Zawadi ya mpira kwa mshindi wa pili |
Saturday, September 13, 2014
KITUMBO ASHANGAZWA NA VIPAJI VYA SOKA KWA VIJANA VIJIJINI - TABORA
ANUWAR KASHAGA AZIDI KUIBOMOA CHADEMA IGUNGA!!!
WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AWASILI TANGA KWA ZIARA YA SIKU MOJA YA KIKAZI.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wasanii wa kikundi cha wanawake wa
cha Tanga cha Msanja baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Tanga
kwa ziara ya siku moja ya kikazi Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo Chiku Gwao.Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wasanii wa kikundi cha wanawake wa
cha Tanga cha Msanja baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Tanga
kwa ziara ya siku moja ya kikazi.
NHIF YATETA NA WACHEZAJI, WATENDAJI KLABU YA YANGA
Katibu
Mkuu wa Yanga Bw. Beno Njovu akizindua semina ya Mfuko wa Bima ya Afya
na Watendaji na wachezaji wa Klabu ya Yanga iliyofanyika jana makao
makuu ya klabu hiyo mtaa Jangwani katikati ni Mkurugenzi
wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti na kushoto ni Christopher Mapunda
Meneja wa NHIF Wilaya ya Ilala klabu ya Yanga imekuwa ya kwanza kuanza
utaratibu wa kuijunga na mfuko wa Bima ya afya. Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti akizu.ngumza na watendaji wa Yanga na wachezaji wakati wa semina hiyo jana Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti akizu.ngumza na watendaji wa Yanga na wachezaji wakati wa semina hiyo jana Mmoja
wa maofisa wa Mfuko wa Bima ya Afya akiwaonyesha makocha wa Yanga
baadhi ya picha alizpoiga nao Kulia ni kocha wa yanga Marcio Maximo. Christopher Mapunda Meneja wa NHIF Wilaya ya Ilala akitoa mada wakati wa semina na wachezaji wa timu ya Yanga jana. Baadhi ya wachezaji na maofisa pamoja na wanachama wa Yanga wakiwa katika semina hiyo. Baadhi ya wanachama wa Yanga wakiwa katika semina hiyo kushoto ni mwanachama wa Yanga Bw Said Hassan Kipara Katibu Mkuu wa Yanga Bw. Beno Njovu akizungumza katikasemina hiyo kulia niHance John Mwankenja Afisa Matekelezo wa NHIF Mmoja wa maofisa akigawa majarida yanayoelezea faida za Mfuko wa Bima ya Afya ya jamii katika semina hiyo Ofisa Mawasiliano mwandamizi NHIF Bw. Luhende Andrew Singu akizungumza na wachezaji hao jana wakati wa semina hiyo
Friday, September 12, 2014
MBOWE ACHACHAMAA!!
Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, ameonya kuwa iwapo
kiongozi yeyote wa chama hicho ataruhusu mgombea wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) wa ngazi yoyote ya uongozi katika uchaguzi, kupita bila kupingwa
katika eneo lake, atawajibika.
Alitoa onyo hilo alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa Bavicha, jijini Dar es Salaam jana.
“Misiruhusu uongozi, kuanzia
serikali ya mtaa kupita bila kupingwa. Ikitokea hivyo, na wewe kiongozi
(wa Chadema) jiandae kuwajibika,” alisema Mbowe.
Aliutaka uongozi mpya wa Bavicha utakaochaguliwa kuendeleza kazi nzuri iliyoachwa na uongozi wa baraza hilo uliopita.
Kazi hizo ni pamoja na namna ya
kuwaandaa vijana, wazee na wanawake, kujiandikisha kwenye daftari la
kudumu la wapigakura na kushiriki chaguzi zote, kuanzia ule wa serikali
za mitaa, vijiji na vitongoji, udiwani, ubunge na urais mwakani.
Mbowe, ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) alisema muda mwafaka ukifika,
watakutana na viongozi wenzake wa vyama vinavyounda umoja huo vya CUF na
NCCR-Mageuzi kuangalia namna watakavyofanya kazi pamoja katika chaguzi
zijazo.
Alisema kifungu cha 6 (3) na (4)
cha katiba ya Chadema kinaelezea ukomo wa uongozi, hivyo akasema wana
kazi kubwa ya kupanua wigo wa chama.
Kwa kuzingatia hilo, alisema watakuwa na kazi ya kutathmini
utendaji wa kila kiongozi katika chama kila baada ya miezi sita kuona
namna alivyochangia kukuza na kukiimarisha chama.
“Kiongozi atakayeruhusu katika eneo lake chama kisikue, atawajibika kabla ya miaka mitano,” alisema Mbowe.
Alisema Chadema siyo ya fujo, bali
ni chama chenye dhamira ya kweli, hivyo akaonya kuwa iwapo mwanachama
wake yeyote anayegombea uongozi kwa kutumia mbinu chafu, ikiwamo rushwa,
atang’olewa hata kama atakuwa amekwishakupitishwa katika uchaguzi.
Awali, akimkaribisha Mbowe
kufungua mkutano huo, Mwenyekiti wa Bavicha anayemaliza muda wake, John
Heche, alisema Chadema imekua na kwamba, kigezo cha hilo ni namna
ilivyofanikiwa kufanya kwa mara ya kwanza uchaguzi, kuanzia ngazi za
msingi.
Aliushukuru uongozi wa Chadema kwa
kuwashughulikia wasaliti ndani ya chama na kusema kamwe vijana
hawatavumilia kuona mtu yeyote anakivuruga chama hicho.
Mapema, Katibu Mkuu wa Bavicha
anayemaliza muda wake, Deogratius Munishi, alisema wajumbe waliotakiwa
kuhudhuria ni 336 na kwamba, hadi kufikia saa 5.40 asubuhi,
waliosajiliwa walikuwa 301 sawa na asilimia 89 ya akidi ya wajumbe wote
wa mkutano huo.
SEKTA ZA MADINI ,UMEME NA KILIMO ZAKUZA PATO LA TAIFA.
Mkurugenzi
wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Morrice Oyuke
(katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ukuaji wa Pato la
Taifa kwa bei ya Soko leo jijini Dar es salaam. Wengine ni Bw. Oswald
Ruboha (kulia) Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Sera na Mipango, Wizara
ya Kilimo na Dkt. Stephen Kirama (kushoto), Mhadhiri wa Uchumi, Chuo
Kikuu cha Dar es salaam.
Na. Aron Msigwa – MAELEZO, Dar es salaam.
Sekta ya Kilimo,Uvuvi, Viwanda ,
Nishati na Madini zimeelezwa kuwa miongoni mwa sekta muhimu
zinazoongoza zaidi katika kuchangia kukua kwa pato la Taifa hadi
asilimia 7.4 katika robo ya kwanza ya mwaka 2014.
Kwa mujibu wa taarifa
zilizokusanywa kutoka katika vyanzo mbalimbali vya uzalishaji nchini na
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kutumia kanuni za kimataifa
kukokotoa pato la Taifa zinaonyesha kuwa sekta hizo zimetoa mchango
mkubwa wa kukua kwa pato la Taifa kwa asilimia 7.4 kuanzia mwezi
Januari hadi Machi, 2014 ikilinganishwa na asilimia 7.1 za mwaka 2013.
Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi
wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Morrice Oyuke akizungumzia ukuaji wa
Pato la Taifa kwa bei ya Soko leo jijini Dar es salaam amesema kuwa Pato
la Taifa katika robo ya mwaka 2014 kuanzia Januari hadi Machi limekua
kwa asilimia 7.4 kutokana na kukua kwa sekta za Kilimo, Uvuvi, Viwanda,
Ujenzi, Umeme na utoaji wa huduma.
Amesema sekta zilizofanya vizuri
katika ukuaji huo ni pamoja na sekta ya uchimbaji wa Madini, mawe na
kokoto ambayo imekua kwa asilimia 8.7 ikilinganishwa na asilimia 1.7 za
mwaka uliopita kutokana na kukua kwa masoko ya uuzaji ya nje ya nchi.
Ameongeza kuwa sekta uzalishaji
wa bidhaa za viwandani imekua kwa asilimia 8.5 kutoka 8.3 huku shughuli
za utoaji wa huduma na uchumi zikiwemo za ukarabati wa magari, pikipiki
na vifaa vingine vya majumbani zikikua kwa asilimia 8.0 kwa robo ya
mwaka 2014.
Bw. Oyuke ameeleza kuwa shughuli
za uchukuzi na mawasiliano zimefikia kasi ya ukuaji wa asilimia 16.5
katika kipindi hicho na kuongeza kuwa huduma za hoteli na migahawa
zimefikia kasi ya ukuaji wa asilimia 3.0, huku shughuli za uendeshaji wa
Serikali zikifikia asilimia 5.1, Elimu asilimia 5.2, huduma za Sfya
na shughuli nyingine zikikua kwa asilimia 4.5.
Aidha, amefafanua kuwa sekta ya
umeme katika robo ya mwaka 2014 imekua kwa asilimia 12.6 ikilinganishwa
na asilimia 6 ya mwaka uliopita kutokana na kupatikana kwa vyanzo
mbadala vya kuzalisha umeme hususan ugunduzi wa gesi nchini ambao
umeondoa tatizo la utegemezi wa umeme wa maji katika kuzalisha umeme.
“Kwa kipindi kirefu sekta ya
umeme imekuwa na mawimbi kwa kiasi kikubwa , umeme wetu umekuwa wa
kutegemea maji ya mvua, baada ya juhudi za Serikali na kugundulika kwa
nishati ya Gesi nchini na kupatikana chanzo mbadala cha nishati tatizo
hili limeshghulikiwa sasa sekta hii imeimarika” Amesisitiza.
Amesema Tanzania sasa inafanya
vizuri kiuchumi katika nchi za Afrika ya Mashariki kwa kuwa ya pili
ikifuatiwa na Uganda, Rwanda na Burundi na kuongeza kuwa hali ya amani
na utulivu iliyopo nchini inaiweka Tanzania katika nafasi nzuri ya kukua
zaidi kiuchumi.
Kwa upande wake mtaalam wa wa
Uchumi kutoka Benki Kuu ya Taifa (BOT) Bw. Davidi Kwimbere akifafanua
kuhusu hali iliyopo ya ukuaji wa uchumi amesema kuwa imechangiwa na
kuongezeka kwa shughuli za uzalishaji .
Amesema sekta ya
Kilimo na uzalishaji wa mazao imekua kutokana na matumizi ya mbolea,
zana bora za kilimo, mbegu bora, madawa na kufafanua kuwa endapo juhudi
zaidi zitaendelea kufanywa na wananchi kwa kuingia katika shughuli
mbalimbali za uzalishaji uchumi utaendendelea kuonekana kwa mtu mmoja
mmoja.
Amefafanua kuwa
maendeleo katika nchi yoyote yanachukua muda na kutoa wito kwa nchi za
Afrika kuendelea kujifunza na kufafanua kuwa nchi zote zilizopiga hatua
kimaendeleo mpaka kufikia asilimia 15 ikiwemo China iliwachukua miaka
20 kuondoa umasikini.
Amesema Tanzania
inayo nafasi nzuri kukua kiuchumi kutokana na kuendelea kuimarika kwa
miundombinu na ukuaji wa sekta za ujenzi, Nishati, madini, Viwanda,
umeme , kilimo na uvuvi hali inayochangia kuongezeka kwa uwekezaji.
WANANCHI WA KATA ZA NYANGAMARA, NANGARU HALMASHAURI YA LINDI VIJIJINI WAPIMWA AFYA ,ZAIDI YA 170 WAJIUNGA PAPO KWA PAPO NA CHF.
MENEJA WA NHIF MKOA WA LINDI FORTUNATA RAYMOND MWENYE MIWANI KULIA
,AKIENDELEA KUTOA UFAFANUZI KWA WANANCHI KUHUSU FAIDA ZA KUCHANGIA
HUDUMA ZA MATIBABU KABLA CHINI YA MFUKO WA AFYA YA JAMII,KUSHOTO NI
SALUM KAZIKAZI MWANANCHI WA KATA YA NYANGAMARA LINDI VIJIJINI. MZEE
ALLI G. CHIKOLO AKIPATA HUDUMA YA UPIMAJI WA KIWANGO CHA SUKARI (RBG)
KUTOKA KWA MTAALAMU WA MAABARA DKT S.MWAMPALE,AMBAPO UPIMAJI WA AFYA KWA
MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA ULIKUWA UKITOLEWA BURE NA MFUKO WA TAIFA WA
BIMA YA AFYA SANJARI NA ELIMU YA KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA WA
JAMII,KATIKA KATA YA NYANGAMARA HALMASHAURI YA LINDI VIJIJINI.
WANANCHI
WA KATA YA NYANGAMARA WAKIWA KWENYE FOLENI WAKIELEKEA KUPATA HUDUMA YA
UPIMAJI WA AFYA BAADA YA KUPEWA ELIMU YA KUJIUNGA NA CHF.NHIF OFISI YA
MKOA WA LINDI UNATEKELEZA MPANGO WA ELIMU KWA UMMA KWA KUYAFIKIA MAKUNDI
MBALIMBALI YA WANANCHI ILI KUHAKIKISHA AZMA YA KUWAFIKIA WANANCHI WOTE
WANACHANGIA MATIBABU KWA ASILIMIA 30% IFIKAPO JUNI 2015 INAFIKWA. AFISA
UANACHAMA WA WA NHIF MARGRETH JACKA AKIWAPA ELIMU YA MFUKO WA AFYA YA
JAMII SAMBAMBA NA NHIF KWA WANANCHI NA WANACHAMA WALIOJITOKEZA KUPIMA
AFYA NA ELIMU. KUSHOTO
MWANANCHI WA KATA YA NANGARU ASHA MTIMBWELE AKIJIUNGA NA CHF PAPO KWA
PAPO BAADA YA KUHAMASIKA NA KUAMUA KUUZA KUKU KWA SHS 10,000.ILI APATE
HUDUMA KWA MWAKA BAADA YA KUGUNDULIKA KUWA SHINIKIZO LA DAMU ( BP) NA
KISUKARIKULIA MRATIBU WA CHF WILAYA YA LINDI VIJIJINI GOODLUCK KHATIBU
AKIMFANYIA USAJILI NA KUPATIWA VITAMBULISHO.
WAHANGA WA MAFURIKO WAPO HATARINI .....KIGOMA
Na Magreth Magosso,Kigoma
IMEFAHAMIKA kuwa, Uongozi wa Mkoa wa Kigoma umeshindwa
kuwapatia eneo la makazi ya kuishi zaidi ya wahanga 100 waliokutwa na mafuriko mwaka jana, katika Manispaa ya kigoma Ujiji eneo la
Katosho Kata ya Kibirizi wilayani hapa kutokana na ukata wa mfuko wa Maafa huku
baadhi ya familia zikiwa hatarini kwa ubakwaji .
Pia manispaa, ilitoa mabati
chakavu 70, ili wapewe wananchi wenye
maisha duni , lakini kutokana na ukubwa wa familia hizo wameamua kuyafungia
katika ofisi ya serikali ya mtaa wa kahabwa katosho wakisubiri mchakato wa
kufidiwa kwa wahanga hao ambao eneo lao limeteuliwa kwa ajili ya mradi wa
ujenzi wa Bandari kavu.
Akifafanua hilo Mjane mmoja Bahati Luseba alisema kaya yake
ni miongoni mwa wahanga hao ambao wanaoishi kwa kutangatanga kutafuta mahali pa
kuishi hali inayowalazimu watoto wake watano wakiwemo wawili wa kike walale katika nyumba isiyosalama
huku akisubiri fedha za fidia ili ajue pa kujenga makazi maalum.
“ awali mganga wa zahanati ya jibulenu alinipa chumba kwa
muda katika zahanati yake , hili tuta ndio
eneo la kibanda changu sina msaada ,pakwenda
sina watoto wanazulula hovyo mtaani
shule wanasuasua nabeba maboksi ya dagaa ziwani ndo napata kahela ka kula na
watoto ” alisema mjane huyo.
Alisema aliishi hapo zaidi ya miaka 40 ndipo Desemaba ,2013
walipokutwa na mafuriko ,ambayo yalibomoa
nyumba yake na kumlazimu alale nje zaidi
ya miezi kumi akisubiri hatma ya malipo ya fidia kutoka serikalini ili
aondokane na adha ya kutangatanga .
Jamboleo lilimtafuta Dkt.Jibulenu ili athibitishe ikiwa alimuhifadhi
mjane huyo katika zahanati yake Dkt.Abuurashid Jibulenu akiri kufanya hivyo
kutokana na mvua kubwa iliyobomoa kaya kadhaa za umma na kudai mjane huyo ni
kuli wa kubeba mizigo mwalo wa kibirizi hivyo hali duni ya maisha inachangia watoto wake kuzulula hovyo mitaani.
Alisema zahanati ipo karibu na ilipokuwa nyumba ya mjane huyo mwenye watoto mapacha wawili wa kike wenye umri(4)baada ya diwani kudai
hana eneo la kumuhifadhi ndipo alimpatia
chumba kimoja kwa muda alale na watoto
kwa lengo la kuwaepusha na baridi na magonjwa hasa kichomi .
Alishindwa kuendelea kumhuhifadhi kutokana na sheria,kanuni
na taratibu za kikazi kuwa ,zahanati si
makazi rasmi kwa asiye mgonjwa .Naye mtendaji wa mtaa wa husika Musa Kiumbe
alisema wahanga wa mafuriko wapo mashakani hadi leo na kudai wanasubiri mthamini
mkuu aweke saini ili wafidiwe na wajue
cha kufanya.
Akijibia hilo Diwani wa kata husika Rashid Yunus ambaye pia
ni Kaimu meya wa manispaa ya kigoma ujiji alisema changamoto ya kushindwa
kuwasaidia wahanga wa mafuriko inatokana na idadai kubwa ya walengwa na
walitoa tulubai 52 kwa kaya 9 sambamba na kuyafungia mabati ili kuepusha
lawama kwa umma kutokana na hali duni za wahanga hao.
Aliongea na mkuu wa wilaya husika Ramadhan Maneno ambaye
alidai mfuko wa maafa hauna fedha za kuondoa adha za wahanga hao Jamboleo
lilimuhoji Maneno juu ya wahanga na hatma ya kusaidiwa alisema hivi`mafuriko
yalitokea mwaka jana ni sababu ipi inayowakera ‘alidai kiongozi huyo.
Maneno alisema waliokubwa na adha ya mafuriko waende katika
manispaa hiyo ili waboreshewe changamoto zao na si kumpa mzigo wa kuwajibika
kwa raia husika.Aidha uchunguzi mdogo umebaini kuwa mbali ya uongozi wa mkoa kushindwa
kuwajibika kwa walengwa.
Pia wanategea fidia zitakazotolewa na mradi wa bandari kavu ziwasaidie kupata makazi mapya wakati ilihali mthamini wa manispaa akiwa jijini Dare salaam
akisubiri saini ya mtathimini mkuu wa serikali ili wahanga wa katosho walipwe
na mradi uanze.
Huku
chama cha wandishi wa habari wanawake(Tamwa) kinadai maendeleo na GBV
yanamahusiano katika ustawi wa jamii,changamoto za umma zishughulikiwe
ili amani na utulivu udumu.
Thursday, September 11, 2014
MWANAMKE AOKOTWA IGUNGA AKIWA TAABANI,NGUO ZALOWA DAMU!!
Mwanamke mmoja ambaye amefahamika kwa jina la Sarah ameokotwa na askari Polisi huko wilayani Igunga maeneo ya Masanga akiwa na michubuko mikononi na miguuni huku nguo zake zikiwa zimelowa kwa damu.Taarifa zilizotolewa na Afisa Maendeleo ya Jamii Bi.Mwashamba Kapipi zimethibitisha kuwa mwanamke huyo ambaye amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Igunga hajatambulika na hawezi kuelezea kwa kirefu kwa mkasa uliompata.Mwashamba ametoa wito kwa jamii yeyote atakaye mtambua mwanamke huyo awasiliane nae kwa simu no. 0714 335929 au 0754 976520 au 0784 761776.
DR.KEBWE AZINDUA RASMI MFUMO WA UBORESHAJI WA UPATIKANAJI WA DAWA NA VIFAA TIBA KUPITIA MZABUNI MMOJA MKOA WA DODOMA
Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma.
Serikali imezindua rasmi Mfumo
wa uboreshaji na kusaidia upatikanaji wa Dawa na Vifaa Tiba kupitia
Mzabuni mmoja Mkoa wa Dodoma.
Uzinduzi huo umefanywa na Naibu
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Steven Kebwe katika sherehe
zilizofanyika leo mjini Dodoma na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali
wakiwemo wawakilishi kutoka Wilaya saba za Mkoa wa Dodoma.
Mhe. Dkt. Kebwe amesema kuwa
mfumo huo ni mzuri na utakuwa shirikishi kwani utahakikisha kuwa jamii
inapata mahitaji sahihi ya dawa na pia wanafanya wa sekta wanafanyakazi
kwa bidii kwa lengo la kupambana na upungufu wa dawa unaoweza
kujitokeza nchini.
Amesema kuwa moja ya vitu
vikubwa wanavyovifanya sasa ni kutekeleza sera ya Matokeo Makubwa Sasa
katika sekta ya afya kwani Barani Africa, Tanzania na Afrika ya Kusini
zimekuwa nchi zinazojitahidi kufuata mifumo mizuri ya dawa kutokana na
taarifa ya shirika la Afya Ulimwenguni (WHO).
“Mifumo hii itatusaidia na
kuboresha mahitaji ya dawa katika vituo vya afya, na hivyo kupunguza
vifo mbalimbali vinavyotokana na wananchi kutumia dawa na tiba ambazo
sio sahihi kwa sababu ya kukosa dawa katika vituo vya afya”, alisema
Mhe. Kebwe.
Hivyo Mhe. Dkt. Kebwe ameziagiza
Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma kuhakikisha zinatekeleza mfumo kwa
ufanisi ili mikoa mingine ije kujifunza kutoka kwao kwa ajili ya
kusaidia kupunguza upungufu wa dawa na vifaa vya tiba hapa nchini.
Amesema kuwa wananchi wanakwenda
katika vituo vya afya wanapenda wakute huduma nzuri na za kuridhisha
huku wakipata dawa na huduma nyingine za upimaji kwa gharama nafuu.
Aidha, Mhe. Dkt. Kebwe amefafnua
kuwa, sasahivi wameamua kuja na mfumo huo kwa kuwa utasaidia sana
kuboresha afya za wananchi na kutekeleza malengo ya Minelia.
Ameongeza kuwa Serikali
itaendelea kujipanga zaidi katika kufundisha na kuelekeza watumishi
na kutengeneza mifumo mipya ambapo kwa ajili ya kusogeza huduma karibu
na wananchi kulingana na bajeti.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt.
Rehema Nchimbi ameishukuru Serikali ya Uswisi kwa msaada mkubwa kwa
Tanzania hasa mkoani Dodoma katika Wilaya husika kwani utasaidia
kuboresha afya za wakazi wa Dodoma.
Dkt. Nchimbi ameongeza kuwa
anaamini kuwa mfumo huo utasimamia na kutekelezwa kama ilivyopangwa ili
mikoa mingine ipate kuja kujifunza kupitia mkoa wa Dodoma.
“Naomba Mhe. Mgeni rasmi wakati
tunasherehekea Uzinduzi huu, tuombe tupate mwongozo kwa udhibiti wa dawa
zinazosambaa kwa kasi kupitia vyombo vya habari”, alisema Mhe. Nchimbi.
Mfumo huo utatoa fursa kwa Duka
la Dawa la Bahari Limited kuzindua mfumo wa usambazaji wa dawa na vifaa
tiba katika vituo vya afya na Hospitali katika Wilaya zote saba za mkoa
wa Dodoma.
Duka hilo limepewa jukumu hilo
baada ya kushinda zabuni na hivyo linatarajiwa kupata fedha zake kupitia
Mfuko wa Afya ya Jamii, Mfuko wa Bima ya Afya na vyanzo mingine vya
Halmashauri za Wilaya zote.
Mfumo huo ni wa kwanza kuanza kutekelezwa hapa nchini na kwa majaribio umeanzia mkoani Dodoma chini ya mradi tuimarishe Afya.
WAGONJWA WA SARATANI WAIOMBA SERIKALI IWEZE KUTOA HUDUMA YA MATIBABU KATIKA HOSPITALI NYINGI ZAIDI
Anna Nkinda – Maelezo
11/9/2014 Serikali imeombwa
kuangalia uwezekano wa kutoa huduma ya matibabu ya ugonjwa wa saratani
za wanawake kwenye Hospitali zingine nchini kwani hivi sasa huduma hiyo
inatolewa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road pekee.
Ombi hilo limetolewa leo na
wanawake wanaokabiliwa na tatizo la ugonjwa wa saratani ya mlango
wa kizazi na matiti wakati wakiongea na waandishi wa habari
waliohudhuria mkutano wa siku tatu wa saratani za wanawake unaofanyika
katika Hoteli ya Court Yard jijini Dar es Salaam.
Wanawake hao walisema inachukua
muda mrefu pale ambapo utagundulika una ugonjwa wa saratani hadi kupata
matibabu lakini kama huduma hiyo itatolewa katika Hospitali zingine
itarahisisha kwa mgonjwa kupata matibabu kwa wakati.
Mmoja wa wanawake anasumbuliwa na
saratani ya titi alisema wanawake wengi wanafikiria ukiugua saratani
unakwenda kufa jambo ambalo siyo kweli kwani yeye ameishi na ugonjwa huo
kwa muda wa miaka 16 sasa.
“Nawashauri wanawake wenzangu
waende kufanya vipimo vya mara kwa mara kwani kuna vipimo ambavyo
ukipima utajua kama unatatizo au la na kama utakutwa na
ugonjwa utapata dawa mapema”, alisema mgonjwa huyo.
Naye mmoja wa wanawake anayeumwa
ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi alisema dalili ya kwanza
aliyoiona ni kutokwa na damu ukeni akaamua kwenda kufanya vipimo na
baada ya kukutwa na tatizo akapata matibabu katika Taasisi ya Saratani
ya Ocean Road.
“Nawashauri wanawake wenzangu
wakiona dalili za ugonjwa huu wasikae kimya na kujidanganya kwa kutumia
dawa za miti shamba bali wawahi Hospitali mapema ambako watapata
matibabu na kupona. Mimi nilipata tatizo la ugonjwa huo mwaka 2011
nilitibiwa na kupona”, alisema.
Kwa upande wake Dkt. Sara Maongezi
ambaye ni Mkurugenzi wa uboreshaji Afya kutoka Taasisi ya Wanawake na
Maendeleo (WAMA) alisema Saratani ya mlango wa kizazi ni moja ya
saratani inayoongoza kwa kuua wanawake wengi nchini.
Alisema mkutano huo ambao
umehudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka nchi za Kenya, Uganda, Malawi,
Zambia, Madagasca, Rwanda na Burundi unalengo la kuwafanya wanawake
waweze kuufahamu ugonjwa huo ili waweze kujikinga kwa wale ambao
hawajapata na kwa walioupata waweze kuwahi mapema Hospitali kwa ajili ya
kupata huduma za matibabu.
“Baada ya Mkutano huu tutatoka
na maazimio ambayo tutayafanyia kazi na kuona jinsi gani tunaweza
kuboresha utendaji wetu wa kazi za kuielimisha jamii kuhusu ugonjwa
huu”, alisema Dkt. Maongezi.
Dkt. Maongezi alisema, katika
nchi za Afrika ya Mashariki takwimu zinaonyesha Tanzania inaongoza kuwa
na wagonjwa wengi wa saratani za wanawake lakini bado hakuna ukusanyaji
sahihi wa takwimu kwani wagonjwa wengi wanafia majumbani na wanaofika
Hospitali kupata matibabu ni wachache.
Walengwa wa mkutano huo ni
wanawake wanaoishi na saratani pamoja na Asasi zinazofanya kazi za
saratani lengo lake ni kwa wadau hao kuweza kuilemisha jamii ili iweze
kuchukua hatua dhidi ya ugonjwa huo.
Mkutano huo umeandaliwa na
Women’s Empowerment Cancers Advocacy Network, (WE CAN) kwa kushirikiana
na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) na Wizara ya Afya na Ustawi
wa Jamii pamoja na wadau wengine wa Saratani .
WATANZANIA WAASWA KUTUNZA VIPATO VYAO WAWE NA MAISHA BORA
Mwezeshaji
wa Taasisi ya MAYEPS Tanzania Lucas Marco (kulia) akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) hivi karibuni jijini Dar es salaam
wakati wa uzinduzi wa kitabu kiitwacho “NITUNZE NIKUTUNZE FAINALI
UZEENI”, chenye maudhui ya kuwasaidia watu wanaofanyakazi ya kujiajiri
au kuajiriwa kufanya maamuzi yaliyosahihi ili waweze kuishi maisha bora
wakati wakiwa kwenye ajira na baada ya kustaafu. Katikati ni Mwenyekiti
wa Taasisi hiyo Rose Mang’enya na kushoto ni Meneja wa Taasisi hiyo John
Masumba Mwezeshaji
wa Taasisi ya MAYEPS Tanzania Lucas Marco (wa pili kulia) akimpongeza
Mwenyekiti wa Taasisi ya MAYEPS Tanzania Rose Mang’enya wakati wa
uzinduzi wa kitabu kiitwacho “NITUNZE NIKUTUNZE FAINALI UZEENI” hivi
karibuni jijini Dar es salaam. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Taasisi
hiyo John Masumba na Afisa Habari Idara ya Habari MAELEZO Eleuteri mangi
(kulia).
(Picha na MAELEZO)
……………………………………………………
BeatriceLyimo- MAELEZO
Taasisi isiyo ya kiserikali ya
MAYEPS Tanzania imezindua kitabu kiitwacho “NITUNZE NIKUTUNZE FAINALI
UZEENI”, chenye maudhui ya kuwasaidia watu wanaofanyakazi ya kujiajiri
au kuajiriwa kufanya maamuzi yaliyosahihi ili waweze kuishi maisha bora
wakati wakiwa kwenye ajira na baada ya kustaafu.
Akizungumza na waandishi wa habari
hivi karibuni jijini Dar es salaam, Meneja wa Taasisi hiyo John Masumba
amesema kuwa uzoefu unaonesha kuwa wafanyakazi katika jamii ya
Kitanzania hawaweki akiba kwa ajili ya kuwekeza kwa madhumuni ya kujenga
uchumi.
Meneja Masumba amesisitiza kuwa
MAYEPS imetambua kwamba ikiandaa warsha moja kwa mwezi juu wafanyakazi
kufanya maamuzi yaliyo sahihi, itawafikia watu 600 kwa mwaka.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Taasisi hiyo Rose Mang’enya aliwapitisha waandishi wa habari juu ya
yaliyomo kwenye kitabu hicho kwa kuendesha warsha fupi iliyowafungua
macho waandishi hao kuhusu namna ya kutunza fedha kuandaa maisha ya
baadaye.
Akinukuu kauli ya mtaalamu wa
uongozi John Maxwell Mwenyekiti huyo alisema kuwa “Watu wanaofanikiwa na
wasiofanikiwa hawatofautiani sana kiuwezo bali wanatofautiana katika
dhamira ya kufika kilele au upeo wa uwezo wao”.
Mang’enya aliongeza kuwa jukumu la
kujenga maisha binafsi lipo kwa muhusika binafsi, hivyo, watumishi
wawe na msimamo sahihi utakaowawezesha kuwa na maisha bora.
Aidha, MAYEPS hutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa Umama na binafsi namna ya kupanga matumizi.
Pia hutoa mafunzo ambayo
yatawezesha wafanyakazi kutambua kuwa fedha za mafao au pensheni
hupungua thamani mwaka hadi mwaka hivyo uwekezaji wa fedha hizo ni
muhimu ufanywe kwa uangalifu.
TAMWA YAWAFUNDA WANDISHI WA HABARI KATAVI,RUKWA NA KIGOMA KUHUSU UKATILI WA KIJINSIA
WANDISHI wa Habari wameaswa kutumia kikamilifu kalamu zao
kuandika athari za ndoa za utotoni na madhara ya ubakaji katika jamii kwa lengo la kutokomeza vitendo hivyo.
Hali hiyo inachangiwa na sehemu kubwa ya jamii kutokujali,kuwajibika
katika kutoa taarifa ya matukio hayo
ambapo kila kukicha vitendo
hushamiri ili hali viongozi wa serikali,wanasiasa na watumishi
wa mungu wanashindwa kubabanua athari na
madhara kwa walengwa kulingana na nafasi
zao.
Akifafanua hilo
Judica Losai ambaye ni msimamizi wa vipindi vya redio kutokaChama cha
Wanahabari Tanzania (Tamwa) alisema dhima ni
kuelimisha umma juu ya athari ya kufumbia macho
vitendo hivyo ambavyo
ni chachu kwa wahanga kuishi kwa kisasi,uoga,chuki dhidi ya jinsia
Fulani kulingana na tukio lilompata awali.
Wandishi wanafursa kubwa kuiboresha jamii husika endapo
itatumia kalamu kubadilisha mfumo kike unaondekeza mfumo dume ambao ni chanzo
cha ukatili wa kijinsia kwa makundi hatarishi hasa wanawake na watoto ambao
ndio wahanaga wa ndoa za utotoni na
ubakwaji.
Kwa upande wa mkufunzi wa mafunzo hayo Deo Mushi alisema
kutokana na elimu hiyo itasaidia wandishi
wa mikoa ya katavi,Rukwa na kigoma kubaini
uhalisia wa matukio katika jamii husika na namna ya kupambana
na ukatili wa ndoa za utotoni na ubakwaji ili jamii tambue athari za mila potofu
zinavyochangia vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Pia kuibua vitendo mbalimbali vya ukatili dhidi ya
wahanga wanaoathirirka na jamii inayofumbia macho matukio hayo kwa maslai
binafsi ambapo inachangia
changamoto ya kuwa na kizazi chenye kuzingatia haki na maadili
mema siku za usoni.
Aidha wametoa wito kwa vyombo vya habari wabadilike kwa
kutoa kipaumbele habari za ukatili wa kijinsia ili kuhamasisha umma wachane na mfumo wa maisha hasi kwenda chanya kwa kuzingatia mila na desturi.
Baadhi ya wafundwa wa
mafunzo hayo ya siku tatu Diana Rubanguka , Irene Temu na Peti Siyame kwa
nyakati tofauti wakili kupitia mafunzo
hayo ni mwanga wa kubaini habari zenye viashiria vya ukatili wa
kijinsia na watawajibika katika jamii
kwa kuibua na kueleimisha madhara na hatua kwa wahanga ili desturi zenye
kuboresha haki,utu wa kila mmoja ili
lengo la kuboresha mahusiano katika jamii husika.
MWANAFUNZI WA DARASA LA SABA ABAKWA AINGIA CHUMBA CHA MTIHANI AKIWA HOI ...KIGOMA
MWANAFUNZI mmoja anayesoma Darasa la saba shule ya msingi
Bukuba (14) wilaya
ya Buhigwe Mkoa wa Kigoma ahofiwa kufeli mtihani wake wa mwisho wa leo (jana)
kutokana na kitendo cha kubakwa na
kijana Amon Samweli (25) ambaye pia mkazi wa kijiji cha mwanga B wilayani humo.
Alisema saa 12 jioni siku
ya jumapili ,alimtuma mtoto huyo kwenda dukani kuchukua simu, lakini binti yake
alichelewa kurudi na aliporudi akamwambia mama yake kuhusu alichotendewa na
Amoni Samwel.
Alichanganyikiwa baada ya kupata habari hiyo kutokana na
hofu na hisia hasi kutoka kwa jamii na alipomchunguza aliona akitokwa na damu nyingi sehemu nyeti
ambazo zilitapakaa kwenye makalio ndipo akampigia simu baba yake kabla ya kwenda kwenye vyombo vya sheria.
Alitoa taarifa katika
kituo cha polisi cha wilayani hapo na kuandika mashtaka na kupewa PF3 kwa ajiri ya
kupata matibabu katika kituo cha afya cha wilayani hapo na kufanyiwa vipimo
vyote hasa ukimwi na magonjwa ya zinaa .
Wakati
huohuo Chama cha wandishi wa habari (Tamwa) waliwasihi wandishi wa
habari kanda magharibi wajikite kuibua habari zenye viashiria vya
ukatili wa kijinsia hasa ubakwaji na ndoa za utotoni.
Aliwauliza walichokuwa wanafanya, nao wakamjibu kuwa wanasoma ghafla Amoni akaanza kumpiga makofi yule mwananfunzi mwenzake
sanjari na kumfukuza eneo lile na kumshikia kisu na kumbeba juu juu na kumpelekea katika shamba la migomba
na kumtendea unyama huo.
Nae Afisa Ustawi wa Jamii wa
hapo Godfrey Kapaya alisema kuwa walifika nyumbani kwa mwanafunzi huyo
na kumfanyia vipimo vilivyothibitisha tukio hilo na alikuwa na majeraha sehemu za siri sanjari na kumpatia dawa za kupunguza
maumivu, kuzuia maambukizi ya magonjwa ya zinaa pamoja na mimba” alisema
Kapaya.
Kapaya aliongeza kuwa kwakuwa mwanafunzi alitakiwa kuingia
kwenye mtihani walimpa ushauri wa kumuondolea
hofu ili afanye mtihani akiwa katika
hari nzuri ya kimawazo.
Kamanda wa Polisi
Mkoani Kigoma, Japhari Muhamed alithibitisha tukio hilo na kuongeza kuwa
mtuhumiwa tayari yuko mahabusu na hatua za kumfikisha mahakamani zinaendelea.ingawa
awali kuna tetesi kuwa mtuhumiwa aliachiwa siku septemba ,8,2014ilihali
alitenda kosa hilo siku ya 7,septemba 2014.
MSHINDI WA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) 2014, MWANAAFA MWINZAGO APOKELEWA KWA SHANGWE NA NDELEMO MKOANI KWAO MTWARA
Mara baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara, Mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 Mwanaafa Mwinzago akitoa Maneno ya Shukrani kwa Wakazi wa Mtwara waliojitokeza kuja Kumpokea uwanja wa Ndege wa Mtwara mapema Leo. Vilevile alitoa Shukrani zake zote kwa Watanzania Wote kwa Kuweza umpigia Kura na Kumfanya aibuke mshindi wa Milioni 50 za Tanzania katika fainali ya Shindano la Kusaka vipaji vya Kuigiza lijulikanalo Kama Tanzania Movie Talents (TMT).
Wapenzi, Mashabiki na wana Mtwara wakiwa Nje ya Uwanja wa Ndege wa Mtwara wakisubiri Kumpokea Mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 Mwanaafa Mwinzago kwaajili ya Kumpongeza kwa Kuibuka MShindi wa SHilingi Milioni 50 za Kitanzania katika Fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT)lililofanyika Mwisho wa Mwezi wa nane katika Ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar Es Salaam.
Wakazi wa Mkoa wa Mtwara wakimpongeza Mshindi wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago ambaye amewasili Mkoani Mtwara ambapo ndio Nyumbani Kwao akitokea Dar Es Salaam mara baada ya Kuibuka Mshindi na Kujinyakulia Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania.
Ndugu, Jamaa na Marafiki wa Mshindi wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago wakipiga picha ya Pamoja mara baada ya Kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara akitokea Dar Es Salaam.
Shangwe na Ndelemo zilitawala katika Viunga Vya Uwanja wa Ndege wa Mtwara kabla na Baada ya Mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014, Mwanaafa Mwinzago kutua katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara akitokea Dar Es Salaam ambapo fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) lilifanyika katika Ukumbi wa Mlimani City.
Msafara wa Kuelekea Nyumbani Kwa MShindi wa TMT 2014 , Mwanaafa Mwinzago Ukitoka katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara.
Msafara Ukielekea Nyumbani kwa Mshindi wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago,
Wazee kwa Vijana wakimpongeza Mwanaafa Mwinzago wakati alipokuwa akipelekwa Nyumbani Kwao kwa Msafara wakati akitokea Uwanja wa Ndege
Vijana nao wakimpongeza Mshindi wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI»