Baadhi
ya Washiriki wa Mkutano wa Tatu(03) wa Umoja wa Taasisi za
Urekebishaji(Magereza) Barani Afrika wakifuatilia Majadiliano ya Mkutano
huo uliofanyika hivi karibuni Maputo, Msumbiji(wa kwanza kulia) ni
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja(wa
kwanza kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Uganda, Dkt.
Johnson Byabashaija(mstari wa nyuma) ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi la
Magereza Nchini Tanzania wakifuatilia mjadala katika Mkutano huo wa
Kimataifa.
Katibu
Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Nchini Tanzania,
Profesa Sifuni Mchome akiwasilisha Mada ihusuyo Urudiaji wa Vifungo
Magerezani kwa Wahalifu(Recividism) katika Mkutano wa Tatu wa Umoja wa
Taasisi za Urekebishaji(Magereza) Barani Afrika uliofanyika hivi
karibuni Maputo, Msumbiji.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, John Casmir Minja akichangia
Mada katika Mkutano wa Tatu(03) wa Umoja wa Taasisi za
Urekebishaji(Magereza) Barani Afrika uliofanyika hivi karibuni kuanzia
July 14 – 17, 2014 Maputo, Msumbiji.
Maafisa
na Askari Magereza wa Msumbiji wakimsikiliza Mgeni rasmi, Rais wa
Jamhuri ya Watu wa Msumbiji, Mhe. Dkt. Armando Guebuza(hayupo pichani)
katika ufunguzi wa Mkutano wa Tatu(03) wa Umoja wa Taasisi za
Urekebishaji(Magereza) Barani Afrika uliofanyika Maputo, Msumbiji.
No comments:
Post a Comment