Mshiriki
wa Tanzania Movie Talents akihojiwa mara baada ya kumaliza usaili
katika Shindano la Tanzania Movie Talents linaloendelea muda huu katika
Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo Soko Matola Mkoani Mbeya
Baadhi
ya washiriki waliojitokeza kwaajili ya kuhudhuria usaili wa Shindano la
Tanzania Movie Talents wakijadiliana jambo kabla ya kuanza kwa usaili.
Washiriki
waliojitokeza kwaajili ya kushiriki mashindano yya Tanzania Movie
Talents wakijaza fomu kwaajili ya usaili wa shindano la Tanzania Movie
Talents linaloendelea Mkoani Mbeya ikiwa unawakilisha Kanda ya Nyanda za
Juu Kusini
Baadhi ya washiriki kutoka Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mkoani Mbeya wakisubiri shindano la Tanzania Movie Talents kuanza.
Kundi
la Kwanza La vijana waliojitokeza kwaajili ya usaili wa Shindano la
Tanzania Movie Talents linaloendelea mkoani Mbeya muda huu.Picha na
Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Mbeya
Hatimaye
Shindano la Tanzania Movie Talents limeanza rasmi leo katika Kanda ya
Nyanda za Juu Kusini ambapo usaili huo unafanyika Mkoani Mbeya Katika
Ukumbi wa Benjamini Mkapa uliopo Soko Matola Mkoani Mbeya.
Mpaka
sasa Washiriki wapatao 150 wamejitokeza kwaajili ya kushiriki shindano
hili la Tanzania Movie Talents ambapo washindi watatu kutoka kanda ya
Nyanda za Juu Kusini watazawadiwa kitita cha Shilingi laki tano za
Kitanzania na Baadae kupewa Tiketi ya Kuelekea Mkoani Dar Es Salaam
kwaajili ya kushiriki fainali itakayowakutanisha Washindi waliopatikana
katika Kanda ya Ziwa, Kati na kanda zilizobakia za Pwani na Kaskazini na
mshindi katika fainali hiyo atajinyakulia Kitita Cha Shilingi Milioni
50 za kitanzania pamoja na Mikataba minono kutoka Kampuni ya Proin
Promotions Limited na washindi kumi katika fainali hizo watakuwa chini
ya kampuni ya Proin Promotions Limited na kuweza kutengeneza filamu ya
Pamoja ambapo watanufaika na Mauzo ya filamu yao.
Mashindano
ya Tanzania Movie Talents yataendelea Mkoani Mbeya kwa Siku nne ambapo
siku ya jumanne washindi wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini watapatikana
na kupewa Zawadi zao.
No comments:
Post a Comment