Na. Paul Marenga-NHIF LINDI
Wananchi wa Kilwa wakiwa kwenye
foleni ya kupata huduma za vipimo kwenye banda la Mfuko wa taifa wa bima
ya afya ambapo huduma za upimajiwa kiwango cha sukari kwenye damu
(RBG),shinikizo la damu (BP),uwiano wa uzito na urefu wa mwili (BMI) na
ushauri wa kitaalamu ulitolewa na madaktari,wakati wa mapokezi ya mwenge
wa uhuru kwenye viwanja vya shule ya msingi Somanga-Kilwa.
Meneja wa mfuko wa taifa wa bima
ya afya mkoa wa Lindi Fortunata Kullaya akitoa taarifa ya utekelezaji wa
zoezi la upimaji afya na mwitikio wa wananchi wa kilwa ambapo takribani
wananchi 257 walijitokeza kupimwa afya na kaya 73 zilijiunga papo kwa
papo na CHF Kwenye banda la mfuko kwa kiongozi wa mwenge kitaifa kwa
mwaka 2014 Rachel Kassanda,ambaye alikagua shughuli mbalimbali
zilizokuwa zikitekelezwa kwenye viwanja vya shule ya msingi somanga
ambapo mwenge wa uhuru ulipokelewa,kulia ni mkuu wa wilaya ya Kilwa
mhe. Abdallah Ulega.
Mnafanya kazi kubwa kuisaidia
serikali katika kutoa elimu kwa jamii kuchangia huduma za afya ili
ziboreke sambamba na upimaji wa afya bure kwa magonjwa yasiyoambukiza
unaomuwezesha mwananchi wa kawaida kupata huduma pasipo
gharama..hongereni sana alisema kiongozi wa mwenge kitaifa Rachel
Kassanda,huku akisisitiza wananchi kutambua CHF ni mali yao hivyo
kujiunga kwao kwa wingi ndiyo msingi wa maboresho ya huduma za afya
hususani upatikanaji wa dawa,kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kilwa
Mhe.Abdallah Ulega,kushoto anayemsikiliza ni Meneja wa NHIF Mkoa wa
Lindi Fortunata Kullaya.
Kiongozi wa mwenge kitaifa mwaka
2014 Rachel Kassanda akiwataka wananchi wa kilwa kujiunga na CHF,kwani
ndiyo mkombozi wa matibabu sasa kwa kuzingatia maboresho ya huduma za
afya yanavyowezekana chini ya sera ya urasimishaji wa majukumu kwa jamii
hususani ya uchangiaji baina ya wananchi na serikali,ambapo mfuko wa
taifa wa bima ya afya unasimamia mfuko wa afya ya jamii kwa niaba ya
serikali ,kulia ni mkuu wa wilaya ya Kilwa mhe.Abdalla Ulega ambaye
ndiye mwenyeji wa mapokezi ya mwenge wa uhuru.
No comments:
Post a Comment