Afisa utamaduni manispaa ya Tabora Mark Katunzi akitoa zawadi kwa mchezaji bora wa mashindano ya PoolTable kwa mkoa wa Tabora Waziri Ally ambaye ni mchezaji wa timu ya Texas ya mjini humo ambayo imejinyakulia ubingwa wa mkoa wa Tabora,Waziri Ally amepata shilingi laki tatu na hamsini elfu wakati timu yake katika Fainali ya michuano hiyo imejinyakulia kitita cha shilingi laki saba taslimu,Mashindano yanayodhaminiwa na kampuni ya bia nchini TBL.
Mratibu wa mashindano ya PoolTable kwa mkoa wa Tabora Joseph Kessy wakati akizungumza katika zoezi la kuhitimisha Fainali ya mashindano hayo yaliyozishirikisha timu sita kutafuta bingwa atakaye wakilisha mkoa katika mashindano ya mchezo huo kitaifa ambayo yanatarajiwa kufanyika jijini Mwanza hivi karibuni.Mwakilishi wa kampuni ya bia TBL mkoa wa Tabora Diamond Mawani akizungumzia namna TBL ilivyojipanga katika kuibua vipaji kwa wachezaji wa mchezo wa PoolTable nchini.
Mwenyekiti wa Chama cha PoolTable mkoani Tabora Nabil Hizza akitoa tathimini ya namna mashindano yalivyoendeshwa kutafuta klabu bingwa ya mkoa wa Tabora katika ukumbi wa Frankmann Hotel.
Afisa Utamaduni Manispaa ya Tabora Mark Katunzi wakati akitoa nasaha kwa wachezaji wa PoolTable walioshiriki katika mashindano hayo.
Mmoja kati ya wachezaji wa mchezo huo kwa wanawake mkoani Tabora ambaye alishiriki mashindano hayo Angela Mfaume akipokea shilingi elfu hamsini zawadi.
Salma Hussein mchezaji wa PoolTable Tabora akipokea zawadi ya shilingi elfu hamsini.
Waziri Ally mchezaji wa timu ya Texas ya mjini Tabora akionesha kitita cha shilingi laki tatu akiwa ni mchezaji bora katika mashindano ya PoolTable mkoa wa Tabora.
Baada ya kumaliza fainali mambo yaliendelea kuwa mazuri katika kufurahia na TBL kwa kuboresha maisha ya wachezaji wa PoolTable.
Mchezaji Salma Hussein akiwa makini katika mashindano hayo
Hiki ndio kikosi kamili cha wachezaji wa timu ya Texas iliyoibuka mshindi katika mashindano ya PoolTable kwa mkoa wa Tabora,Texas itashiriki mashindano ya Taifa ya mchezo huo jijini Mwanza.
No comments:
Post a Comment