Pages

KAPIPI TV

Tuesday, October 23, 2012

WANAFUNZI ADAIWA KUUA KWA KUDAIWA KUDHULUMIWA SHS,5,000-SERENGETI

Na Antony Mayunga-Serengeti
MWANAFUNZI wa kidato cha pili sekondari ya Mugumu wilayani Serengeti
Mwang’omba Kegocha(16)anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma ya
kumchoma kisu Chacha Pasta(29)baada ya kudaiwa kudhulumiana ths 5,000
kwenye kamali.

Tukio hilo linadaiwa kutokea oktoba 20 majira ya saa 1:30 usiku mwaka
huu katika eneo la mtaa wa Sedeko wakati wanacheza kamali
limethibitishwa na polisi wilayani hapa.

Kwa mjibu wa habari za kipolisi na mashuhuda mbalimbali inadaiwa kuwa
mtuhumiwa alimchoma kisu ubavu wa kushoto na kufa papo hapo baada ya
marehemu kumpiga kofi mtuhumiwa ambaye alimdai tsh,5,000=ambazo
inadaiwa alikuwa anamdai.

Habari hizo zinasema kuwa kitendo cha kupigwa kofi kilimfanya
mtuhumiwa kukimbilia nyumbani kwao na kuwaacha wenzake akiwemo
Marehemu wakicheza kamali na aliporudi wakati hana taarifa alifika na
kumchoma bila kusema neno lolote.

Inasemekana baada ya kutenda unyama huo marehemu hakuweza kunyanyuka
na kufa papo hapo na waliokuwa wakicheza naye kukimbia ,huku mtuhumiwa
naye akikimbia na kwenda kujificha.

“Alikimbilia mitaa ya vilabuni na kujificha ,hata hivyo kutokana na
ushirikiano wa jeshi la polisi na wananchi walifanikiwa kumkamata
mtuhumiwa huyo”alisema shuhuda mmoja.

Ili kuhakikisha wanapunguza matukio hayo ya watu kuchomana visu jeshi
hilo limeanzisha kitengo maalum cha kutoa elimu kwa jamii ,ikiwa ni
pamoja na kuwawezesha kufuata sheria.

No comments: