ndevelwa manispaa ya Tabora.

Tukio hilo la kinyama linalodaiwa kufanyika majira ya saa moja jioni nyumbani kwa marehemu hao wawili raia wasio kuwa na hatia,imeelezwa kuwa waliouawa ni Kharid Said(50) na mkewe Amina Ally(53) .

Akizungumza na mtandao huu mtoto wa marehemu hao Bi.Zainabu Kharid alisema majira hayo ya saa moja jioni jana ,watu wawili wakiwa na mapanga walifika hapo nyumbani kwao na kuanza kumshambulia baba yake(Kharid) na mara baada ya mama yake(Amina) kujaribu kuuliza kulikoni,watu hao walianza kumpiga mke wa marehemu kwa kutumia fimbo hali  iliyofanya Zainabu na yeye kujaribu kuwasaidia wazazi wake akapigwa pia fimbo iliyompata mkononi.

Unyama huo haukishia hapo waharifu hao waliendeleza unyama huo kwa kuwakamata Kharid na mkewe Amina na kuwapeleka ndani na kuzidisha mashambulizi kwa kuanza kuwakatakata kwa mapanga hadi kufa.

Zainabu ambaye kwa mujibu wa maelezo yake,alizuiliwa kuingia ndani ambako wazazi wake walikuwa wakiendelea kusurubiwa kwa  mapanga maeneo mbalimbali ya miili yao na hivyo aliamua kwenda kuomba msaada kwa majirani ambao walifika huku nao wakiwashuhudia wauaji hao wakiondoka taratibu bila woga.

Hata hivyo Zainabu alipoulizwa na mkuu wa wilaya ya Tabora kuhusu mauaji hayo,alisema kumekuwa na ugomvi wa muda mrefu baina ya wazazi wake na mjomba wake yaani kaka wa mama yake kuhusu mogoro wa ardhi na hata kufikia huyo mjomba wake ambaye amefahamika kwa jina la Mheshimiwa Maganga Ally kuahidi kufanya mauaji kutokana na mzozo huo.

''Mi naamini kuwa hao watu walitumwa na mjomba kwani hata mchana niliwaona alikuwa amewabeba kwenye pikipiki na ukizingatia baba alikuwa ametoka mahakamani kufungua kesi dhidi ya kauli hizo za mjomba ambaye alikuwa akimtishia kumuua mara kwa mara"alisema Zainabu

Aliongeza kwa kusema kuwa"Baba aliwahi kwenda kushitaki polisi lakini mjomba akamwambia yeye hawezi kufanywa chochote kwani Polisi wote amewashika mkononi yaani anatumia fedha zake"

Mkuu wa wilaya ya Tabora Bw.Suleiman Kumchaya,kufuatia tukio hilo amviagiza vyombo vya dola kuwasaka wauaji hao ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.

Hadi sasa Jeshi la Polisi linamshikilia Mheshimiwa Maganga Ally kwa kuhusika na tuhuma za mauaji hayo.     

 
Post a Comment