Pages

KAPIPI TV

Friday, July 6, 2012

JESHI LA POLISI TABORA LAJIZATITI KUDHIBITI AJALI ZA BODABODA

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Anthony Rutha akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake mjini Tabora.

Hastin Liumba,Tabora

KAMA ilivyo katika mikoa mingine hapa nchini, mkoa wa Tabora haujabaki
nyuma katika mjumuiko wa ongezeko la kasi la pikipiki zinazoendesha
biashara ya kusafirisha abiria.

Ni ukweli usiopingika kwamba usafiri wa pikipiki umepunguza tatizo la
usafiri katika mkoa wetu wa Tabora mijini na vijijini na hasa hasa kwa
wananchi wenye kipato cha kati na cha chini.

Usafiri huu umekuwa ukitumiwa na baadhi ya watumishi wa serikali
waendapo na kutoka ofisini na pia wananchi wanaohitaji usafiri wa
haraka kutoka eneo moja hadi jingine.


Lakini hata hivyo usafiri huu umekuwa ukisababisha ongezeko kubwa la
ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani, ikiwa ni pamoja na ajali
mabalimbali na uhalifu mwingineo.

Sababu zinazochangia waendesha pikipiki kuwa chanzo cha ongezeko la
makosa ya usalama barabarani hapa mkoani Tabora ni pamoja  ni nyingi.

Kamanda wa jeshi la polisi,mkoani Tabora, Antony Rutta, alifanya
mahojiano na mwandishi wa makala hii na kuelezea jinsi jeshi la polisi
lilivyojipanga kukabiana na changamoto mbalimbali ikiwemo utoaji wa
elimu kwa waendesha pikipiki hizo maarufu kama bodaboda.

Rutta alianza kwa kueleza sababu mbalimbali zinazosababisha vijana
waendeshao bodaboda wanavysababisha ajali kuwa ni pamoja na baadhi ya
waendesha pikipiki kutokuwa na elimu na ujuzi wa kutosha juu ya sheria
za usalama  barabarani.

Kamanda anaongeza kuwa sababu nyingine ni pamoja na baadhi ya
waendesha  pikipiki kutokuwa na leseni zinazo waruhusu
kuendesha pikipiki hizo.

Aidha alisema wapo baadhi ya vijana ambao hujifunza pikipiki kwa masaa
machache na pengine kwa siku moja kesho yake anachukua au anapewa
pikipiki na kuingia mitaani na kuanza  kutafuta abiri wakati bado
hajawa na ujuzi na uzoefu wa kutosha kufanya shughuli hiyo.

Alieleza zaidi kuwa baadhi ya waendesha pikipiki kuendesha pikipiki
hizo wakiwa wamelewa,huku baadhi yao wakiendesha pikipiki kukiuka kwa
makusudi sheria za usalama barabarani.

Aidha naeleza zaidi kuwa baadhi ya waendesha pikipiki kuendesha
kutumia pikipiki ambazo
wanajua fika kuwa ni mbovu katika shughuli zao za biashara na matokeo
yake kusababisha ajali.

Kamanda Rutta anafafanua kuhusu ajali zilizotokea katika kipindi cha
kuanzia mwezi January hadi Juni 2012 jumla ya makosa ya  ukiukwaji wa
sheria za usalama barabarani mkoani Tabora.

Alisema makosa ambayo yaliyofanywa na waendesha pikipiki,ni 2,083.
kati ya makosa hayo jumla ya makosa 1,683 yalilipiwa faini kwa njia ya
"Notification" ambapo jumla ya sh milioni 47,910,000  zimekusanywa .

Aidha anaongeza kuwa matukio mengine 400 wahusika walirekebishwa ikiwa
ni pamoja na kupewa onyo kali kulingana na uzito wa makosa
waliyoyatenda.

‘‘Makosa 1,683 yalilipiwa  faini kwa njia ya "Notification" ambapo
jumla ya sh milioni 47,910,000 zimekusanywa’’.

Kamanda Rutta anafafanua zaidi kuwa matukio mengine 400 wahusika
walirekebishwa na waendesha pikipiki 85 na ajali hizo zimesababisha
vifo vya watu 13 na majeruhi 76.

‘‘Katika kipindi hicho hicho cha January hadi Desemba 2012, jumla ya
ajali zilizosababishwa na waendesha pikipiki ni 85 na ajali hizo
zimesababisha vifo vya watu 13 na majeruhi 76”.alisema kamanda Rutta.

Akizungumzia matatizo yanawakumba kamanda Rutta alisema, waendesha
pikipiki wajulikanao kwa jina maarufu kama "boda boda" wamekuwa
wakikumbana na matatizo mablimbali wakiwa wanaendelea na biashara zao.

Akitaja matatizo hayo Rutta altaja kuwa  kwa kipindi cha January hadi
juni 2012, wamekumbwa na changamoto kadhaa ikiwemo kutekwa na
kunyanganywa pikipiki zao na wakati mwingine kuuwawa.

Aidha aliongeza kuwa matatizo mengine ni pamoja na wakati wakiendesha
shughuli zao, kwa kipindi cha January – Juni 2012, yameripotiwa
matukioa saba ya kunyanganywa pikipiki na kutokana na matukio haya
waendesha pikipiki watatu wameuwawa.

Aidha matatizo mengine ni kujeruhiwa na watu/wateja wasiowaaminifu na
wenye nia ovu wakati wakiendesha biashara zao.

Alifafanua zaidi  kwa kipindi cha Januari hadi Juni,2012, yameripotiwa
matukio mawili ya katika kipindi cha nyuma kulikuwepo na matukio ya
kutegewa kamba njiani na hasa nyakati za usiku na makundi ya watu
wenye nia ovu dhidi ya waendesha pikipiki hao.

Alisema matukio hayo katika kipindi cha Januari hadi julai,2012,
hakuna tukio lililojitokeza la kuwekwe kamba njiani.

Mikakati ya jeshi la polisi inayofanywa kupunguza ajali na kudhibiti
makosa ya usalama brabara na uhalifu.

Kamanda Rutta alisema kuwa jeshi la polisi linatoa elimu kwa waendesha
pikipiki,faida ya utii wa sheria bila  shuruti .

Alisema kuwa jeshi la polisi linatoa elimu kwa waendesha pikipiki kwa
kutumia vyombo
vya  habari mbalimbali na pia kupitia mikutano mbalimbali inayofanyika
baina ya waendesha pikipiki na viongozi wa jeshi la polisi mkoani
hapa.

Aidha Rutta anaongeza kuwa mkakati mwingine wamekuwa wakitoa elimu kwa
askari wa usalama barabarani wanapo kuwa doria,na elimu hutolewa
katika kituo cha polisi wakati wanapo kuwa wamekamatwa kutokana na
makosa mbalimbali.

Aidha aliongeza jeshi la polisi limekuwa likitoa elimu  kwa utaratibu
kwa kuwafuata katika maegesho yao,ambapo elimu inayotolewa ni pamoja
na kuwataka wawe na leseni ya udereva na wavae sare.

Aidha pia wamekuwa wakiwaasa kuwa na umoja ambao utawasaidi kupunguza
matatizo wanayokumbana nayo barabarani, na kutolipwa fedha na mteja
wake ama kuwayang'anya pikipiki , kujeruhiwa na wakati mwingine kuuawa
na majambazi ambayo hujifanya ni wateja.

Alisema hatua hizo ana imani zitasaidia kuwabaini waendesha pikipiki
ambao siyo waadirifu,ambao huwapeleka abiria sehemu zisizo husika na
kuwanyanga'nya  mali zao, kuwabaka akina mama  na hata kuwaua.

‘‘Kuna matukio mawili ya mfano ya waendesha pikipiki hizo hivi
karibuni mteja mmoja alikodi pikipiki moja akiwa ana mfuko wa samaki
pamoja na vitu mbalimbali walipofika karibu na duka fulani hapa hapa
mjini Tabora abiri huyo alimtaka asimame ili anunue vitu vinginezaidi,
abiria huyo alipoteremka tu kijana huyo mwendesha pikipiki aliondoka
pamoja na mizigo ya mteja wake.” Aliongeza.

Alisema bodaboda huyo kwa vile hakuvaa sare wala hakuwa na utambulisho
hakutambulika mpaka sasa .

Aidha aliongeza tukio jingine ni mwendesha pikipiki mmoja ambaye
alichukuliwa na mteja hapa hapa mjini akapelekwa pembeni ya mji na
akauawa kisha akatobolewa macho yote.

‘‘Haya yote yasingetekelezwa kwa urahisi iwapo wangekuwa katika umoja
naamini wangekuwa  katika taratibu za utendaji  isingekuwa rahisi kwa
waovu hao kutekeleza maovu hayo”.alisema.

Hata hivyo alisema elimu inaendelea kutolewa hadi vijijini katika
wilaya zote, kwa kushirikiana
na  wenye viti wa vitongoji na madiwani ambao wanatoa ushirikiano
mkubwa kwa kuwahamasisha wananchi hadi vijijini ili na wao elimu
iwafikie.

Alieleza zaidi kuwa wamekuwa wakiwahimiza hawa waendesha pikipiki za
biashara wapatapo wateja au abiria wkati wa usiku wajenge tabia ya
kusindikizana kwa lengo la kujihakikishia usalama wa maisha yao na
pikipiki zao dhidi ya wateja au abiria ambao sio waminifu na
waadilifu.

Alisema jeshi la polisi linatumia na litaendelea kutumia umoja wa
waendesha pikipiki kama kikundi maalumu cha kukabiliana na uhalkifu na
wahalifu mkoani Tabora.

Alifafanua kuwa shughuli hizi zinafanywa na wandedha pikipiki zinzttoa
mchango mkubwa kwa wananchi Tabora na nchi kwa ujumla na kwa kiasi
kikubwa inapunguza kujihusisha na matukio ya kihalifu.

Hata hivyo kamanda Rutta alisema amekuwa akitoa ushauri kwa waendesha
pikipiki hizi kuwa wanapaswa kuzingatia sheria za usalama barabarani
kwa lengo la kupata ufanisi katika biashara zao.

Aidha aliongeza kutoa wito kwa wamiliki wa pikipiki bodaboda hizo kuwa
kabla hawajakabidhi kijana yoyote pikipiki kwa ajili ya biashara,
wahakikishe kuwa kijana huyo anayo leseni,ujuzi na uzoefu wa kutosha
katika uendeshaji wa pikipiki.

Alisema hatua hiyo itasadia sana kuepusha ajali nyingi,pamoja
waendesha pikipiki wasio waaminifu ama wale wanaotumiwa na vikundi vya
kihalifu.

No comments: