Mradi wa
ujenzi wa Gati katika mwalo wa kibirizi katani humo mkoani hapa,upo
mashakani kuanza kwake ,kutokana na wahanga wa eneo hilo wapatao 53 kuipa siku 30
Manispaa ya kigoma ujiji ili kuboreshewa
stahiki zao kwa mujibu wa
Sera na Sheria ya Ardhi husika.
Hayo yalisemwa juzi na mwanasheria wa kujitegemea Daniel
Rumenyela katika ofisi za chama cha wandishi wa habari mkoani hapa,akiwakilisha
adha za wananachi hao, juu ya ufinyu wa fidia usiozingatia sheria ya ardhi ya
mwaka 1999 .
“uthamini ulifanyika
2012 na malipo 2014,kifungu cha( 5),( 4 )ya sheria ya ardhi na sera ya ardhi inataka fidia itolewe kwa
wakati na haraka kwa wahanga na ikichelewa
tathimini ifanywe kila
baada ya miezi sita, ili fidia ilingane na hitaji la leo” alibainisha
Rumenyela.
Alisema wamempa siku
30 Mkurugenzi wa manispaa ya kigoma Ujiji ,ili aweze kuboresha haki stahiki za wahusika kwa sheria husika kwa
lengo la kuboresha ustawi wa jamii na maendeleo kwa ujumla.
Meneja wa Mamlaka ya Bandari TPA wa hapa Patrick Namahuta alipohojiwa juu ya hili alisema mchakato wa kufidiwa kwa walengwa ulifanywa na mthamini wa manispaa hiyo kwa mujibu wa sheria husika na wao walitenga bajeti zaidi ya milioni 600 ili kukidhi hitaji la walengwa.
Alisema TPA taifa ilitoa fidia kwa wahanga hao pasipo mkoa kuhusishwa kikamilifu katika kuhakiki picha na akaunti za walengwa, ili anayelipwa akiri ni sahihi na kusisitiza malipo yalifanywa makao makuu na akaunti za wahanga zilipelekwa na manispaa husika.
Namahuta alisema lengo
la mradi huo ni kuboresha huduma kwa wadau,ambapo mwalo wa kibirizi ni chachu kibiashara kwa nchi jirani za Burundi na
jamuhuri ya watu wa kongo(DRC) na
ili kukidhi haja za walengwa kwa ukanda wa ziwa Tanganyika zinahitajika gati 19 ambayo
itaongeza ufanisi kwa mamlaka hiyo.
Mkuu wa wilaya ya hapa Ramadhan Maneno amekiri mchakato
ulifanywa na manispaa husika kupitia mthamini wao na walicholipa TPA ni matokeo
ya uthamini na kusisitiza wananchi walishirikishwa kwa kila hatua na kuwasihi
walengwa wasitake malipo yalingane.
Alisema mfumo mbovu wa malipo
ya fidia hauko vyema, kutokana na
TPA mkoa kutoshirikishwa katika kila hatua na endapo ingeshirikishwa ni rahisi kubaini haki na batili kwa lengo la
kuondoa utata wa fidia hizo kwa wananachi,ambao
wanamtazamo hasi kwa manispaa katika uwajibikaji .
Kaimu Mkurugenzi wa manispaa hiyo Moses Weransari alisema mthamini
alizingatia uhalisia wa thamani za wahanga
na kwa mara ya mwisho kufanya tathimini ilikuwa 2013 na wahanga kulipwa rasmi kupitia akaunti zao ni Juni,2014 .
No comments:
Post a Comment