Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye amesema Chama Cha
Mapinduzi hakimzuii mwanachama yeyote kutangaza nia ya kugombea Uongozi
katika muhula unaofuata isipokuwa Chama kimezuia kampeni za mapema kwani
ndio chanzo cha makundi ndani ya Chama akizungumza kwenye kipindi cha
Baragumu kinachorushwa na Channel 10 ,Nape alisema taratibu za kugombea
Uongozi ndani ya chama zipo na kuna Kanuni mbili, moja ni ya Kanuni za
Viongozi na Maadili na pili Kanuni zinazosimamia Uchaguzi ndani ya CCM,
akinukuu kutoka kwenye kitabu cha Kanuni za Viongozi na Maadili ,Nape
alisema “Wanachama wenye nia ya kugombea nafasi ya uongozi katika muhula
unaofuata anaweza kutangaza nia ya kugombea lakini haruhusiwi kufanya
kampeni kabla ya muda”.
Akizungumzia juu ya adhabu wanazopewa waliokiuka alisema adhabu hizi
zina shabaha ya kuwasaidia wanachama na Viongozi kujirekebisha.Nape pia alizungumzia suala zima la upatikanaji wa Katiba Mpya,alisema CCM imeshikamana sana kiasi cha kuwachanganya Wapinzani, aliendelea kwa kusema Kanuni,Sheria zinazotumika ni makubaliano ya wote.(Wapinzani walishiriki katika kamati kutengeneza kanuni na sheria na zikapitishwa Bungeni wakiwemo na Rais akasaini).
Chanzo: kamerayangublog.com
No comments:
Post a Comment