KATIBU mkuu wa chama cha Alliance for change and Transparency(ACT) taifa Samson Mwigamba amewataka viongozi wa chama hicho
kuanzia ngazi ya kata na majimbo kuhakiki viongozi watakaogombea katika uchaguzi ujao 2014 wa
serikali za mitaa kwa kuwasimika viongozi wenye upeo wa mambo na wanaokubalika
katika jamii.
Akitoa
kauli hiyo kigoma Ujiji jana katika kikao cha viongozi na wanachama
wa chama hicho kutoka jimbo la Kigoma Kaskazini, Kusini na kigoma mjini
alisema watumie fursa ya hiyo kuwapa nafasi viongozi wenye sifa na
vigezo kwa lengo la kuboresha mfumo wa utawala.
Alisema ili chama kiweze kupata nyadhifa mbalimbali za
uongozi ni lazima kila kiongozi katika jimbo alilopo ahakikishe kunakuwa na
uongozi kamili katika vijiji ,ili kunyakua majimbo katika
nafasi za udiwani, ubunge na urais.
Hata hivyo aliwataka viongozi na wanachama kuacha siasa za
matusi katika majukwaa na badala yake watumie lugha za hekima,busara na
kizalendo kwa hoja zenye mashiko ya kuelimisha umma na
kufanya kazi kwa uwazi na uwajibikaji.
Mwigamba alisema lengo la chama hicho kurekebisha siasa ya
nchi kupitia vyama pinzani kwa kuondoa tofauti zilizopo pamoja na kuondoa
utashi wa mwasisi wa chama katika vyama vilivyopo, kuwa na demokrasia ya kweli
ambapo vyama vingine havizingatii hilo.
Naye katibu wa mawasiliano na habari Muhamedi Masaga alisema
kuanzishwa kwa chama sio kwa lengo la kudhohofisha vyama vingine ni kuwa na chama
chenye mshikamano, umoja na kulinda uzalendo wa n chi ili kushika dola ya nchi katika
chaguzi zijazo.
Alisema katika ziara walizozifanya katika mikoa mitatu, mkoa
wa kigoma umekuwa kinara wa wanachama
waanzilishi ambao wamefikia 570 ikifuatiwa na Katavi 400 pamoja na Tabora 150 ambapo
ni mwanzo unaoleta matumaini katika kukiendeleza chama.
No comments:
Post a Comment