Pages

KAPIPI TV

Saturday, March 10, 2012

POLISI WAUA MAJAMBAZI WATATU TABORA"Walivunja nyumba ya mfanyabiashara kwa jiwe la FATUMA wakiwa na silaha SMG na risasi 20"

Wakazi wa mjini Tabora wakiangalia miili ya watu watatu wanaodaiwa kuwa ni majambazi ambayo imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete.
 Miili ya watu hao wanaodaiwa kuwa ni majmbazi  Abutwalib Issa,Fredrick Manase na Eliya ambaye ndio imedaiwa kuwa ni mmiliki wa silaha hiyo anaishi wilayani Mpanda.
 Mwili wa Abutwalib Issa(32)au Twaha kama alivyokuwa akifahamika kuwa ni jambazi sugu anayetumia silaha za kivita.
 Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora  S.S.P Yusuph Mruma akiwaonesha waandishi wa habari silaha aina ya SMG waliyokuwa wakiitumia majambazi katika tukio hilo.


Jeshi la polisi mkoani Tabora limewaua kwa kuwapiga risasi watu watatu wanaodaiwa kuwa ni majambazi  ambao walivamia nyumba ya mfanyabiashara mmoja kata ya Ipuli mjini Tabora wakiwa na silaha bunduki aina ya SMG.

Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora S.S.P Yusuph Mruma amewaeleza waandishi wa habari kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa nane usiku ambapo watu hao watatu walifika nyumabni kwa mfanyabiashara huyo na kuvunja  mlango wa nyumba yake kwa kutumia jiwe kubwa maarufu FATUMA baada ya kufyatua risasi hewani.
Aidha Mruma alisema kwakuwa askari Polisi tayari walikuwa wanataarifa za uvamizi huo walijipanga tayari kwa kukabiliana nao majambazi hayo ambayo yamekutwa na risasi zaidi ya ishirini.
Hata hivyo katika mapambano hayo majambazi mawili yakufa papo hapo huku jambazi moja lilijeruhiwa vibaya na kujificha katika kichaka.

Kwa mujibu wa maelezo ya Kaimu kamanda Mruma,ilipofika asubuhi askari Polisi waliokuwa katika mapambano hayo walimpata jambazi huyo ambaye alitoa siri yao na matukio kadhaa ambayo tayari wameshiriki mkoani Tabora na maeneo mengine.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa mmoja wa majambazi hayo aliyefahamika kwa jina la Abutwalib Issa ni mkazi wa ng'ambo manispaa ya Tabora huku Fredrick Manase akitambuliwa kuwa ni mwenyeji wa Kahama na mwingine ni Eliya ambaye inadaiwa kuwa ndio mmiliki wa silaha hiyo.    
Post a Comment