Pages

KAPIPI TV

Saturday, April 19, 2014

KIGOMA WATAKA WABUNGE BUNGE MAALUMU LA KATIBA KURUDISHA POSHO


Na Magreth Magosso,Kigoma


WAJUMBE wa Bunge maalum  la  Katiba  waliokacha kikao hivi karibuni wametakiwa warudishe posho za kikao kutokana na kitendo chao cha kushindwa kuwa na demokrasia kwa kuvumilia changamoto mbalimbali zinazotokea katika mijadala muhimu ya kujadili rasimu ya katiba ya watanzania.


Hayo yamebainika kufuatia maoni ya baadhi ya wananchi wa  manispaa ya kigoma ujiji wakati wakizuya wabunge kuvikao vya bunge hilo vinavyoendelea mjini Dododma kwa madai ya kubaguliwa, kutukanwa na kudhalilishwa na wabunge wa chama  tawala, CCM.

Katibu wa Chama cha NRA Taifa Fadhili Kiswaga alisema mijadala inayoendelea katika bunge hilo linawachosha watanzania kusikia viloja visivyo na mashiko kwa umma badala yake wawakilishi walio wengi wapo kwa ushabiki wa kichama badala ya kujenga taifa  kwa kuzingatia hoja zenye mashiko na maslai ya wananchi.


“kitendo cha kutoka nje hakina maana kwetu,basi warudishe na posho kama wanashindwa kupigania hoja mezani  na si kususa  mimi naona waliotoka nje si wazalendo ,mzalendo hachoki kutetea haki za msingi ikiwa ana hoja zenye mashiko” alibainisha Kiswaga.


Mwalimu Alphonce Mbasa    alisema baadhi ya wabunge  wapo katika kubaguana hali ambayo ni mbaya kwa umma pamoja na itikadi ya kichama,badala ya kujadili kilicholetwa na tume ya rais iliyongozwa na Jaji Sinde Warioba kwa  maana ya  kuboresha kilichopo na si kulazimisha mambo yasiyo katika waraka huo.


Akinukuu sheria ya rasimu hiyo namba 83 kipengele cha 23,24,25,26 na waraka husika unabainisha watajadili kile kilichoko kwenye rasimu ,pia suala la muungano ni makubaliano baina ya watanganyika na watu wa Zanzibari huku akidai kitendo cha kutoka nje kwa baadhi ya wabunge ni moja ya kuonyesha kile kilichopo ni batili .

Antony Kayanda alisema kitendo cha wabunge kutoa hoja za ukabila ni chachu ya kuwagawa wananchi wanaofuatilia mijadala hiyo hali inayokwaza walengwa wa katiba hiyo hasa wakulima na wanyonge waliosahulika na serikali kutokana kukosa  elimu  ya uraia kubaini uhalisia wa mambo kulingana na matamshi ya baadhi ya wabunge wenye hulka ya kuweka utabaka wa ukabila na udini.


Naye Mratibu wa Asasi ya Ndela Youth Development ya hapa Adolfu Leopard aliwashauri wabunge hao wasihofu mikinzano ya hoja,badala yake waongeze uzalendo kwa kufafanua hoja zao na wachie wananchi wafanye maamuzi kwenye kupiga kura juu ya walichoboresha na si kususia vikao.

Thursday, April 17, 2014

KINANA AMALIZA ZIARA WILAYA YA MLELE


1._Kinana__akikabidhi_kadi_kwa_mmoja_wa_wanachama_wampya_wa_CCM__katika_kikao_cha_shina_kilichofanyika_nyumbani_kwa_balozi_wa_shina_namba_tano_tawi_la_Nsimbo_Joseph_Wavuu_49d03.jpg
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana  akikabidhi kadi ya CCM kwa mmoja wa wanachama wampya wa CCM Geofrey Mbwaga, katika kikao cha shina kilichofanyika nyumbani kwa balozi wa shina namba tano, tawi la Nsimbo, Joseph Wavuu, wilaya ya Mlele mkoani Katavi, leo, Aprili 16, 2014, akiwa katika ziara ya kuimarisha uhai wa Chama na kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama wilayani humo
3._Nape_akizungumza_na_Mzee_aarom_Kasilo_wakati_wa_kikao_kilichohudhuriwa_na_Kinana_nyumbani_kwa_balozi_wa_shina_namba_tano_tawi_la_Nsimbo_Joseph_Wavuu_0c1d4.jpg
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Mjumbe wa Shina namba tano, Mzee Aarom Kasilo, wakati wa kikao kilichohudhuriwa na Kinana nyumbani kwa balozi wa shina hilo, tawi la Nsimbo, Joseph Wavuu, leo, Aprili 16, 2014, akiwa katika ziara ya kuimarisha uhai wa Chama na kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama wilayani humo
7._Kinana_akikagua_ujenzi_wa_kisima_cha_maji_Kijiji_cha_Nsimbo_3_497f2.jpg
6._Kinana_akishiriki_kufyatua_matofali_ujenzi_wa_kisima_cha_maji_Kijiji_cha_Nsimbo_3_04529.jpg
  Kinana akibeba tofali baada ya kulifyatua waliposhiriki kufyatua matomali kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa kisima cha maji wa kijiji cha Mwenge, katika Halmashauri ya Nsimbo, leo, Aprili 16, 2014, akiwa katika ziara ya kuimarisha uhai wa Chama na kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama wilayani humo.

MPANGO MKAKATI WA NATIONAL HOUSING CORPORATION MKOA WA KATAVI/RUKWA 2010/2011

9
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Shirika la Nyumba Mkoa wa Katavi  Ndugu Nehemia Msigwa juu ya miradi ya ujenzi wa nyumba itakayofanyika ndani ya mkoa wa Katavi.7 Pichani ni Michoro ya Nyumba zitakazojengwa mkoani Katavi na Shirika la Nyumba ya Taifa,ambapo wilaya ya Mlele ,Shirika la Nyumba linajenga nyumba 60 na zitachukua  miezi nane kukamilika. 
…………………………………………………………………………….
Shirika la Nyumba Mkoa wa Katavi/Rukwa  umejizatiti katika kutekeleza mpango Mkakati wa Shirika wa miaka mitano yaani 2010/2011 hadi 2014/2015 kama ilivyokwa mikoa mingine katika Shirika la Nyumba la Taifa. 

Mpango huu umekuja wakati mwafaka kushughulikia tatizo la uhaba wa nyumba za makazi na biashara kwa Mkoa huu wa Katavi/Rukwa. Katika Mpango Mkakati huu, Shirika limejiwekea Dira, Dhima, Maadili ya Msingi, Malengo na Matarajio ya Shirika.

Wakati  Utekelezaji wa Mpango huu unaendelea kwa sasa,  unasaidia sana katika kukuza uchumi kwa katika mkoa wetu kwa njia ya kuongeza Ajira mbalimbali pamoja na kodi, na hili linatokana na uwezo mkubwa wa sekta ya Nyumba katika kukuza uchumi katika eneo husika. 

Zaidi sana ni Msisitizo wetu NHC-Katavi/Rukwa kuwa,  Maendeleo ya Mikoa hii, lazima yaendane na Ujenzi wa Nyumba Bora za Makazi na za Biashara.

 Na kwa hili NHC tunaelekea kukamilisha malengo yetu mawili ya kuwa Kiongozi Mahiri katika Kuendeleza Milki na Pia kuwa Msimamizi Mahiri wa Miliki si hapa Katavi tu bali Tanzania Nzima.

Kwa sasa kuna miradi Mitano ambayo ipo katika hatua mbalimbali ambayo inatekelezwa na Shirika katikakufikia malengo shirika tuliyojiwekea.

Kuna Mradi wa Ilembo ambao unatarajiwa kukamilika 30/Mei/2014. Mradi huu una jumla ya nyumba 90. Ni mradi mkubwa kwa eneo kama la Mpanda ambao utakuwa name gharama ya said I ya Tsh. 3.1 Bil. kuwepo na umesaidia sana kutia hamasa kwa wananchi wa Mpanda kuongeza kasi katika sekta ya ujenzi wa Nyumba, pia umesaidia kuleta mandhari bora ya makazi. 

Ni matarajio yetu,  kwa kuwa tumeshaanza kuuza nyumba hizo,  Taasisi za Serikali, Mashirika ya Umma, Mashirika Binafsi, Halmashauri za Miji ambazo katika mkoa wa katavi watumishi wake wengi wanakosa Nyumba bora za kuishi watazichangamkia Nyumba hizi kwa kuzinunua na kuwapangiza watumishi wake. 

Vilevile ni matarajio yetu kuwa Wananchi nao kila mmoja binasfi watajitokeza kwa wingi kununua Nyumba hizi ambazo ni Bora kwa makazi.

Katika Wilaya Mpya ya Mlele, Mradi wa nyumba za Gharama nafuu upo katika hatua za awali, ni mmatarajio yetu mara baada kukamilika kwa Mradi huo tatizo la uhaba wa nyumba Bora za Kuishi pale Inyonga, ambapo ndipo makao makuu ya Wilaya, litakuwa limedhibitiwa kwa kiasi kikubwa, rai yetu ni ileile kwa taasisi za serikali, Mashirika ya Umma, pamoja na Mashirika Binasfi zichangamkie fursa hiyo ya kupata nyumba kwa ajili ya Watumishi wake.

Miradi kama hii ya Ilembo-Mpanda pamoja na Inyonga tunatarajia pia kuipeleka katika Wilaya za Kalambo pamoja na Nkasi mkoa wa Rukwa na Halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi. Miradi katika wilaya hizi itaanza mara tu taratibu husika zitakapo kamilika. 

Ninatoa Ari kuwa halmashauri ambazo zitatoa ushirikiano chanya kwa NHC katika kutatua tatizo hili la uhaba wa nyumba bora za makazi kwa wafanyakazi wake na wananchi kwa ujumla ndio itakayofikiriwa zaidi, hii ni pamoja na changamoto za bei kubwa za Viwanja tunazokumbana nazo kutoka kwa halmashauri husika.

Katika orodha ya Miradi ambayo ipo katika Mkoa huu ni pamoja na Mradi wa Jengo la Biashara litajengwa katika eneo la Paradise-Mpanda hapa Mkoani Katavi na Mradi wa Nyumba za Makazi katika eneo la Jangwani-Sumbawanga Mkoani Rukwa.  

Miradi hiyo yote imeshatangazwa kwa ajili ya Kupata wakandarasi watakao jenga miradi hiyo, hivyo muda si mrefu miradi hiyo itaanza rasmi.

Katika hatua nyingine, ili kutatua tatizo la uhaba wa kumbi za mikutano, Shirika la Nyumba la Taifa kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mji ya Mpanda watajenga Ukumbi wa Kisasa wa Mikutano katika eneo la madini (Madini Plot). 

Huu ni mradi mwingine katika Mji wa Mpanda ambao si tu utaleta mandhari nzuri kwa Mkoa wa Katavi bali pia Utafanya Mkoa wa Katavi kuwa Kitovu cha mikutano muhimu ya Ushirikiano kwa mikoa ya kanda hii ya ziwa Tanganyika na Nchi jirani, hivyo pia kuchangai ukuaji wa uchumi katika mkoa huu.

Napenda pia kuchukua fursa hii kuzishauri Halmashauri za Miji taasisi za serikali, mashirika ya umma yote yanao jiusisha na utoaji wa huduma za miundo mbinu (Maji, Umeme pamoja na Barabara) kuwa sisi NHC ni wabia wao wakubwa kwani tunachangia kwa kiasi kikubwa kuwatafutia wateja wapya katika kila Mradi husika. 

Hivyo pindi tunapoanza ama hata kabla ta kuanza mradi husika huduma zao zinahitajika.

MPANGO WA SHIRIKA LA NYUMBA WA KUSAIDIA VIJANA KWENYE HALMASHAURI ZA WILAYA NA MIJI MASHINE ZA KUFYATULIA MATOFALI
Katika kuunga mkono jitihada za dhati zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  kuongeza ajira za vijana na kupunguza umaskini hapa nchini na hasa Mikoa ya Katavi na Rukwa, Shirika limeamua kutoa mashine za kufyatulia matofali kwa Halmashauri zote zilizoko katika Mikoa hii, zikiwemo Halmashauri za Mlele, Nsimbo, Mpanda Mji pamoja na Halmashauri ya Mpanda Vijijini kwa Mkoa wa Katavi, Pia Halmashauri Manispaa ya Sumbawanga, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi-Namanyere Pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo katika Mkoa wa Rukwa.

Mashine hizo zitatumiwa na vikundi vya vijana vitakavyoundwa na Halmashauri kwa kushirikiana na Meneja wa Mikoa wa NHC. Kila kikundi cha vijana kitapewa msaada wa mashine nne (4) ambazo, kila mashine itakuwa ikihudumia vijana wapatao 10 hivyo vijana 40 katika kila Halmashauri.  

Pamoja na msaada wa mashine, Shirika litatoa Shilingi laki tano (500,000/=) kwa kila kikundi kama kianzio cha vijana hao kununua vifaa muhimu vya kuwezesha kazi ya kufyatua matofali kuanza. Aidha, vikundi hivyo vya vijana vitaweza baadae kuunda SACCOS zao na hivyo kupanua shughuli zao za kiuchumi.

Ili kufanikisha mpango huo,  Shirika kwa kushirikiana na Wakala wa Utafiti wa Vifaa Bora vya Ujenzi wa Nyumba (NHBRA) iliyo chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, pamoja na Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA) litatoa mafunzo ya siku 21 kati ya mwezi Desemba 2013  na Januari 2014 kwa wakufunzi wapatao 50, ya namna ya kutumia mashine hizo. 

Wataalam hawa ndio watakaotumika katika kuvifundisha vikundi vya vijana katika Halmashauri kuanzia mwezi Januari hadi Juni 2014.

Shirika la Nyumba la Taifa linatanguliza Shukrani kwa kutuunga mkono katika kufanikisha jambo hili muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu.

“KATAVI  BILA UMASIKINI INAWEZEKANA, KWA KUWA MAISHA NI NYUMBA” 
MAISHA YANGU NYUMBA YANGU 
 IMETOLEWA NA 
NEHEMIA L. MSIGWA
MENEJA WA MKOA
SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA

JE,NI KWELI WAZANZIBAR KUTOKA CHAMA TAWALA WANAUFYATA WAKIFIKA DOM MJENGONI?


Wajumbe wa Bunge la Katiba wakiwa bungeni mjini Dodoma jana.Picha na Emmanuel Herman

Mhariri Mkuu MOblog Tanzania
Bunge la Katiba linaloendelea mjini Dodoma ni vituko, vioja, uchafuzi, lugha za matusi, mipasho kama ‘kitchen party’ au uwanja wa fisi pale kwenye bar ya rafiki yangu wa kitambo mwandishi mwezangu Baraka Karashani.

Kwani wajumbe wa Bunge la Katiba hawana aibu, woga au ndiyo kusema mshipa wa aibu umeingia mafuta ya taa waheshimiwa nyie kulikoni jamani mbona taabu wananchi hawaelewi nini kinaendelea maana ni serikali tatu au mbili kama msahafu vile ahhaaaaa jamani.

Kwa sababu watu wazima kurushiana matusi kama vile mpo kwenye gurio la nguo au mnandani au sewa kwa madada zetu pale Buguruni haileti picha kwa wananchi wanaotizama Bunge hilo nchi nzima halafu mnachukua 300,000 kwa siku kibindoni kwenye nyama choma chako chako maana yake nini?

Kwa mantiki hiyo basi jana nilitamani kwa udi na uvumba kutizama angalau kwa masaa kadhaa majadiliano ya Bunge la Katiba linaloendelea mjini Dodoma kwa kutambua umuhimu wake kwa vizazi vya sasa na vijavyo kwa hiyo niliamua kwa makusudi kabisa kutizama wajumbe wa Bunge hilo maalum wakirubana kwa hoja na si kwa vioja.

Lakini Mjumbe pekee aliyenikuna jana ni Mhe Mbarouk Salum Ally kutoka visiwani aliyesema kwamba wajumbe kutoka Zanzibar wamekuwa kama “Mbayuwayu’ vigeugeu kwa sababu wakiwa visiwani wanataka serikali tatu kwamba muungano unawabana wakija Dodoma wanalowa maji wapole kama maji ya mtungi hivi ni kweli?

Eti ni kwanini wazanzibari wanalalamika kuhusu kero za muungano kila kukicha mara hili mara lile lakini wakipata fursa wanaufyata kama alivyosema Jussa juzi au si kweli jamani nini kinatokea mpaka wakifika Dodoma hoja zao zinakuwa kapuni kabisa!

Mjumbe huyo wa Bunge la katiba amesema kwamba wazanzibar wengi ndani ya Bunge na hasa wa kutoka chama tawala wanalalamika chini kwa chini na wakiwa visiwani wanasema sasa tunataka serikali tatu yaani serikali ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Shirikisho lakini wakifika kwenye vikao vya chama chao wanaloa kabisa hawathubutu kabisa kusema chochote!

Lakini hebu tujikumbushe kidogo wazanzibari kulalamika kwamba serikali ya bara inawabana au Tanganyika kujificha ndani ya Muungano haikuanza leo yaani piga ua huo ndio ukweli malalamiko ya watu wa visiwani kuhusu muundo wa muungano yalianza tangu mzee karume watu wanasema na baadaye Aboud Jumbe ambaye alitiwa ndani kabisa kwa kile wanachosema watu kuchafuka kwa hali ya hewa 1984.

Kwa hiyo swala la muundo na kero za muungano lipo kitambo Zanzibar inataka mamlaka yake kamili na ndiyo maana hivi karibuni 2010 waliandika katiba yao na kutamka bayana kwamba Zanzibar ni nchi ndiyo ambayo kimsingi inasigana na katiba ya Muungano nani anabisha?

Sasa kinachofanya wasiseme ukweli kwamba jamani serikali tatu ndio suluhisho la kudumu la kero za muungano ni kipi? Basi kuanzia sasa kama hawawezi na tumpe rungu Jakaya kikwete ya kuwalazimisha kubadili katiba yao na Zanzibar si nchi tena mbali ni sehemu ya Muungano ndiyo kwa hapo nami namuunga mkono Rais Jakaya Kikwete kwa hilo.

Hata kama rasimu ya katiba ya Jaji warioba inasema serikali tatu ndio maoni ya wananchi lakini kwa sababu wenyewe Zanzibar wameridhika na muundo wa sasa hakuna shida kazi ni moja kwa chama tawala kuhakikisha Rais wa SMZ Ali Mohammed Shein anabadilisha vipengele kadhaa kwenye katiba yao ya 2010 ili twende sawa ndiyo.

Watasema sana lakini huo ndiyo ukweli waache malumbano yasiyokwisha huko mjengoni kama vilabu vya pombe ya kibuku na mnazi kama uwanja wa fisi!
Naomba kuwasilisha 

Kutoka MO Blog

LASWA YAPELEKA NEEMA YA MSAADA WA KISHERIA KILOLO NA IRINGA


Watoa huduma ya kisheria kutoka  wilaya ya Kilolo   wakiwa katika  picha ya pamoja na mgeni rasmi ,wakufunzi na uongozi  wa LASWA
Mgeni rasmi mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo Bw. Abdul Manga akimkabidhi  mhitimu wa mafunzo hayo Pendo Elia kutoa  wilaya ya Iringa vitendea kazi na cheti kulia ni katibu mtendaji wa asasi isiyo  ya kiserikali ya  Legal Aid and Social welfare association( LASWA)  mkoani Iringa Oscary Waya

Na  Francis Godwin Blog  WANANCHI waliokuwa  wakipoteza  haki zao kwa  kukosa msaada wa kisheria katika wilaya ya Iringa na Kilolo mkoani Iringa watafutiwa ufumbuzi  wa  kudumu wa kisheria kwa kusogezewa wataalam  watakao wapa msaada  wa  kisheria  bila malipo 
Akizungumza jana mjini Ilula  wilaya ya Kilolo  wakati  wa kuhitimisha mafunzo ya  kisheria kwa  wahitimu hao katibu mtendaji wa  asasi isiyo  ya kiserikali ya  Legal Aid and Social welfare association( LASWA)  mkoani Iringa Oscary Waya  alisema kuwa jumla ya vijana zaidi ya 50  wamepewa mafunzo ya kisheria  ili  kuisaidia jamii ambayo imekuwa ikipoteza haki kwa  kukosa msaada  wa  kisheria.
 
Alisema kuwa asasi yake imeamua kutoa mafunzo ya kisheria kwa vijana  hao ambao kutoka  kata za wilaya za Kilolo na Iringa Vijijini ili  kuisaidia jamii ya maeneo hayo kupata huduma ya bure ya msaada wa  kisheria wa  bure .
 
Bw  Waya alisema kuwa kutokana na uvunjifu wa amani na kushindwa kutimizwa kwa sheria kwa wananchi wa vijijini, LASWA waliamua kuwaandaa vijana  hao na  kuwapa mafunzo  ambayo yataendelea kuwa msaada kwa wananchi na kuepuka kupoteza  muda kwa kukimbilia mahakamani ama katika mabaraza ya kata.
 
Alisema kuwa wahitimu wa mafunzo ambayo yamefanyika kwa miaka mitatu kwa nyakati tofauti yamewezesha watu 27 kutoka wilaya ya Kilolo na wengine 24 kutoka wilaya ya Iringa Vijijini kuhitimu ambapo kwa miaka mitatu jumla ya milioni 179,990,000 zimetumika katika kutoa mafunzo ili vijana hao ili kuisaidia jamii kuondokana na kero mbalimbali zinazowakandamiza kwa  kutojua sheria .
 
Baadhi ya wahitimu wakizungumzia mafunzo hayo Bw. Ramadhan Mhehe, Bi. Rukia Kihwele, Bw. Mkude Mng’ong’o na Lucas Kidungu walisema kuwa kero ambazo wamekuwa wakikumbana nazo katika maeneo ya vijiji, kata na tarafa ambazo wananchi wanakabiliana nazo ni pamoja na kero za migogoro ya ardhi, ndoa, mirathi, unyanyaswaji wa kijinsia kwa wanawake na wanaume ambapo kero nyingi chanzo chake zinatokana na mfumo dume uliopo katika jamii ya watu wanamoishi.

Hata  hivyo  alisema  kuwa  kwa kuwa  vijana hao  wataendelea  kutoa huduma ya  bure ambayo itawasaidia  wananchi kutoa msaada  wa kisheria  ni vema serikali ama   wahisani kujitokeza ili  kuwasaidia vijana hao ambao  wataendelea  kufanya kazi hiyo kwa  kujitolea  bila malipo  tofauti na mabaraza ya kata .
Bw  waya  alisema kwa  sasa  vijana hao mbali ya kuifanya kazi hiyo ya  huduma ya kisheria bado wameanzishiwa asasi zao  mbili moja ikiwepo Ilula na nyingine Mseke na  kwa  sasa  wana miradi ya kiuchumi ukiwemo  wa upandaji miti.
 
 Kwa  upande  wake mgeni  rasmi  katika ufungaji wa mafunzo hayo ,mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo Bw. Abdul Manga aliwataka wahitimu hao  kwenda kutoa msaada wa kisherika katika kila kata katika wilaya za Kilolo na Iringa Vijijini kwa  uhakika  bila kuwatoza  pesa  wananchi kama ilivyo mabaraza ya kata ambayo yamekuwa  yakilazimisha kesi  ili kupata pesa .
 
Manga alisema kuwa mabaraza ya kata yanayoshughulikia kuamua kesi na kero mbalimbali za wananchi kutokana na kuhitaji malipo ya fedha ili waweze kufanya maamuzi ya kusimamia sheria katika maeneo yao yamesababisha watu wengi kujiweka kando na mabaraza hayo na badala yake wamekuwa wakiendelea kuteseka kutokana na kushindwa kupatiwa haki kwa kukosa pesa.
 
“Malengo ya LASWA ya kutoa mafunzo kwa ninyi watu 51 ili kila kata za Iringa Vijijini na Kilolo watu wapate msaada wa kisheria ni makubwa na yamezingatia ubinadamu na hali nzima ya utu kwa watu wote kwa kuwa juhudi zao za kutoa mafunzo unalenga kuitatulia kero mbalimbali za kijamii wananchi wote wa vijijini, hivyo mtatakiwa mkawajibike kikamilifu kwa jamii na kuwashauri wananchi kutopenda kesi kwa jambo ambalo  linawezekana kupatiwa  ufumbuzi ”, 
Lakini pia ninaiomba serikali ili sisi wanasheria tuweze kutoa mafunzo na elimu kwa mabaraza yetu yote ya kata ambayo yanasimamia haki na sheria kwa wananchi wetu ili kila wakati sheria ambazo zinatakiwa kuamuliwa zitende haki kwa wananchi mara kwa mara ndani ya jamii endapo mabaraza ya kata yatapatiwa elimu mbadala yataweza kutenda haki sahihi kwa wananchi wetu.
 
Alisema kuwa uwepo wa gharama kubwa za kufuatilia kesi katika maeneo ya vijijini pamoja na kuwasafirisha mashahidi na kuupata ukweli kwa walalamikaji ambao umekuwa ukitendewa ndivy sivyo ambapo alisema kuwa itakuwa ni faraja kubwa endapo mafunzo hayo yataleta faida kubwa kwa wananchi ambao wanatakiwa wakombolewe kupitia watu waliojifunza mafunzo ya sheria.

KIKAO CHA 25 CHA BODI YA TAIFA YA PAROLE CHAMALIZIKA LEO JIJINI ARUSHA

image (2)

MAMA KIKWETE AWATAKA WAKAZI WA KATA YA MSINJAHILI KUTOOGOPA KUVUTA UMEME MAJUMBANI MWAO

IMG_3981
Na Anna Nkinda- Maelezo, Lindi
Wakazi wa kata ya Msinjahili wilayani Lindi wametakiwa kutoogopa kuvuta umeme majumbani mwao kwa kuhofu kuwa wakifanya hivyo wataonekana ni matajiri kwani matumizi ya umeme ni ya gharama naafuu ukilinganisha na  mafuta ya taa.

Mwito huo umetolea jana na  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Taifa (NEC) wilaya ya Lindi mjini wakati akiongea  kwa nyakati tofauti  na viongozi wa Halmashauri kuu ya tawi ya Chama hicho  katika matawi ya  Muungano, Jitegemee, Sinde na Mnali yaliyopo katika kata ya Msinjahili wilaya ya Lindi mjini.

Mama Kikwete ambaye pia ni Mke wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete alisema ili kuboresha  maisha ya wananchi Serikali imejitahidi kupitisha  umeme wa gesi katika  vijiji vilivyopo katika kata hiyo na kupunguza gharama ya uvutaji ambazo ni nafuu  jambo la muhimu ni kwa wananchi kuutumia.

“Kuwa na umeme nyumbani kwako na kuutumia ni mwanzo wa maendeleo,  hata watoto wako wataweza kuutumia mwanga huo kwa kujisomea hasa nyakati za usiku  na hivyo kufanya vizuri katika mitihani yao”, alisema Mama Kikwete.

Aidha Mjumbe huyo wa NEC  pia aliwataka  viongozi hao  wa Halmashauri kuu ya tawi kuwahimiza watu wanaowaongoza katika maeneo yao kutumia mvua zinazoendelea kunyesha kulima chakula cha kutosha jambo ambalo litawafanya kuwa na chakula cha ziada na hivyo kuepukana na kitendo cha  kuomba chakula kwa majirani.

Akizungumzia kuhusu suala la uongozi Mama Kikwete aliwahimiza  wanawake kutoogopa kuomba na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi  katika chaguzi zijazo ili waweze  kupata nafasi ya kuongoza na hivyo kufika katika ngazi ya maamuzi.

Mama Kikwete alisisitiza , “Sisi wanawake tunakabiliwa na changamoto nyingi  na mtu pekee anayeweza kuziongelea changamoto zetu kiusahihi ni mwanamke mwenyewe hivyo basi msiogope kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wakati wa uchaguzi ukifika mkifanya hivyo kutakuwa na viongozi wengi wanawake ambao wataweza kuwakilisha matatizo na mawazo yetu katika ngazi za juu za uongozi wa chama na Serikali”.  
MNEC huyo alimalizia kwa kuwahimiza viongozi hao wa Halmashauri kuu ya tawi ya CCM kuishi maisha ya  upendo, mshikamano na amani kwani jamii ikiishi maisha hayo itaweza kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo kwa kushirikiana.

Kwa upande wake  katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Lindi Haji Tajiri aliwataka viongozi hao kuwa  waaminifu katika ndoa zao  na kuepuka tabia ya kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja (michepuko) kwa kufanya hivyo  wataepukana na ugonjwa wa Ukimwi.

“Chama Cha Mapinduzi  kinahitaji kuwa na watu wenye afya njema ili waweze kufanya vizuri kazi za chama nawaomba muwe waaminifu kwa wapenzi wenu mkifanya hivyo mtaepekana na Ugonjwa wa Ukimwi”, alisema Tajiri.

Katibu huyo wa Jumuia ya Wazazi mkoa pia aliwaomba  kinamama  kuiga  mfano wa Mama Salma Kikwete ambaye anafanya kazi kubwa ya kujitoa katika shughuli mbalimbali za kijamii na kutetea haki zao, wasichana  na watoto na kuongeza  kwamba   anastahili pongezi kwani  yeye ni mama na mlezi wa taifa.  
Mjumbe huyo wa NEC taifa akiwa katika kata ya Msinjahili alifungua mashina ya wakereketwa wa CCM Jumuia ya wazazi  katika tawi namba  tatu  la Sinde na namba mbili  la Mnali.

Mama Kikwete ambaye ni mjumbe wa NEC Taifa kupitia wilaya ya Lindi mjini alikutana na viongozi hao wa Halmashauri kuu ya tawi ya CCM kwa ajili ya kuimarisha kazi za chama hicho ikiwa ni pamoja na kufanya vikao na viongozi.

ZITTO:KITAKACHOVUNJA MUUNGANO SI SERIKALI TATU


zittopx_3684f.jpg
Dodoma. 
Mjumbe wa Bunge la Katiba, Zitto Kabwe amesema kuandikwa kwa Katiba isiyokubaliwa na pande zote kutasababisha gharama kubwa kuliko zile zinazotajwa za serikali tatu.

Akichangia hoja kwenye Bunge hilo jana, Zitto alisema kuna kila sababu ya kukaa na kukubaliana ili kupata Katiba itakayokubalika pande zote.

"Muundo wa Muungano una hatari ya kuvunjika iwapo hakuna matakwa ya dhati ya watu kuungana... Maneno ya kusema Serikali tatu zitavunja Muungano ni ya siasa na hayana msingi wa kisayansi. Urusi ilivunjika sababu haikuwa na demokrasia na siyo sababu ya idadi ya Serikali," alisema.

Zitto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), alisema hofu ya gharama inayotajwa katika uendeshaji wa muundo wa serikali tatu haina msingi wowote kwa kuwa hakuna ushahidi wa kitaalamu unaothibitisha gharama hizo
.
"Nimesikia watu wanasema eti tutalazimika kujenga ikulu mpya, nani kasema lazima tuwe na marais watatu? Tunaweza kuwa na rais mmoja kwenye nchi na wakuu wa nchi washirika wawili... Ni jambo la makubaliano tu," alisema.

Alisema bajeti ya mwaka huu ni Sh18 trilioni, kati ya hizo Sh5.3 trilioni ndizo zinazohudumia wizara za Muungano, lakini serikali ina uwezo wa kukusanya kodi zaidi ya Sh10 trilioni pamoja na mapato mengine.

"Kuna jumla ya Sh2.3 trilioni hatuzikusanyi kila mwaka kutoka kwenye kampuni kubwa, kwa uwezo wetu wa pato la ndani asilimia 17 tunao uwezo wa kuendesha serikali ya muundo wa idadi yoyote.

"Hofu ya Serikali ya Muungano kutokuwa na fedha ni sababu halisi, ni kweli kwamba ushuru wa bidhaa pekee yake hauwezi kutuendeshea serikali. Sasa nini kazi yetu, tunaingia hapa ili kuboresha hayo maeneo, kama hatuwezi tumekuja kufanya nini hapa?" alihoji.

Jussa akomaa
Mjumbe wa Bunge hilo, Ismail Jussa jana alisisitiza kwamba Wazanzibari wengi hawapo tayari kuendelea na mfumo wa serikali mbili kwa sababu unawatesa na kuwadhalilisha.

Jussa ambaye ni mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kupitia CUF, alisema haoni haya kuzungumzia suala hilo kwa niaba ya Wazanzibari.

"Hoja nyingi zimetoka (kuhusu Muungano), lakini naendelea kuzungumza kwa niaba ya wananchi wa Zanzibar na katika hili sioni haya kwa sababu naamini kwamba wanakisimamia kile ambacho sisi tunasimamia nacho ni Zanzibar yenye mamlaka kamili," alisema Jussa.

Alisema amekuwa akijiuliza kwa nini serikali mbili zinang'ang'aniwa na CCM licha ya kunung'unikiwa na baadhi ya wanachama wake kwa miaka 50?

"Hapa wala maneno hayo hayajasemwa na CUF, wala na mpinzani. Hapa ninayo Ripoti ya Amina Salum Ali ya Novemba 1992 ikiorodhesha matatizo lukuki ya mfumo wa serikali mbili na wajumbe wake hawa wote walikuwa ni kutoka CCM, mwenyekiti wake Amina Salum Ali, katibu wake Ali Juma Shamhuna ndiyo walioleta ripoti hii," alisema Jussa huku akionyesha ripoti hiyo.
 
Kutokana na hali hiyo, alisema anaona ni kuwadanganya Wazanzibari kwamba serikali mbili zitatatua matatizo yao, hivyo kuwafanya wajiulize mbona hazikuyatatua kwa miaka 50 iliyopita.

HATIMAYE WASHINDI WATATU WA SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS KANDA YA KATI WAPATIKANA


Na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Dodoma

Hii ni baada ya washindi watatu kutoka Kanda ya Kati kupatikana katika shindano la kusaka vipaji vya kuigiza lililoendeshwa na Kampuni ya Proin Promotion Limited (PPL). Fainali ya kuvisaka vipaji kwa kanda ya Kati  ilifanyika jana Mnamo tarehe 15 April 2014 Mkoani Dodoma na washindi kutangazwa na Jaji Mkuu wa shindano hilo, Roy Sarungi aliyesaidiwa na Yvonne Chery ‘Monalisa’ na Single Mtambalike ‘Richie Richie.’

Roy kwa kusaidiana na Yvonne Chery ‘Monalisa’ na Single Mtambalike ‘Richie Richie.’ aliwatangaza Joyce Rebeca, Moses Obunde na Mwinshehe Mohamed kuwa washindi wa shindano la kusaka vipaji vya kuigiza Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents ambapo kila mmoja alipewa zawadi nono ya Sh 500,000. Shindano hilo liliwashirikisha washiriki 500, lakini ni washiriki watano wenye vipaji waliofanikiwa kuingia tano bora na baadaye majaji walifanya kazi kubwa ya kuwachagua na kuwatangaza washindi watatu.

Mshiriki mkubwa kuliko wote , Idrisa Ally  (40), alionesha kipaji cha hali ya juu cha kuigiza na alizawadiwa na majaji Sh 100,000. Idrisa hatakwenda kushiriki fainali za mashindano hayo zinazotarajiwa kufanyika Agosti mwaka huu jijini Dar es Salaam kutokana na umri wake kuwa mkubwa kuliko kigezo cha umri kilichowekwa cha kuanzia miaka 14 hadi 35, ingawa majaji waliahidi kuwasiliana naye kwa lengo la kuendeleza kipaji chake umri wake utakaporuhusu.

“Tumebaini kuwa Kanda ya Kati hususani Mkoa wa Dodoma kuna vipaji vingi vya sanaa ya uigizaji na katika hili Idrisa Ally ametuthibitishia yeye ni mzee mwenye kipaji, lakini amedhihirisha kuwa ana kipaji cha kuigiza,” anasema Jaji Mkuu wa shindano hilo, Sarungi anasema sanaa ya uigizaji ni muhimu kwa vijana, kwa vile sasa hutoa fursa ya ajira ambapo imewawezesha vijana wengi nchini kujiajiri wenyewe na kuimarika kiuchumi.

“Ni matumaini yangu kuwa kwa washindi hawa wa Kanda ya kati hawataishia hapa watajiendeleza zaidi kwani uigizaji sasa ni ajira,” anasema. Mshiriki Moses Obunde  alishindwa kuzuia furaha yake baada ya kutangazwa mshindi, aliangua kilio kuashiria furaha aliyokuwa nayo na kuufanya ukumbi mzima kutaharuki.
Ofisa Uhusiano wa Proin Promotion Limited (PPL), Josephat Lukaza, ambao ndio waratibu na waandaaji wa shindano hilo la kusaka vipaji vya uigizaji, anasema mashindano hayo yanaendeshwa kikanda, ambapo kwa kuanzia walianza kusaka vipaji kwa Kanda ya Ziwa na Kumalizika Jana katika Kanda ya kati Mkoa wa Dodoma na hatimaye zoezi hili kuamia Kanda ya Juu Kusini ambapo usaili utafanyika Mkoani Mbeya kuanzia tarehe 19 April.

“Baadaye tutaelekea Kanda ya Njanda za Juu Kusini lakini tunashukuru kwa ushirikiano tulioupata kwa wakazi wa Kanda ya Kati, tumepata washiriki 600, ambao tuliwachuja hadi kuwapata washindi watatu waliokidhi vigezo tulivyovihitaji,” anasema Lukaza. Baadhi ya vigezo kwa mujibu wa Lukaza, vilikuwa ni mshiriki kuwa na umri kuanzia miaka 14 hadi 35, anayejiamini, mbunifu, anayemiliki jukwaa na igizo lake libebe ujumbe wa kuelimisha.

Anasema lengo la PPL kuzungukia kanda hizo sita nchini ni kuhakikisha kuwa inavisaka vipaji vya vijana kupitia sanaa ya maigizo, ambavyo vimejificha ili viendelezwe na kampuni yake. “Tumeamua kuwekeza katika sanaa maana sanaa ni fursa kama zilivyo fursa zingine nchini na ni matumaini yetu kuwa jamii itatuunga mkono katika safari ndefu tuliyo nayo ya kuvisaka na kuviendeleza vipaji,” anaeleza ofisa huyo uhusiano.
Anasema PPL inaendesha shindano hilo kwa kanda sita nchini ambazo ni Kanda ya Ziwa, Magharibi, Pwani, Kati, Kaskazini na Kusini.

“Kwa sasa tumeanza na mikoa sita, lakini matarajio yetu ya baadaye ni kuifikia mikoa yote nchini ambapo tunaamini kuna vipaji vingi vya wasanii vimejificha ili waweze kupata ajira kupitia vipaji vyao,” anasema na kuongeza kuwa mshindi wa jumla baada ya mashindano ya kikanda kumalizika atapatikana Agosti mwaka huu jijini Dar es Salaam, ambako ataondoka na zawadi nono ya Sh milioni 50.

Anasema usakaji vipaji hivyo huendeshwa kwa umakini na umahiri mkubwa kupitia kwa majaji na watu wenye utalaamu wa tasnia ya filamu na teknolojia ya habari (IT) walio chini ya kampuni yake, ambao pia huzingatia miiko na maadili ya kazi hiyo kwa kila mshiriki. Anasema PPL imesajiliwa rasmi mwaka 2013 kupitia Sheria ya Usajili wa Makampuni ambayo hushughulika na ukuzaji wa sanaa ya filamu nchini.

“Pia tunashughulika na usimamizi wa uzalishaji wa filamu nchini, uzalishaji na usambazaji wa DVD na filamu zilizokamilika kuingia sokoni na matarajio yetu ya baadaye ni kuwa kampuni bora katika Bara la Afrika,” anaeleza. Wakizungumza na gazeti hili, washindi waliobuka kidedea waliwashukuru waandaaji wa shindano hilo kwa kuibua vipaji vyao ambavyo wanasema visingeweza kutambulika.

Crecensiah anasema anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumwibua katika shindano hilo na kumwezesha kuwa mshindi, ambapo sasa anaamini kuwa ndoto yake ya kuwa msanii wa kimataifa imetimia. “Namshukuru Mungu kwa yote, lakini zaidi niwashukuru waandaaji wa shindano hili kwa kutumia muda wao na fedha kuvisaka vipaji, binafsi naona kiu yangu ya kuwa muigizaji wa kimataifa imetimia, nitaongeza juhudi kubwa katika tasnia ya filamu,” anasema msanii huyo. Naye Janeth anasema penye nia pana njia, kwa madai kuwa alikuwa na kiu ya kuwa msanii wa kuigiza kwa muda mrefu hasa baada ya kuwaona wasanii mbalimbali kupitia luninga nchini.

“Kwa kweli naweza kusema nimepata maji ya kunywa dhidi ya kiu yangu ya kuwa msanii, ni kazi ambayo nilikuwa naipenda tangu nikiwa mtoto namshukuru sana Mungu na waandaaji wa shindano hili la kusaka vipaji vya kuigiza,” anaeleza mshindi huyo. Kwa upande wake, Joshua Wambura anasema ushindi wake ni mwanzo wa safari yake ndefu katika kuingia katika tasnia ya filamu ndani na nje ya nchi.

Tuesday, April 15, 2014

JOTI MSANII AMBAYE ANAZIDI KUPATA UMAARUFU NCHINI NA NJE YA NCHI BILA KUWA NA MAJIGAMBO

Msanii wa vichekesho nchini maarufu JOTI anazidi kuendelea kujipatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi huku idadi ya watu wanaomkubali ikizidi pia kuongezeka....JOTI ambaye anaonesha kujali watu wanaomkubali katika tasnia hiyo ya uchekeshaji na amekuwa hana unyanyapaa kwa watu wote jambo ambalo linazidi kumpa nafasi kwa mashabiki wake na kuonekana kuwa ni msanii ambaye kwa hali ya kawaida bado ataendelea kuwa nyota mbele ya watu...Nimemsikia na kumuona mara kadhaa msanii huyu nguli ambaye karibu kila kona amekuwa mtu wa watu na pia hasikiki kuwa na mtazamo wa kujitengenezea  umaarufu  kupitia mfumo wa kuandaa  kashfa za ajabu ajabu kwenye magazeti  kama walivyo wasanii wengine nchini ambao hujipandisha chati kwa mfumo huo...JOTI nimekutananae tena hapa Dodoma akiwa anazungumza na baadhi ya watu ambao walikuwa na hamu kubwa ya kumsikiliza.

SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS LAPOKELEWA VYEMA NA WATANZANIA MIKOA YA MWANZA NA DODOMA

  
Na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Dodoma

Watanzania wa Mikoa ya Mwanza na Dodoma wameipongeza kampuni ya Proin Promotions Limited kupitia shindano lao la Kusaka vipaji vya Kuigiza Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents kwa kuamua kuanzisha shindano hilo ambalo limeanza kuonyesha matumaini kwa vijana wenye vipaji vya kuigiza ambao walisahaulika katika tasnia hiyo ya filamu nchini.

Shindano hili la Tanzania Movie Talents linawawezesha watanzania wote wenye vipaji vya kuigiza kuweza kujitokeza ili kuweza kuonyesha vipaji vyao na kuvikuza kwa kutumia fursa hii iliyoanzishwa na kampuni ya Proin Promotions Limited


Wakiongelea kuhusu shindano hili la Tanzania Movie Talents, wakazi wa Mkoa wa Dodoma walisema" tunafurahishwa sana na shindano hili kuweza kuanzishwa Tanzania na Afrika Mashariki na Kati kwani sasa tunaweza kupata nafasi katika tasnia ya filamu baada ya kuanza kuonyesha vipaji vyetu vya kuigiza"

"Tanzania Movie Talents inamgusa kila mtanzania mwenye vipaji vya kuigiza kwani ni nafasi kwa vijana na watanzania wote wenye vipaji vya kuigiza kuweza kujitokeza kwaajili ya kuonyesha uwezo na vipaji vyao vya kuigiza, Shindano la Tanzania Movie Talents ni mkombozi wa Vijana na watanzania ambao wana vipaji vya kuigiza ambapo kupitia shindano hili vijana wanaweza kupata nafasi za ajira kupitia tasnia ya filamu nchini ambapo washiriki watakuwa wameweza kuonekana na hatimaye kuitwa kwaajili ya kufanya kazi.


Kwa upande wake baadhi ya wafanyakazi wa timu ya Tanzania Movie Talents walithibitisha kuwa 'Tanzania Movie Talents imepokelewa vizuri na watanzania wa Mikoa ya Mwanza na Dodoma  kwani tumeona ongezeko la washiriki waliojitokeza kwaajili ya usaili wa kushiriki katika Shindano hili kubwa na la kwanza Afrika Mashariki na Kati.

 Hii nikutokana na ukweli kwamba washiriki wote wanaofika kwaajili ya Usaili hawatozwi kiasi chochote cha pesa kutoka timu ya Tanzania Movie Talents na pia kufurahishwa na uamuzi wa Majaji wa Timu ya Tanzania Movie Talents,  niwazi kabisa kuwa kutotozwa kwa kiasi chochote cha pesa kwa washiriki kumekuwa ni kivutio kikubwa kabisa hivyo kuongeza idadi ya washiriki katika kila Kanda tunayoenda"alisema Stephen Mapunda Mkazi wa Mkoa wa Dodoma

POLISI WAPEWA ELIMU YA UKATILI WA KIJINSIA KIGOMA

Na Magreth Magosso Kigoma.

POLISI  Mkoa wa Kigoma wametakiwa wawe makini katika upokeaji wa elimu sahihi ya ukatili wa kijinsia kwa lengo la kudhibiti na kutatua changamoto hiyo kwa wananchi ambayo inachagia kuzorotesha  uchumi wa  jamii zetu.

Akifafanua hilo kwenye uzinduzi wa mafunzo ya siku Nne kwa wakaguzi wa madawati ya jinsia na maofisa polisi wa Kigoma na Tabora wakilenga kuwapa elimu  ya utambuzi juu ya ukatili wa kijinsia  kuwa ni  kosa la jinai kwa tija ya kupunguza vitendo hivyo na kulinda utu wa wahanga.

Pia Naibu Kamishna mkuu wa Polisi Dawati la jinsia na watoto Taifa Adolphina Chialo alisema, miongoni mwao hushindwa kuwasaidia wahanga waliofanyiwa vitendo  vya ukatili kutokana na mfumo dume ulioathiri jamii kuona wanaume kupiga wake zao ni sehemu ya upendo na mwanamke akichukua hatua anatengwa na familia hali inayozidisha unyonge kwa wanawake .

“badilikeni, ukatili unaathiri mfumo wa maisha ya wahanga kisaikolojia na kimwili,sasa mafunzo haya chachu kwenu kuwajibika,hatuna bajeti ya madawati toka serikalini lakini tuonyeshe nia yetu kwa pamoja tutengewe fungu la kuendesha  na semina kwa wadau na umma” alisema Chialo.

Akifungua mafunzo hayo mgeni rasmi ambaye pia ni Ofisa ustawi jamii Manispaa ya Kigoma Ujiji Agnes Punjila alishauri askari polisi waongeze udadisi kwa kufuatilia vyombo vya habari na matukio kadhaa katika mikoa mingine na nje ya nchi ili kujiimarisha katika kukabiliana na sheria tata za kuwashtaki watendaji wa matukio husika.

Kwa upande wa Mkaguzi mkuu wa dawati la jinsia kigoma Amina Kihando alisema changamoto ya  kutofanikisha kukamata wahalifu wasifikishwe kwenye vyombo vya sheria inatokana  na wahanga kutiwa hofu na jamii kwa mujibu wa mila,tamaduni na imani za kidini pasipo kubaini athari zake pia ni chachu kwa familia kuwa sehemu ya ukatili kutokana na kumaliza kesi kinyemela.

Alisema watu wa ukanda wa ziwa ni miongoni mwa wahanga wa matukio hayo,lakini wanashindwa kuwapeleka wahusika mahakamani kutokana na changamoto ya usafiri na kipato cha kugharamia kesi husika,Huku akiri matukio ya ubakaji ni mengi pamoja na walezi wa familia huyafumbia macho kwa hofu ya kujenga uhasama baina ya mtenda na mtendewa.

Naye Kamanda wa Polisi Fresser Kashai  na wakili wa Halmashauri ya wilaya ya kigoma Idd Ndabhona kwa nyakati tofauti walisema mafunzo hayo ni tija kwa jamii husika kutokana na kushamiri vitendo vya kutelekeza watoto,ubakaji na lugha chafu  ambapo jamii huona ni kawaida ilihali  kisheria ni kosa la jinai,mtendewa ana haki za msingi kushtaki.
 

Mtandao huu umebaini kuwa  ,kitaifa madawati  ya kijinsia yapo 417 ambapo madawati 8 yana ofisi zake,sanjari na watendaji wake hawana upeo mpana wa sheria na namna ya kukabiliana na kesi za aina hizo hali inayochangia ukatili kusimika mizizi katika familia na viongozi kwa ujumla hasa kwa kutojitambua,kuthamini, kujali na kuwajibika.

Hivyo kuchangia  kizazi kisichojali ambapo Aprili,2014 dawati hilo mkoa limepokea kesi 20  kutoka wilaya sita za mkoani haopa,huku kesi 6 zipo mahakamani ni moja ya kiashiria cha elimu finyu kwa umma, kukosekana kwa sheria maalum juu ya ukatili ili  kusaidia wahanga  kesi zimalizwe mapema kwa mujibu wa sheria husika  tija kuboresha maisha ya umma kwa kuzingatia usawa na haki.