Pages

KAPIPI TV

Monday, July 21, 2014

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA ASHIRIKI MKUTANO WA TATU(03) WA UMOJA TAASISI ZA MAGEREZA BARANI AFRIKA, MAPUTO MSUMBIJI

image_3
image_1
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa Tatu(03) wa Umoja wa Taasisi za Urekebishaji(Magereza) Barani Afrika wakifuatilia Majadiliano ya Mkutano huo uliofanyika hivi karibuni Maputo, Msumbiji(wa kwanza kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja(wa kwanza kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Uganda, Dkt. Johnson Byabashaija(mstari wa nyuma) ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza Nchini Tanzania wakifuatilia mjadala katika Mkutano huo wa Kimataifa.
image_2
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Nchini Tanzania, Profesa Sifuni Mchome akiwasilisha Mada ihusuyo Urudiaji wa Vifungo Magerezani kwa Wahalifu(Recividism) katika Mkutano wa Tatu wa Umoja wa Taasisi za Urekebishaji(Magereza) Barani Afrika uliofanyika hivi karibuni Maputo, Msumbiji.
photo
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, John Casmir Minja akichangia Mada katika Mkutano wa Tatu(03) wa Umoja wa Taasisi za Urekebishaji(Magereza) Barani Afrika uliofanyika hivi karibuni kuanzia July 14 – 17, 2014 Maputo, Msumbiji.
image
Maafisa na Askari Magereza wa Msumbiji wakimsikiliza Mgeni rasmi, Rais wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji, Mhe. Dkt. Armando Guebuza(hayupo pichani) katika ufunguzi wa Mkutano wa Tatu(03) wa Umoja wa Taasisi za Urekebishaji(Magereza) Barani Afrika uliofanyika Maputo, Msumbiji.

NAPE : CCM HAIKATAZI MWANACHAMA WAKE KUTANGAZA NIA YA KUGOMBEA UONGOZI

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye amesema Chama Cha Mapinduzi hakimzuii mwanachama yeyote kutangaza nia ya kugombea Uongozi katika muhula unaofuata isipokuwa Chama kimezuia kampeni za mapema kwani ndio chanzo cha makundi ndani ya Chama akizungumza kwenye kipindi cha Baragumu kinachorushwa na Channel 10 ,Nape  alisema taratibu za kugombea Uongozi ndani ya chama zipo na kuna Kanuni mbili, moja ni ya Kanuni za Viongozi na Maadili na pili Kanuni zinazosimamia Uchaguzi ndani ya CCM, akinukuu kutoka kwenye kitabu cha Kanuni za Viongozi na Maadili ,Nape alisema “Wanachama wenye nia ya kugombea nafasi ya uongozi katika muhula unaofuata anaweza kutangaza nia ya kugombea lakini haruhusiwi kufanya kampeni kabla ya muda”.
   Akizungumzia juu ya adhabu wanazopewa waliokiuka alisema adhabu hizi zina shabaha ya kuwasaidia wanachama na Viongozi kujirekebisha.
Nape pia alizungumzia suala zima la upatikanaji wa Katiba Mpya,alisema CCM imeshikamana sana kiasi cha kuwachanganya Wapinzani, aliendelea kwa kusema Kanuni,Sheria zinazotumika ni makubaliano ya wote.(Wapinzani walishiriki katika kamati kutengeneza kanuni na sheria na zikapitishwa Bungeni wakiwemo na Rais akasaini).
Chanzo: kamerayangublog.com

MAMIA YA WANANCHI SOMANGA KILWA WAJITOKEZA KUPIMA AFYA BURE,KAYA 70 ZAJIUNGA NA CHF PAPO KWA PAPO WAKIPOKEA MWENGE WA UHURU.

822
Na. Paul Marenga-NHIF LINDI
841
Wananchi wa Kilwa wakiwa kwenye foleni ya kupata huduma za vipimo kwenye banda la Mfuko wa taifa wa bima ya afya ambapo huduma za upimajiwa kiwango cha sukari kwenye damu (RBG),shinikizo la damu (BP),uwiano wa uzito na urefu wa mwili (BMI) na ushauri wa kitaalamu ulitolewa na madaktari,wakati wa mapokezi ya mwenge wa uhuru kwenye viwanja vya shule ya msingi Somanga-Kilwa.
868
Meneja wa mfuko wa taifa wa bima ya afya mkoa wa Lindi Fortunata Kullaya akitoa taarifa ya utekelezaji wa zoezi la upimaji afya na mwitikio wa wananchi wa kilwa ambapo takribani wananchi 257 walijitokeza kupimwa afya na  kaya 73 zilijiunga papo kwa papo na CHF Kwenye banda la mfuko kwa kiongozi wa mwenge kitaifa kwa mwaka 2014 Rachel Kassanda,ambaye alikagua shughuli mbalimbali zilizokuwa zikitekelezwa kwenye viwanja vya shule ya msingi somanga ambapo mwenge wa uhuru ulipokelewa,kulia  ni mkuu wa wilaya ya Kilwa mhe. Abdallah Ulega.
882
Mnafanya kazi kubwa kuisaidia serikali katika kutoa elimu kwa jamii kuchangia huduma za afya ili ziboreke sambamba na upimaji wa afya bure kwa magonjwa yasiyoambukiza  unaomuwezesha mwananchi wa kawaida kupata huduma pasipo gharama..hongereni sana alisema kiongozi wa mwenge kitaifa Rachel Kassanda,huku akisisitiza wananchi kutambua CHF ni mali yao hivyo kujiunga kwao kwa wingi ndiyo msingi wa maboresho ya huduma za afya hususani upatikanaji wa dawa,kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe.Abdallah Ulega,kushoto anayemsikiliza ni Meneja wa NHIF Mkoa wa Lindi Fortunata Kullaya.
892
Kiongozi wa mwenge kitaifa mwaka 2014 Rachel Kassanda akiwataka wananchi wa kilwa kujiunga na CHF,kwani ndiyo mkombozi wa matibabu sasa kwa kuzingatia maboresho ya huduma za afya yanavyowezekana chini ya sera ya urasimishaji wa majukumu kwa jamii hususani ya uchangiaji baina ya wananchi na serikali,ambapo mfuko wa taifa wa bima ya afya unasimamia mfuko wa afya ya jamii kwa niaba ya serikali ,kulia ni mkuu wa wilaya ya Kilwa mhe.Abdalla Ulega ambaye ndiye mwenyeji wa mapokezi ya mwenge wa uhuru.

WANANCHI WAITOLEA MACHO MANISPAA-KIGOMA

Na Magreth Magosso,Kigoma
 
Mradi wa ujenzi wa Gati katika mwalo wa kibirizi katani humo mkoani hapa,upo mashakani  kuanza kwake ,kutokana na  wahanga wa eneo hilo wapatao 53 kuipa siku 30 Manispaa ya kigoma ujiji ili kuboreshewa  stahiki zao  kwa mujibu wa Sera  na Sheria ya Ardhi husika.
Hayo yalisemwa juzi na mwanasheria wa kujitegemea Daniel Rumenyela katika ofisi za chama cha wandishi wa habari mkoani hapa,akiwakilisha adha za wananachi hao, juu ya ufinyu wa fidia usiozingatia sheria ya ardhi ya mwaka 1999 .
“uthamini  ulifanyika 2012 na malipo 2014,kifungu cha( 5),( 4 )ya sheria ya ardhi  na sera ya ardhi inataka fidia itolewe kwa wakati na haraka kwa wahanga na ikichelewa  tathimini  ifanywe   kila baada ya miezi sita, ili fidia ilingane na hitaji la leo” alibainisha Rumenyela.
Alisema  wamempa siku 30 Mkurugenzi wa manispaa ya kigoma Ujiji ,ili aweze kuboresha  haki stahiki za wahusika kwa sheria husika kwa lengo la kuboresha ustawi wa jamii na maendeleo kwa ujumla.
 

Meneja wa Mamlaka ya Bandari TPA wa hapa Patrick Namahuta alipohojiwa juu ya hili alisema mchakato wa kufidiwa kwa walengwa ulifanywa na mthamini wa manispaa hiyo kwa mujibu wa sheria husika na wao walitenga bajeti zaidi  ya milioni 600 ili kukidhi hitaji la walengwa.
 

Alisema TPA taifa ilitoa fidia kwa wahanga hao pasipo mkoa kuhusishwa kikamilifu katika kuhakiki picha na akaunti za walengwa, ili anayelipwa  akiri ni sahihi na kusisitiza malipo yalifanywa makao makuu na akaunti za wahanga zilipelekwa na manispaa husika.
 Namahuta  alisema lengo la mradi huo ni kuboresha huduma kwa wadau,ambapo  mwalo wa kibirizi  ni chachu kibiashara kwa nchi jirani za Burundi na jamuhuri ya watu wa kongo(DRC)  na    ili kukidhi haja za walengwa kwa ukanda wa  ziwa Tanganyika  zinahitajika gati 19 ambayo  itaongeza ufanisi kwa mamlaka hiyo.
Mkuu wa wilaya ya hapa Ramadhan Maneno amekiri mchakato ulifanywa na manispaa husika kupitia mthamini wao na walicholipa TPA ni matokeo ya uthamini na kusisitiza wananchi walishirikishwa kwa kila hatua na kuwasihi walengwa wasitake malipo yalingane.
 Alisema mfumo mbovu wa  malipo  ya fidia hauko vyema, kutokana na  TPA mkoa kutoshirikishwa katika kila hatua  na endapo ingeshirikishwa  ni rahisi kubaini haki na batili kwa lengo la kuondoa utata wa fidia hizo kwa wananachi,ambao  wanamtazamo  hasi kwa  manispaa  katika uwajibikaji .
Kaimu  Mkurugenzi  wa  manispaa  hiyo Moses Weransari alisema mthamini alizingatia uhalisia wa thamani za wahanga  na kwa mara ya mwisho kufanya tathimini ilikuwa 2013 na  wahanga kulipwa rasmi kupitia akaunti zao ni  Juni,2014 .

KOMWETA HEMED MANETI A.K.A CHIRIKU WA VIJANA JAZZ AFUATA NYAYO ZA MAREHEMU BABA YAKE HEMED MANETI ULAYA

1970462_1454799778083088_1638018053_n
Komweta Hemed Maneti a.k.a Chiriku mwanamuziki wa bendiya Vijana Jazz
1486871_1427285270834539_2027172492_n
Marehemu Hemedi Maneti Ulaya Chiriku aliyekuwa mwamuziki wa bendi ya Vjana Jazz enzi hizo.
......................................................................................................
Komweta Hemed Maneti a.k.a Chiriku ni Mtoto wa mwanamuziki wa zamani marehemu Hemedi Maneti Ulaya Chiriku aliyekuwa akiimba katika bendi ya umoja wa vijana Vijana Jazz enzi hizo ambapo anasema amekuwa kwenye muziki kwa muda mrefu japokuwa kama ilikuwa kama kujifurahisha, Komweta Hemed Maneti alianza muziki kama kazi mwezi Agosti mwaka 2013 akiimba katika bendi ya Vijana Jazz ambayo marehemu baba yake Mzee Hemedi Maneti Ulaya aliitumikia kwa mafanikio enzi za uhai wake.

Komweta Hemed Maneti a.k.a Chiriku amekuwa akijizolea umaarufu mkubwa katika bendi hiyo kwani mashabiki wengi wamekuwa wakimkumbuka marehemu baba yake mara anapoimba jukwaani kwani kwa kiasi kikubwa sauti zinaendana na marehemu baba yake Hemed Maneti, Bendi ya Vijana Jazz imekuwa ikipata umaarufu siku hadi siku katika maonyesho yake yanayofanyika kwenye klabu ya Kilwa Road Pub Ijumaa, Jumamosi wanapiga Jet Lumo na Jumapili kwenye ukumbi wa Vijana Hall Kinondoni.

Komweta mpaka sasa ana Nyimbo mbili na zipo mbioni kutoka akiwa ameimba kwa kushirikiana na bendi ya Vijana Jazz mtunzi akiwa ni yeye mwenyewe nyimbo yake Inaitwa (Walimwengu) na nyingine inaitwa (Nitajuaje) ukiwa ni utunzi wa Shomary Ally lakini yeye akiwa mwimbaji kiongozi katika wimbo huo pamoja naye Julius Mwesiwa.

Wanamuziki wakongwe waliobaki kwenye bendi ya vijana Jazz ambao waliwahi kuimba na marehemu Hemed Maneti ni Shomary Ally,Abdallah Mgonahazeru na Roshy Mselela, Ndoto za Komweta Hemed ni kuwa mwanamuziki wa kimataifa na kuipepeprusha vema bendera ya Tanzania ndani na nje ya mipaka ya TANZANIA ameolewa na ana mtoto mmoja wa miaka 5 anayeitwa Fahad.

 Anaongeza kuwa Changamoto za kazi ya muziki na malezi ni nyingi lakini muhimu ni kujua jinsi gani utapanga ratiba zako vizuri na kuhakikisha unafanya maandalizi mazuri kwa ajili ya mtoto na hili halinishindi natimiza majukumu yangu vizuri kama mama
Ni kweli kwamba mara nyingi nakuwa nafanya kazi siku za wikiendi hivyo nakosa muda wa kutosha wa kukaa na mtoto ukizingatia ndiyo siku na yeye anakuwa anapumzika haendi shule, lakini kama mama unatakiwa kujua majukumu ya familia yako ninafurahia maisha na familia yangu na mtoto wangu ni mweye furaha sana ninamshukuru mungu kwa hilo,
hata hivyo siku za jumatatu zinakuwa zina changamoto kubwa sana hasa katika kumwandalia mahitaji yake kwa ajili ya kwenda shule kwakuwa nakuwa nimechoka na kazi.

Mwanamuziki huyo anasema mashabiki wa bendi ya vijana wamempokea vizuri sana kusema kweli anaongeza kuwa "Nashukuru Mungu sana kwa hilo
na hili linajidhihirisha ninapokuwa nafanya shoo zangu...watu hawakai chini mara nyingi wanakuwa wakicheza..."
Anamaliza kwa kusema "Umaarufu wa marehemu baba yake mzee Hemed Maneti upo na siwezi kuuepuka...lakini kubwa watu wananipima kutokana na utendaji na ufanisi wangu wa kazi yangu niwapo jukwaani".

MAAFISA BARAZA LA HABARI TANZANIA WATEMBELEA CHUO CHA MUSOMA UTALII NA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI TABORA

Baadhi ya maafisa kutoka Baraza la Habari Tanzania MCT,Bi.Pili Mtambalike,Bi.Alakok Mayombo na Bw.John Nguya walitembelea Ofisi ya Chama cha Waandishi wa habari Tabora ambapo waliambatana na wenyeji wao Mkurugenzi wa Chuo Cha Musoma Utalii  Tabora Bw.Shaaban Mrutu na Mkufunzi wa chuo hicho Bw.Marwa Robert.

CHADEMA YAZIDI KUTEKETEZWA NA MOTO WA CHAMA KIPYA CHA ACT, TABORA NAKO CHAWAKA


TABORA, Tanzania
WIMBI la viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kukikimbia zimeendea, kufuatia Katibu wa Chama hicho  mkoani Tabora, Othman Balozi na kundi la wanachama wengine kibao kutangaza leo kujiunga na chama kipya cha  ACT Tanzania, ambacho kinaaminika kuasisiwa na aliyekuwa Natibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe ambaye kwa sasa amebakia ni mbunge tu kwa tiketi ya chama hicho.

Mbali na Balozi aliyewaongoza wajumbe 78 wa baraza kuu la Chadema hivi karibuni kwenda kwa msajili wa vyama kulalamikia katiba ya Chadema kukiukwa, pia wamo viongozi mbali mbali wa mabaraza ya kimkoa kiwilaya na majimbo walioamua kujitoa na kujiunga na Chama kipya cha ACT-Tanzania

Viongozi hao ni mwenyekiti wa Bavicha mkoa wa  Tabora Hussein Kundecha,mratibu wa uhamasishaji Bavicha  wilaya ya Tabora mjini Nzuki Machibya na Ramadhan Simba Mwenyekiti wa Chadema jimbo la Bukene.

Wengine ni Suni Yohane aliyewahi kuwa katibu wa Chadema wilaya ya Nzega pamoja na mwenyekiti wa baraza la wanawake katika wilaya hiyo.

Wimbi hilo pia limewazoa wanachama wa kawaida kutoka Chadema na CUF pamoja na watu ambao 200 ambao  hawakuwahi kuwa wanachama wa chama chochote hapo awali.

Kuhama kwa viongozi hao kumekuja ikiwa ni siku moja baada ya waliokuwa viongozi wa Chama hicho mkoa wa Kigoma kubwaga Manyanga

Waliobwaga Manyanga kwa Mkoa wa Kigoma hiyo juzi ni Jafari Kasisiko Mwenyekiti, katibu Msafiri Wamalwa na iti wa Baraza la wanawake wa  mkoa wa Kigoma kubwaga Manyanga

Akizungumzia sababu ya kujiondoa Chadema Balozi alisema kabla ya kufikia uamuzi huo alimpa taarifa mwenyekiti wake wa mkoa Kansa Mbaruku juu ya uamuzi huo

Alisema akiwa miongoni mwa viongozi wa awali kukipokea Chadema katika mkoa wa Tabora,amechoshwa na chama hicho kuacha misingi yake ya  kidemokrasia na kukumbatia Ubabe na dharau huku wakiwanyooshea vidole  vya usaliti wale wanaohoji baadhi ya mambo wasiyoridhika nayo ndani ya Chama hicho.

“Leo mimi ni mtu huru na nimewasikiliza ACT na falsafa yao ya uwazi na kuamua kujinga kwa hiari yangu sasa huu uwazi waudhihirishe na sitasita kuhoji pale penye matatizo nawasihi katika hali hiyo wawe wavumilivu kwa tutakayohoji”alisema Balozi.

RAIS KIKWETE AKAGUA KILIMO CHA KAHAWA MBINGA


D92A6133
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi miche bora ya kahawa mkulima mdogo Bi Dorothea Komba wakati alipolitembelea na kukagua shamba la kahawa AVIV Farm linalomilikiwa na kampuni ya Olam katika kijiji cha Lipokela wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma leo.Kampuni ya Olam imepanga kutoa jumla ya miche milioni tatu kwa wakulima wadogo elfu mbili katika vijiji vinne vinavyozunguka shamba hilo katika kipindi cha miaka mitano ili kuwashirikisha kuzalisha kahawa bora.
D92A6149
Meneja wa Shamba la Kahawa la AVIV Farm linalomilikiwa na kampuni ya Olam Bwana Medappa Ganapati akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mche bora wa kahawa iliyozaa vyema wakati Rais alipolitembelea na kukagua shamba la kahawa katika kijiji cha Lipokela, wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma leo
D92A6169
Meneja wa Shamba la Kahawa la AVIV Farm linalomilikiwa na kampuni ya Olam Bwana Medappa Ganapati akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mche bora wa kahawa iliyozaa vyema wakati Rais alipolitembelea na kukagua shamba la kahawa katika kijiji cha Lipokela, wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma leo
D92A6517 D92A6622 D92A6648
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua Soko la Kimataifa la Mkenda lililopo katika kijji cha Mkenda Mpakani mwa Msumbiji na Tanzania leo.kulia ni mbunge wa Peramiho Mh.Jenister Mhagama.Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi Mkoani Ruvuma(picha na Freddy Maro)

Sunday, July 20, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKABIDHI ZAWADI ZA WASHINDI WA MASHINDANO YA QUR-AN JIJINI DAR

01
1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mshindi wa pili wa mashindano ya kuhifadhi Qur-an, ambaye ni Mtanzania, Said Omary Said, wakati wa hafla ya hitimisho la mashindano hayo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, leo Julai 20, 2014. Wa pili kushoto ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi. Picha na OMR
2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mshindi wa kwanza wa mashindano ya kuhifadhi Qur-an, Hatham Sadar, kutoka nchini Kenya wakati wa hafla ya hitimisho la mashindano hayo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, leo Julai 20, 2014. Wa pili kushoto ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi. Picha na OMR
3
-Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na baadhi ya viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na washindi watatu wa mashindano hayo baada ya kukabidhiwa zawadi zao. Picha na OMR
4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na baadhi ya viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mashindano hayo baada ya kukabidhiwa zawadi zao. Picha na OMR
5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na baadhi ya viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na washindi watatu na majaji wa mashindano hayo baada ya zoezi la kukabidhi zawadi. Picha na OMR
6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam, wakati akiondoka kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee baada ya kukabidhi zawadi za washindi wa mashindano ya kuhifadhi Qur-an, yaliyomalizika leo Julai 20, 2014, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
7
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam, wakati akiondoka kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee baada ya kukabidhi zawadi za washindi wa mashindano ya kuhifadhi Qur-an, yaliyomalizika leo Julai 20, 2014, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
8
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam, wakati akiondoka kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee baada ya kukabidhi zawadi za washindi wa mashindano ya kuhifadhi Qur-an, yaliyomalizika leo Julai 20, 2014, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

ACT YAZOA VIONGOZI WA CHADEMA TABORA


Na Mwandishi wetu maalumu.
 
CHAMA kipya cha siasa hapa nchini Alliance for Change and Transparency
(ACT) kimedhamiria kukiondoa madarakani chama tawala (CCM) kwa kuwa
viongozi wake hawana uchungu na dhamira ya kweli ya kumaliza kero za
wananchi zilizokithiri katika
nyanja mbalimbali hapa nchini jambo ambalo limechangia wananchi wengi
kuwa na maisha duni.

Hayo yalibainishwa na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho Kadawi Lucas
Limbu katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika uwanja wa
stendi ya zamani mjini Tabora ambapo alieleza kuwa CCM imeshika dola
kwa mda mrefu sana lakini viongozi wake hawajali wananchi na hawana
uzalendo kwa Taifa.

Limbu alisema inasikitisha sana kuona Watanzania walio wengi
wakiendelea kuishi katika hali ya sintofahamu wakati nchi yao
imejaliwa kuwa na utajiri mwingi sana, badala yake utajiri huo ambao
ni rasilimali za Taifa ukiendelea kuibiwa na watu wachache badala ya
kuwanufaisha wazawa wote.

Alisema tokea nchi hii inapata uhuru baba wa Taifa hayati Mwalimu
Nyerere alisimama imara kupinga aina zote za unyonyaji, alikemea
vikali mtu au kiongozi yeyote yule kujinufaisha kupitia mgongo wa
wanyonga sambamba na kufukuza viongozi wazembe na wasio waadilifu
wasiotetea maslahi ya mwananchi.

Alibainisha kuwa CCM haina viongozi wenye uchungu wa kutetea wanyonge
na kusimamia rasilimali za nchi yao kama alivyokuwa Mwl Nyerere ndio
maana watu wachache wanazidi kunemeeka wakati kero za wananchi
zikizidi kuongezeka kila kona ya nchi, kero za ardhi, madini, elimu
n.k hazikustahili kuwepo mpaka sasa, enzi za Nyerere elimu ilikuwa
bure, yeye aliwezaje, CCM wameshindwaje?

Akizungumzia msimamo wa ACT katika mchakato wa katiba mpya unaoendelea
sasa Limbu alisema wanataka serikali 3 zilizoboreshwa zitakazokuwa na
Rais mmoja tu wa Jamhuri ya Muungano, kama Rais atatoka upande fulani
wa Muungano upande uliobaki utoe Makamu wa Rais na kila upande uwe na
mtendaji mkuu wa serikali na bunge lake.

Katibu Mkuu wa Chama hicho Samson Mwigamba alisema ACT ndicho chama
pekee chenye uwezo wa kuing’oa CCM madarakani kwa kuwa kimedhamiria
kusimamia fursa zote zilizoko hapa nchini zimnufaishe mwananchi na
nguvu yake kubwa ni kujali uzalendo, usawa, uwazi, demokrasia n.k
wakati vyama vingine vimejaa ubinafsi tu na vimeshindwa kulisimamia
hilo.

Kaimu Katibu wa Mawasiliano na Uenezi  wa chama hicho Mohamed Masaga
alisema ACT haina mpango wa kuua chama chochote cha Siasa bali ACT
imekuja kuleta demokrasia ya kweli na kusimamia rasilimali za Taifa
ili zisomeshe watoto wetu, ziondoe umaskini na kuleta uzalendo.

Katika mkutano huo wanachama zaidi ya 90 kutoka vyama mbalimbali vya
siasa walijiunga na chama hicho wakiwemo Katibu wa CHADEMA mkoa wa
Tabora Bw.Athman Alfan balozi, aliyekuwa Mwenyekiti wa BAVICHA mkoani
Tabora Hussein Juma Wakundecha, aliyekuwa mjumbe wa NEC CHADEMA Maulid
Bwiru ambaye sasa ndiye Kaimu Mwenyekiti wa ACT mkoa wa Tabora.

Wengine ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Kata ya Chemchem katika manispaa ya
Tabora kupitia CHADEMA Idd Omar  na aliyekuwa mgombea udiwani kupitia
CHADEMA katika uchaguzi uliopita katika kata ya Kitongoni mjini Kigoma
Kacheche Maulid Kacheche.

"RAGE AANDAMWA NA WAPAMBE WAKE,WAANZA KUMZUNGUUKA,WAMCHAFUA,WAJIANDAA KUVUTA FOMU YA UBUNGE WAKATI WA KURA ZA MAONI CCM"

Mbunge wa jimbo la Tabora mjini Mh.Ismail Aden Rage.
Mwandishi wetu maalumu-Tabora 
Katika hali ambayo si ya kawaida ingawa kisiasa ni jambo la kawaida kabisa na huenda likawa ni jambo ambalo  hataweza kulisahau maishani mwake Mbunge wa Jimbo la Tabora mjini Mheshimiwa Aden Rage kutokana na mbinu chafu zinazodaiwa kuanza kufanyiwa mbunge huyo na kuhakikisha anapoteza nafasi yake wakati wa kura za maoni kupitia Chama cha Mapinduzi.

Mtandao huu wakati unaendelea kufuatilia makundi ndani ya CCM kwa mkoa wa Tabora  katika maandalizi ya kuwania nafasi mbalimbali ikiwemo ya Udiwani na Ubunge,imebainika kuwa kundi linalodai kumuunga mkono Mbunge wa jimbo la Tabora mjini Aden Rage limekuwa ni miongoni mwa wasaliti wa kwanza wa kupanga mipango na mbinu chafu za kumuhujumu kwa wajumbe ambao watakaoingia kupiga kura za maoni wakati utakapowadia.

Moja kati ya mbinu chafu ambazo hata Mheshimiwa Rage hazitambui zinazodaiwa kufanywa na wapambe wake ni pamoja na kuwataka wajumbe ambao kati yao ni makatibu wa matawi,kata,wanajumuiya mbalimbali zikiwemo za wazazi,UWT na kiasi kwa UVCCM na  kuonesha hali ya kumuunga mkono mbunge huyo wakati anapokutana nao kwenye vikao vya siri na vya hadharani jambo ambalo ni kinyume.

Hata hivyo mwanya huo pia unadaiwa kutumiwa na Wapambe hao kumuhadaa Mheshimiwa Rage ajione kuwa yuko pamoja nao kumbe miongoni mwao wamejipanga kuvuta fomu wakati wa kura za maoni jambo ambalo Rage hajalijua na hasa kwa wengine ambao wamepandikizwa katika kambi yake huku ikionesha namna anavyowaamini na kujihakikishia kuwa ndio watu watakaompa msaada mkubwa  wa kupiga debe wakati wa uchaguzi katika kura za maoni.

Aidha kwa upande mwingine wapo wapambe ambao ni viongozi ndani ya CCM wameonesha hali ya kumsaidia katika masuala mbalimbali lakini pindi Mheshimiwa Rage anapokuwa hayupo katika jimbo lake hutumia nafasi hiyo wao kujinadi na hata kutoa fedha kwa wanaccm  huku wakiendelea kumchafua kisiasa.

Katika hali hiyo pia baadhi yao wamefanikiwa katika mpango mahususi wa kumjengea mazingira Mheshimiwa Rage akosane na baadhi ya viongozi wa CCM ngazi za wilaya na mkoa jambo ambalo ni hatari kisiasa ingawa mpango mwingine ulikuwa umeandaliwa na wapambe wake kuhakikisha wanamuingiza kwenye mgogoro mkubwa wa Waislamu katika msikiti mkuu wa Ijumaa Gongoni mpango ulikwama baada ya mbunge huyo kutahadharishwa  mapema  na kadhia hiyo.

Wapambe hao wanaodaiwa kumuandama kimyakimya  Mheshimiwa Rage ambao wamegawanyika katika makundi mawili hadi matatu,Wachache ni wale ambao wamejipanga kuvuta fomu kuwania nafasi ya Ubunge kwa kutambua madhaifu aliyonayo,Wapili ni wale ambao wametumwa kuwa karibu naye na kujifanya wanamuunga mkono na kujaribu kumpandikizia chuki dhidi ya watu wengine ili Rage aendelee kuwathamini pamoja na kuvujisha siri za vikao vya ndani,wengine ni wale ambao wapo kwa ajili ya kutaka kujipatia fedha ingawa kundi hili Rage amekuwa makini sana na kuchukua tahadhari.

Kwawale ambao ni wapambe waliotumwa kuwa karibu na Mheshimiwa Rage kwa lengo la kuchimbua habari mbalimbali na kuandaa mazingira ya siasa chafu dhidi yake,mtandao huu umebaini kuwa malipo yao yanatokana na taarifa  wanazochukua kwa mbunge na kuzipeleka kwa waliowatuma ili kuweza kufanikisha mikakati yao.

Pamoja na utekelezaji  mzuri wa ilani ya chama chake kwa wananchi  unaofanywa na mbunge huyo ikiwemo uchimbaji wa visima vya maji safi na kusaidia wakulima  bado Wapambe hao wa karibu wa Mheshimiwa Rage wamekuwa wakimhujumu kuwa hajafanya lolote.   

MAONI YA MTANDAO:
Mheshimiwa Rage jaribu ulipitie upya na uwe makini sana na kila anayejidai anakuunga mkono kwakuwa hadi sasa kwa wapambe wote ulionao ni mmoja tu ndiye yupo pamoja nawe na Mungu anajua hilo.Kumbuka yaliyowatokea waheshimiwa kama Prof.Mgombelo,Mwanne Mchemba na Aziza Suleyum ambao walijenga mazingira ya kuwaamini watu wao wa karibu na hatimaye Kijani ikageuka kuwa Nyekundu.

Kuna watu upo nao wenzako wapo kazini,ni lazima wafikishe taarifa ili wapate malipo yao,zipo fedha zinatoka ndani ya mkoa na nyingine inatoka nje ya mkoa,tumia mbinu ulizotumia wakati ukiongoza klabu ya Simba najua lazima utawabaini.

Ukifika wakati wa uchaguzi pia zidisha umakini kwani wapo ambao wanataraji kuona umefilisika kabisa hata uombe au kukopa  nauli ya kukupeleka Dar-es-salaam.   

TAPELI LILILOJIDAI KISHOKA WA TANESCO LADAKWA LIVE MLIMANI CITY

10500539_819006161445574_7780628803053090260_n

Pichani juu na chini ni Kishoka wa Tanesco aliyekamatwa Mlimani City.

Na Mwandishi wetu
TAPELI lililokubuhu kwa masuala ya kulaghai watu kwa njia ya kujifanya kishoka washirika la Umeme Nchini, Tanesco, jana asubuhi limedakwa baada ya kuwekewa mtego walipokuwa wakitaka kutapeli kwa mmoja wa Afisa wa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma- Ledama.

Kwa mujibu wa Bi. Usia akieleza tukio hilo, alidai kuwa tapeli huyo alifika asubuhi akiwa na wenzake sita, nyumbani kwake wakasema wanatoka Tanesco wamekuja kucheki mita ya Luku. 

Hata hivyo wakakorokocha wakasema mita imechezewa kwa hiyo wanakata Umeme na kung’oa mita, eti waliona kwenye GPS yao kuwaUmeme hauendi vema.

“wakasema fidia na kurudisha umeme kiofisi ni milioni 8! ila tukiwapa milioni 2 wataturudishia. nikawauliza kama mita imechezewa mbona tunanunua umemewa laki 3 kwamwezi? si ingepaswa tulipe kidogo? wakasema wakati mwingine wakiweka hiyo resistance (eti ndo kifaa cha kuiba Umeme) huwa kinafyatuka halafu Umeme unakwenda zaidi! “ alielezea Bi. Usia.

Na kuongeza kuwa vishoka hao wakakata Umeme wakaondoka, tujipange. tujadiliana na mzee tukapata mashaka maana walikuwa wakali halafu wanalazimisha mambo, wamevaa vitambulisho lakini wamevigeuza kwahiyo havisomeki. tukapiga simu Tanesco kuwauliza wakasema hao ni vishoka tuitePolisi, basi tukawapigia simu waje wachukue laki tano waturudishie Umeme, mengine Jumatatu. wakaja fasta wakarudisha Umeme, nikawaambia naenda aTM wasubiri nikawaacha na mzee nikatoka mbio mpaka Polisi chuo nikawahadithia wakanipa Polisi 3 nikaja nao nyumbani, tukawakuta wameondoka.

Mzee akawapigia simu waje hela imepatikana wakasema tukutane Mlimani City, tukafanikiwa kukamata mmoja wengine wakakimbia. tumemuacha selo, tukaandikisha maelezo. tunasubiri hatua itakayofuata.
10417599_819006198112237_2101442257557265538_nHapa likiwa chini ya ulinzi na pingu mkononi.

CHIKAWE AMWAGA MISAADA YA MABATI 100 NA JEZI ZA MIPIRA NACHINGWEA

PIX  1
PIX 2
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (Kulia), akimkabidhi jezi za timu sita za mpira wa miguu Afisa Mtendaji wa Kata ya Nditi, Patrick Mwasambungu kwa ajili ya kuzikabidhi timu hizo zilizopo katika Kata hiyo katika Jimbo la Nachingwea mkoani Lindi. Waziri Chikawe pia alitoa mabati 100 kwa ajili ya ujenzi ya Ofisi Kuu ya CCM katika Kata hiyo ya Nditi. Mbunge huyo wa Nachingwea yupo jimboni mwake kwa ajili ya kufanya ziara ya kuzungumza na viongozi wa CCM katika ngazi mbalimbali. Picha na Felix Mwagara.
PIX 3
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (Kushoto), akikiangalia kifusi cha mchanga kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Mnerongongo ambayo ipo katika hatua ya mwisho kukamilika ujenzi wake. Katika ujenzi wa ofisi hiyo, Waziri Chikawe alitoa mabati 100 ambayo tayari yameezekwa. Mbunge huyo wa Nachingwea yupo jimboni mwake kwa ajili ya kufanya ziara ya kuzungumza na viongozi wa CCM katika ngazi mbalimbali. Picha na Felix Mwagara.
PIX 4
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (Kushoto), akikagua ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Mnerongongo ambayo ipo katika hatua ya mwisho kukamilika ujenzi wake. Katika ujenzi wa ofisi hiyo, Waziri Chikawe alitoa mabati 100 ambayo tayari yameezekwa. Mbunge huyo wa Nachingwea yupo jimboni akifanya ziara ya kuzungumza na viongozi wa CCM katika Kata za Wilaya za Nachingwea mkoani Lindi. Picha zote na Felix Mwagara.

HOFU YATANDA KWA WASHIRIKI WA SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS, HUKU WENGINE WAKITAMANI WIKI IJAYO ISIFIKE.

Baadhi ya washiriki wa Fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) wakiwa mbele ya Majaji tayari kwa kupewa maoni yao na hatimaye kutaja watakaotoka chomwa na jua la utosi kwa Wiki hii. Kutoka Kulia ni Tishi Abdallah, Katikati ni Mtawa Kapalata na Kushoto ni Joshua Wambura.
Anneth Peter (katikati) akiwa mwenye huzuni kubwa kutokana na Mshiriki mwenza kutoka kanda ya Kaskazini Kareb John (hayupo pichani) kutoka kwenye shindano mara baada ya kuchomwa na jua la utosi.
 Washiriki wawili waliondolewa katika Shindano kwa wiki hii wakiwa mbele ya Jukwaa mara baada ya kutangaziwa kushindwa kuendelea kutokana na kuwa na idadi chache ya kura kutoka kwa watazamaji.Wa kwanza kushoto ni Kareb John na Malima Deogratius ambao wameaga mashindano
  Kareb John na Malima Deogratius mara baada ya kutangaziwa kuyaaga mashindano..
 Mara baada ya Kareb John Kuaga mashindano Mshiriki kutoka kanda ya Kaskazini Annet Peter alionekana mwenye huzuni kubwa
 Washiriki wakiwa na huzuni kutokana na wenzao kuaga mashindano.Picha zote na Josephat Lukaza wa Proin Promotions, Dar Es Salaam

Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited - Dar Es Salaam.
Ni wiki ya Pili sasa ya mchujo katika Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) ambapo washiriki wengine wawili wamechomwa na Jua la Utosi na hatimaye kuaga shindano. 

Mchujo huo ni muendelezo wa Mchujo ambao kila wiki washiriki wawili watachomwa na jua la utosi na hatimaye kupelekea kuaga shindano la TMT.

Mpaka sasa Washiriki wanne tayari wameshayaaga mashindano na kupelekea washiriki 16 kubakia katika mchujo unaofuata.

Mpaka sasa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) limekua ni shindano lililoteka hisia za watanzania wengi waliopo ndani na nje ya Nchi kutokana na ubora, Uhalisia na Ubunifu wa hali juu kutoka kwa Waandaaji na waendeshaji pamoja na washiriki kuonyesha Vipaji vyao.

Ili kuweza kumnusuru mshiriki wako asichomwe na Jua la Utosi unachotakiwa ni kumpigia kura kadri uwezavyo ili kumfanya abaki ndani ya Nyumba ya TMT.

Mara baada ya washiriki wa wiki hii kuondolewa katika shindano hali imezidi kuwa ni simanzi kwa washiriki kutokana na kutokujua ni zamu ya nani kutoka wiki ijayo.

Washiriki waliotoka wiki hii ni Kareb John ambae alikua mmoja kati ya Washindi watatu kutoka kanda ya Kaskazini Mkoani Arusha huku Mshiriki Malima Deogratius akiwa ni Mshindi kutoka KAnda ya Pwani Mkoani Dar Es Salaam.

Ili kuweza kumnusuru mshiriki umpendae unachotakiwa kufanya ni Kuandika neno "TMT" ikifuatiwa na namba ya Mshiriki halafu unatuma kwenda namba 15678. Mfano TMT00 tuma kwenda 15678. Piga kura kadri uwezavyo ili kumnusuru mshiriki wako kutochomwa na Jua na Utosi wiki ijayo.

Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) ni shindano lililobuniwa na Kampuni ya Proin Promotions Limited ambayo inahusika na utengenezaji, Usambazaji na Uuzaji wa filamu za Kitanzania huku ikiwa na malengo pia ya Kuibua vipaji vya Kuigiza na Mpira wa Miguu kwa Wanawake. 

Shindano hili Pia linaendeshwa na Kusimamiwa pia na Kampuni bora ya Usambazaji wa Filamu nchini ya Proin Promotions Limited
Huzuni na Simanzi zaendelea kutawala ndani ya Nyumba ya TMT kwa washiriki hao wawili kuondoka lakini Pia Hofu Yaendelea Kutanda ndani ya Nyumba ya TMT kwa washiriki kwa kutokujua ni zamu ya nani sasa kuchomwa na jua la utosi litakalompelekea kuaga shindano kwa wiki ijayo.

MABONDIA WAKUTANA NA KUUNDA UMOJA WA KUSAIDIANA KATIKA MAMBO MBALIMBALI

Bondia Said Chiddy kushoto akizungumza wakati wa mkutano wa umoja wa mabondia kwa ajili ya kusaidiana katika mambo mbalimbali uliofanyika katika ukumbi wa Vijana Kinondoni jana picha na www.superdboxing coach.blogspot.com
Mmoja wa wadau wa mchezo wa masumbwi nchini Khalifa Kiumbe Moto  kushoto akichangia mada wakati wa mkutano wa kuunda umoja wa mabondia uliofanyika katika ukumbi wa Vijana Kinondoni Dar es salaam picha na

Bondia Japhert Kaseba akizungumza kabla ya kufunga mkutano huo aliouitisha kwa ajili ya kuunda umoja wa mabondia kusaidiana kwa mambo mbalimbali picha na

www.superdboxing coach.blogspot.com

Saturday, July 19, 2014

"TIMU YA CHIPUKIZI NI CHIMBUKO LA WANASOKA TABORA"

Timu ya watoto wenye kipaji cha soka inayofahamika kama Chipukizi ya mjini Tabora,watoto hawa huanza kujifunza mpira wa miguu kuanzia miaka minane chini ya mwalimu wao mchezaji wa zamani wa timu ya Milambo Didas Kunde.