Pages

KAPIPI TV

Thursday, September 11, 2014

MWANAFUNZI WA DARASA LA SABA ABAKWA AINGIA CHUMBA CHA MTIHANI AKIWA HOI ...KIGOMA

Na Magreth Magosso, Kigoma.
 
MWANAFUNZI mmoja anayesoma Darasa la saba shule ya msingi Bukuba  (14)   wilaya ya Buhigwe Mkoa wa Kigoma ahofiwa kufeli mtihani wake wa mwisho wa leo (jana) kutokana na kitendo cha kubakwa  na kijana Amon Samweli (25) ambaye pia mkazi wa kijiji cha mwanga B wilayani humo.
 
 
Alisema  saa 12 jioni siku ya jumapili ,alimtuma mtoto huyo kwenda dukani kuchukua simu, lakini binti yake alichelewa kurudi na aliporudi akamwambia mama yake kuhusu alichotendewa na Amoni Samwel.
 
Alichanganyikiwa baada ya kupata habari hiyo kutokana na hofu na hisia hasi kutoka kwa jamii na alipomchunguza  aliona akitokwa na damu nyingi sehemu nyeti ambazo zilitapakaa kwenye makalio ndipo akampigia simu baba yake  kabla ya kwenda kwenye vyombo vya sheria.
 
Alitoa  taarifa katika kituo cha polisi  cha wilayani hapo na  kuandika mashtaka na kupewa PF3 kwa ajiri ya kupata matibabu  katika  kituo cha afya  cha wilayani hapo na kufanyiwa vipimo vyote  hasa ukimwi na magonjwa ya zinaa .
 
Wakati huohuo Chama cha wandishi wa habari (Tamwa) waliwasihi wandishi wa habari kanda magharibi wajikite kuibua habari zenye viashiria vya ukatili wa kijinsia hasa ubakwaji na ndoa za utotoni.


Kwa upande wa mwanafunzi husika (linahifadhiwa,)  alisema kuwa baada ya kutumwa na mama yake alikutana na mwanafunzi mwenzake wa kiume na kumuomba amuelekeze walichofundishwa darasani na ndipo Amoni Samweli alipowakuta.
 
Aliwauliza walichokuwa wanafanya, nao  wakamjibu kuwa wanasoma ghafla Amoni  akaanza kumpiga makofi yule mwananfunzi mwenzake sanjari na kumfukuza eneo lile na kumshikia kisu na kumbeba  juu juu na kumpelekea katika shamba la migomba na kumtendea unyama huo.
 
 
Nae Afisa Ustawi wa Jamii wa  hapo Godfrey Kapaya alisema kuwa walifika nyumbani kwa mwanafunzi huyo na kumfanyia vipimo vilivyothibitisha tukio hilo na alikuwa na majeraha sehemu  za siri sanjari na kumpatia dawa za kupunguza maumivu, kuzuia maambukizi ya magonjwa ya zinaa pamoja na mimba” alisema Kapaya.
 
Kapaya aliongeza kuwa kwakuwa mwanafunzi alitakiwa kuingia kwenye mtihani walimpa  ushauri wa kumuondolea hofu  ili afanye mtihani akiwa katika hari nzuri ya kimawazo.
 
 
 Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma, Japhari Muhamed alithibitisha tukio hilo na kuongeza kuwa mtuhumiwa tayari yuko mahabusu na hatua za kumfikisha mahakamani zinaendelea.ingawa awali kuna tetesi kuwa mtuhumiwa aliachiwa siku septemba ,8,2014ilihali alitenda kosa hilo siku ya 7,septemba 2014.

No comments: