Pages

KAPIPI TV

Friday, March 9, 2012

KISHEN ENTERPRISES KUDHAMINI TABORA MARATHON"Yatoa Shilingi laki nne kwa washindi"

 Waandaaji wa Tabora Marathon,kutoka kushoto ni Tullo Chambo(mshauri ufundi Tabora Marathon),katikati ni Seraphine Baraka Meneja masoko Kishen Enterprises Ltd, 
 Viongozi wa Chama cha riadha mkoa wa Tabora pamoja na waandishi wa habari katika kikao cha pamoja kilichofanyika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini humo.

Kampuni inayojihusisha na uuzaji wa pikipiki za aina mbalimbali nchini Kishen Enterprises imetoa udhamini katika mashindano ya riadha yaliyopewa jina la Tabora Marathon ambayo yanafanyika mjini Tabora tarehe 10 machi 2012.

Meneja  masoko wa kampuni ya Kishen Enterprises, Seraphine Baraka amewaambia waandishi wa habari mjini Tabora kuwa, Tabora Marathon imelenga zaidi kuibua vipaji kwa wanariadha walioko mkoani humo pamoja na kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko mkoani humo.

Seraphine amesema kampuni hiyo mbali na kutenga  kiasi cha shilingi laki nne kwa ajili ya washindi lakini pia imetoa zaidi ya t.shirt mia moja kwa ajili ya washiriki wa mashindano hayo.

Aidha alifafanua kiasi cha zawadi zitakazotolewa kwa washindi ni mshindi wa kwanza kwa upande wa wanaume na wanawake watajinyakulia kiasi cha shilingi laki moja taslimu,ambapo mshindi wa pili atapata kiasi cha shilingi sitini elfu.

Kwa upande wa washindi wa tatu watapata shilingi elfu hamsini huku mshindi wa nne hadi wa kumi watapata kifuta jasho shilingi elfu kumi kila mmoja.    

No comments: