Na Magreth
Magosso,Kigoma
Wanafunzi 27 waliomaliza katika Shule ya Sekondari ya Muyama katani humo,Wilaya ya Buhigwe mkoani hapa,wameshindwa kujiunga na masomo ya kidato
cha sita na vyuoni baada ya Mkuu wa shule Elias Mzehe kutafuna fedha za malipo
ya mtihani wa Taifa kidato cha Nnne .
Hali hiyo
imesababisha Wizara ya Elimu na Ufundi ishindwe kutoa matokeo ya wanafunzi 28 waliohitimu masomo 2013 kwa wakati na 2014 wajiunge na elimu ya juu kitendo kinachowaathiri wanafunzi hao kisaikolojia kwa
sintofahamu ya ufaulu wao ili wathubutu na mambo mengine .
Diwani wa kata ya Muyama Moshi Abdallah alibua hoja hiyo kwenye kikao
cha madiwani akimtaka mkurugenzi wa halmashauri ya buhigwe Charles Kaondo atoe ufafauni juu ya
uwajibishwaji kwa mwalimu mkuu wa
sekondari ya muyama na mamuzi
yaliyofanywa na idara ya elimu ili
kuwaokoa wanafunzi husika watimize ndoto
zao.
Akifafanua hilo Ofisa Elimu wilaya ya
buhigwe Malicelina Mbehoma alipohojiwa na
gazeti hili lini matokeo yatatoka alidai,
mchakato upo mbioni kukamilisha deni la wizara kwa wananfunzi 28 ambao wapo
njia panda hadi sasa kujiunga na elimu zingine kutokana na kukosa vyeti vya kujiunga na vyuo
sanjari na elimu ya ziada.
“ kweli
mwalimu alikusanya fedha za ada za mtihani wa taifa wa kidato hicho kwa wazazi na akafanyia
yake,hali iliyochangia watoto wakae majumbani lakini kuanzia siku 14 mambo
yatakuwa shwari” alisema Mbehoma
Aliongeza
kwa kusema,wamemwajibisha kwa ngazi ya awali ya kumshusha cheo,kulipa ada hizo
ambapo wanakata mshahara wake lakini kutokana na deni analodaiwa ni zaidi ya milioni mbili ni kubwa kuliko mshahara wake .
Alisema deni
hilo ni chachu ya kusubili hatua ya ziada hasa la kisheria kwa mujibu wa kanuni
na taratibu za sheria za kazi,hivyo kaka wa mwalimu Elias Mzehe amekubali
kusaidia hilo ili kupunguza ukali wa maisha ya mwalimu huyo na adhabu tarajiwa.
Kwa upande
wa Mkurugenzi Kaondo alimshanga diwani huyo kuibua hoja hiyo ambapo kimsingi haina haja kuwekwa hadharani katika kikao
hicho,kutokana na majibu aliyompa awali wakati akifuatilia changamoto `shida
ipo wapi huyu diwani alikuja ofisini kwangu na nikampa majibu mazuri sasa
anauliza tena kwenye kikao cha madiwani ili iweje”.
Naye Diwani
wa kata ya Kajana wilaya hiyo Robison
Ngeze akiongezea katika hilo alisema lengo la diwani ni kubainisha umma kinachoendelea katika
maeneo yao ili wabaini adha na utatuzi wa changamoto mbalimbali ikiwemo hiyo ambayo ni kero kwa walengwa na si kuumbuana .
Baadhi ya
wanafunzi Ajuae Daniel ,Amri Chares na Juma Rashid waliokosa matokeo kwa
nyakati tofauti walisema wanashindwa kujua lini matokeo hayo yatatoka na wahofu
wenye jinsia ya kike kuolewa katika muda
usiomuafaka kutokana na kukaa bila
kujishughulisha ni rahisi kushawishika.
No comments:
Post a Comment