Pages

KAPIPI TV

Sunday, March 11, 2012

MCHUNGAJI MBAGATTA ACHOMA HIRIZI ZA MAJAMBAZI WALIOUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA POLISI"Kanisa lapongeza jeshi la Polisi kwa kuokoa roho za waumini wake"

 Mch.ELIAS MBAGATTA:Akichoma hirizi za majambazi watatu waliouawa katika mapambano ya kurushiana risasi  kati yao na askari wa jeshi la polisi mjini Tabora,majambazi hayo yaliyokuwa yakitumia silaha aina ya SMG ikiwa na risasi zaidi ya ishirini yalikutwa na hirizi baada ya kufariki kufuatia kipigo hicho.
Mchungaji Mbagatta wa kanisa la Injili Afrika Agape Tabora akiwaombea waumini wake Bw.Enocent Joram na mkewe baada ya kusalimika kufuatia tukio la kuvamiwa na majambazi huko kata ya Ipuli manispaa ya Tabora. 
 
Mke wa Enocent akitoa maochozi kanisani wakati yeye na mumewe wakitoa ushuhuda wa tukio hilo ambalo wao walisalimika.
Mchungaji Mbagatta akifungua Hirizi mbele ya waumini wake katika kanisa lake iliyokuwa imeokotwa baada ya kuuawa majambazi hayo.

 Maiti za majambazi hayo ambayo yalifahamika kwa majina ya Abutwalib Issa mkazi wa Ng'ambo manisapaa ya Tabora,Fredrick Manase mkazi wa Kahama na Eliya mkazi wa Katumba wilayani Mpanda,maiti hizo ziliwekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete mjini Tabora

Enocent akihadithia mkasa wa kuvamiwa na majambazi hayo mbele ya Mchungaji na waumini katika kanisa la Injili Afrika lililopo eneo la Mwanza Road Tabora mjini.

"Kwakweli mimi na familia yangu tunamshukuru Mungu kwa kuwawezesha askari Polisi hawa wakiongozwa na RPC wao wamesalimisha maisha yetu, maana la sivyo leo hii hapa kanisani mngekuwa mnafanya ibada ya kutusalia tukiwa maiti"alisema Enocent huku wakitokwa na machozi mbele ya waumini.


No comments: