WAJUMBE wa Bunge maalum
la Katiba waliokacha kikao hivi karibuni wametakiwa
warudishe posho za kikao kutokana na kitendo chao cha kushindwa kuwa na
demokrasia kwa kuvumilia changamoto mbalimbali zinazotokea katika mijadala
muhimu ya kujadili rasimu ya katiba ya watanzania.
Hayo yamebainika kufuatia maoni ya baadhi ya wananchi wa manispaa ya kigoma ujiji wakati wakizuya
wabunge kuvikao vya bunge hilo vinavyoendelea mjini Dododma kwa madai ya
kubaguliwa, kutukanwa na kudhalilishwa na wabunge wa chama tawala, CCM.
Katibu wa Chama cha NRA Taifa Fadhili Kiswaga alisema
mijadala inayoendelea katika bunge hilo linawachosha watanzania kusikia viloja
visivyo na mashiko kwa umma badala yake wawakilishi walio wengi wapo kwa
ushabiki wa kichama badala ya kujenga taifa
kwa kuzingatia hoja zenye mashiko na maslai ya wananchi.
“kitendo cha kutoka nje hakina maana kwetu,basi warudishe na
posho kama wanashindwa kupigania hoja mezani na si kususa mimi naona waliotoka nje si wazalendo
,mzalendo hachoki kutetea haki za msingi ikiwa ana hoja zenye mashiko”
alibainisha Kiswaga.
Mwalimu Alphonce Mbasa alisema baadhi ya wabunge wapo katika kubaguana hali ambayo ni mbaya
kwa umma pamoja na itikadi ya kichama,badala ya kujadili kilicholetwa na tume
ya rais iliyongozwa na Jaji Sinde Warioba kwa maana ya kuboresha kilichopo na si kulazimisha mambo
yasiyo katika waraka huo.
Akinukuu sheria ya rasimu hiyo namba 83 kipengele cha
23,24,25,26 na waraka husika unabainisha watajadili kile kilichoko kwenye
rasimu ,pia suala la muungano ni makubaliano baina ya watanganyika na watu wa
Zanzibari huku akidai kitendo cha kutoka nje kwa baadhi ya wabunge ni moja ya
kuonyesha kile kilichopo ni batili .
Antony Kayanda alisema kitendo cha wabunge kutoa hoja za
ukabila ni chachu ya kuwagawa wananchi wanaofuatilia mijadala hiyo hali
inayokwaza walengwa wa katiba hiyo hasa wakulima na wanyonge waliosahulika na
serikali kutokana kukosa elimu ya uraia kubaini uhalisia wa mambo kulingana
na matamshi ya baadhi ya wabunge wenye hulka ya kuweka utabaka wa ukabila na
udini.
Naye Mratibu wa Asasi ya Ndela Youth Development ya hapa
Adolfu Leopard aliwashauri wabunge hao wasihofu mikinzano ya hoja,badala yake
waongeze uzalendo kwa kufafanua hoja zao na wachie wananchi wafanye maamuzi
kwenye kupiga kura juu ya walichoboresha na si kususia vikao.
No comments:
Post a Comment