CHAMA cha
wandishi wa habari Mkoa wa Kigoma,wametakiwa watumie chama chao kujiunga na mfuko wa Afya (Nhif) kwa lengo
la kupunguza
changamoto ya kipato inayochangiwa na kutokuwa na mikataba ya ajira
husika.
Hayo
yalisema na Meneja wa mfuko huo mkoani
hapa Elias Odhiambo alipokuwa akizungumza na wanachama hao kigoma Ujiji ,katika ofisi za KGPC kwa tija ya kutaka watumie fursa ya
huduma ya vikundi ili kunufaika na mafao ya matibabu yatolewayo na mfuko huo.
“ changamoto
kubwa ni uhakika wa kipato,ambapo kupitia huduma mpya ya vikundi rasmi vya
uzalishaji mali ni nafuu kwenu, kujiunga na bima ya afya na kila mwanachama
atachangia sh.76,800 tu kwa mwaka” alibainisha Odhiambo.
Alianisha
huduma ya vikundi ni chachu kwa kila mtanzania kuwa na uwezo wa kuchangia kiasi
hicho kwa mwaka na endapo atahitaji kuongeza hitaji la mtegemezi anapaswa
amchangie kiasi hichohicho,kwa dhati ya kuondoka na adha ya kulipa matibabu ya papo kwa papo.
Alisema
wananchi wote waliopo katika vikundi vidogo na vikubwa ambavyo vipo kihalali ni
wakati wao kutumia fursa hiyo. ambayo inakidhi hali halisi ya maisha ya
mtanzania na kusisitiza wananchi wathubutu hilo kwa faida ya leo na siku za
usoni.
Mwenyekiti
wa Kgpc Deogratius Nsokolo aliunga mkono huduma hiyo ,ambayo ni fursa kwa
wanachama wake,ambao asilimia 99 hawana mikataba ya ajira ,hali inayochangia
washindwe kwenda kupima afya zao kwa wakati .
Alisema wataweka utaratibu,kanuni na sheria kwa kuhakiki kila mchango wa mwandishi kuingia katika mfuko huo kwa wakati, ili kuwajengea uwezo wa kulipia huduma
hiyo ambayo ni tija katika uwajibikaji wao.
No comments:
Post a Comment