Pages

KAPIPI TV

Saturday, October 27, 2012

BAADHI YA WATOTO TABORA HATARINI KWA PICHA ZA NGONO KWENYE MTANDAO

Hii sasa ina ashiria hatari kwa watoto kutumia muda mwingi katika kuperuzi picha za ngono kwenye mtandao.

Kwa mara ya kwanza nilipokuwa nikifika kwenye Internet Cafe ili niweze kuangalia mambo mbalimbali yaliyojiri ulimwenguni,nilikuwa nikishuhudia watoto nao wanaingia na kuomba muda wa kuperuzi kwenye mtandao kwa muhudumu kati ya dakika 30 hadi dakika 120.

Suala la kulipia muda huo kwa watoto niliobahatika kuwaona haikuwa shida sana,na kila ninapowakuta kwenye kompyuta wanakuwa bize sana hali iliyonilazimu nianze kuwafuatlia na kutaka kujua nini wanafanya kwenye mitandao hiyo.

Wapo niliowakuta wakiangalia picha za wachezaji wa mpira wa miguu na wasanii maarufu duniani,hilo halikunipa shida kama lile la baadhi yao tena waliowengi walikuwa wakitumia mitandao ya kijamii kama FACEBOOK. 

Nilipojaribu kumuuliza mmoja niliyekumbana nae,..hakuwa tayari kunijibu bali alikuwa kimya huku akizidi kuangalia kile kilichomleta hapo kwenye Internet Cafe.

Kwakuwa jicho halina mpaka,na kwa vile nimekaa kwenye kiti kilichopo jirani naye, nilijionea kitu ambacho sikufikilia kama mtoto mdogo kama yule angeweza kutafuta mambo makubwa kama hayo kupitia mtandao wa Google.

Ni picha za Ngono,tena chafu zisizosatahili hata kuangaliwa na mtu mzima tena mwenye akili timamu.

Pasipo shaka yoyote mtoto huyo aliendelea kujivinjali kwenye picha hizo zikiwemo za mnato na zile za video.

Jamani,jamani,jamani,......tena kibaya zaidi nikamsikia vizuri akimlalamikia yule mhudumu wa Cafe hiyo..."Dada mbona hii kompyuta haina sauti,...sasa mi ntaangaliaje video za bila sauti?''alikuwa akisema mtoto huyo wakati akiangalia kupitia Youtube huku akionesha kana kwamba ile ilikuwa haki yake ya kimsingi ambayo hajatekelezewa.

Hofu yangu watoto wetu wanaingia hatarini muda si mrefu kutokana na jambo hili.         
Post a Comment