Pages

KAPIPI TV

Friday, September 12, 2014

WAHANGA WA MAFURIKO WAPO HATARINI .....KIGOMA

 
Na Magreth Magosso,Kigoma
 
IMEFAHAMIKA kuwa, Uongozi wa Mkoa wa Kigoma umeshindwa kuwapatia eneo la makazi ya kuishi zaidi ya wahanga 100 waliokutwa na mafuriko mwaka jana,  katika Manispaa ya kigoma Ujiji eneo la Katosho Kata ya Kibirizi wilayani hapa kutokana na ukata wa mfuko wa Maafa huku baadhi ya familia zikiwa  hatarini kwa ubakwaji .
 
Pia  manispaa, ilitoa mabati chakavu 70, ili wapewe  wananchi wenye maisha duni , lakini kutokana na ukubwa wa familia hizo wameamua kuyafungia katika ofisi ya serikali ya mtaa wa kahabwa katosho wakisubiri mchakato wa kufidiwa kwa wahanga hao ambao eneo lao limeteuliwa kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa Bandari kavu.
 
Akifafanua hilo Mjane mmoja Bahati Luseba alisema kaya yake ni miongoni mwa wahanga hao ambao wanaoishi kwa kutangatanga kutafuta mahali pa kuishi hali inayowalazimu  watoto wake  watano wakiwemo  wawili wa kike walale katika nyumba isiyosalama huku akisubiri fedha za fidia ili ajue pa kujenga makazi maalum.
 
“ awali mganga wa zahanati ya jibulenu alinipa chumba kwa muda katika zahanati yake ,  hili tuta ndio eneo la  kibanda changu sina msaada ,pakwenda sina  watoto wanazulula hovyo mtaani shule wanasuasua nabeba maboksi ya dagaa ziwani ndo napata kahela ka kula na watoto ” alisema mjane huyo.
 
Alisema aliishi hapo zaidi ya miaka 40 ndipo Desemaba ,2013 walipokutwa na mafuriko ,ambayo  yalibomoa nyumba yake na kumlazimu alale nje  zaidi ya miezi kumi akisubiri hatma ya malipo ya fidia kutoka serikalini ili aondokane na adha ya kutangatanga .
 
Jamboleo lilimtafuta Dkt.Jibulenu ili athibitishe ikiwa alimuhifadhi mjane huyo katika zahanati yake Dkt.Abuurashid Jibulenu akiri kufanya hivyo kutokana na mvua kubwa iliyobomoa kaya kadhaa za umma na kudai mjane huyo ni kuli wa kubeba mizigo mwalo wa kibirizi hivyo hali duni ya maisha inachangia  watoto wake kuzulula hovyo mitaani.

Alisema zahanati ipo karibu na ilipokuwa nyumba ya mjane  huyo mwenye watoto mapacha wawili  wa kike wenye umri(4)baada ya diwani kudai hana eneo la kumuhifadhi ndipo  alimpatia chumba kimoja kwa muda  alale na watoto kwa lengo la kuwaepusha na baridi na magonjwa hasa kichomi .
 
Alishindwa kuendelea kumhuhifadhi kutokana na sheria,kanuni na taratibu za kikazi kuwa ,zahanati  si makazi rasmi kwa asiye mgonjwa .Naye mtendaji wa mtaa wa husika Musa Kiumbe alisema wahanga wa mafuriko wapo mashakani hadi leo na kudai wanasubiri mthamini mkuu aweke saini ili  wafidiwe na wajue cha kufanya.
 
Akijibia hilo Diwani wa kata husika Rashid Yunus ambaye pia ni Kaimu meya wa manispaa ya kigoma ujiji alisema changamoto ya kushindwa kuwasaidia wahanga wa mafuriko inatokana na idadai kubwa ya walengwa  na  walitoa tulubai 52 kwa kaya 9 sambamba na kuyafungia mabati ili kuepusha lawama kwa umma kutokana na hali duni za wahanga hao.
 
Aliongea na mkuu wa wilaya husika Ramadhan Maneno ambaye alidai mfuko wa maafa hauna fedha za kuondoa adha za wahanga hao Jamboleo lilimuhoji Maneno juu ya wahanga na hatma ya kusaidiwa alisema hivi`mafuriko yalitokea mwaka jana ni sababu ipi inayowakera ‘alidai kiongozi huyo.
 
Maneno alisema waliokubwa na adha ya mafuriko waende katika manispaa hiyo ili waboreshewe changamoto zao na si kumpa mzigo wa kuwajibika kwa raia husika.Aidha uchunguzi mdogo umebaini kuwa mbali ya uongozi wa mkoa kushindwa kuwajibika kwa walengwa.
 
Pia wanategea fidia zitakazotolewa na mradi  wa bandari kavu  ziwasaidie kupata makazi mapya wakati ilihali  mthamini wa manispaa akiwa jijini Dare salaam akisubiri saini ya mtathimini mkuu wa serikali ili wahanga wa katosho walipwe na mradi uanze.

Huku chama cha wandishi wa habari wanawake(Tamwa) kinadai maendeleo na GBV yanamahusiano katika ustawi wa jamii,changamoto za umma zishughulikiwe ili amani na utulivu udumu.

No comments: