Mhariri Mkuu MOblog Tanzania
Bunge
la Katiba linaloendelea mjini Dodoma ni vituko, vioja, uchafuzi, lugha
za matusi, mipasho kama ‘kitchen party’ au uwanja wa fisi pale kwenye
bar ya rafiki yangu wa kitambo mwandishi mwezangu Baraka Karashani.
Kwani
wajumbe wa Bunge la Katiba hawana aibu, woga au ndiyo kusema mshipa wa
aibu umeingia mafuta ya taa waheshimiwa nyie kulikoni jamani mbona taabu
wananchi hawaelewi nini kinaendelea maana ni serikali tatu au mbili
kama msahafu vile ahhaaaaa jamani.
Kwa
sababu watu wazima kurushiana matusi kama vile mpo kwenye gurio la nguo
au mnandani au sewa kwa madada zetu pale Buguruni haileti picha kwa
wananchi wanaotizama Bunge hilo nchi nzima halafu mnachukua 300,000 kwa
siku kibindoni kwenye nyama choma chako chako maana yake nini?
Kwa
mantiki hiyo basi jana nilitamani kwa udi na uvumba kutizama angalau
kwa masaa kadhaa majadiliano ya Bunge la Katiba linaloendelea mjini
Dodoma kwa kutambua umuhimu wake kwa vizazi vya sasa na vijavyo kwa hiyo
niliamua kwa makusudi kabisa kutizama wajumbe wa Bunge hilo maalum
wakirubana kwa hoja na si kwa vioja.
Lakini
Mjumbe pekee aliyenikuna jana ni Mhe Mbarouk Salum Ally kutoka visiwani
aliyesema kwamba wajumbe kutoka Zanzibar wamekuwa kama “Mbayuwayu’
vigeugeu kwa sababu wakiwa visiwani wanataka serikali tatu kwamba
muungano unawabana wakija Dodoma wanalowa maji wapole kama maji ya
mtungi hivi ni kweli?
Eti
ni kwanini wazanzibari wanalalamika kuhusu kero za muungano kila
kukicha mara hili mara lile lakini wakipata fursa wanaufyata kama
alivyosema Jussa juzi au si kweli jamani nini kinatokea mpaka wakifika
Dodoma hoja zao zinakuwa kapuni kabisa!
Mjumbe
huyo wa Bunge la katiba amesema kwamba wazanzibar wengi ndani ya Bunge
na hasa wa kutoka chama tawala wanalalamika chini kwa chini na wakiwa
visiwani wanasema sasa tunataka serikali tatu yaani serikali ya
Tanganyika, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Shirikisho lakini
wakifika kwenye vikao vya chama chao wanaloa kabisa hawathubutu kabisa
kusema chochote!
Lakini
hebu tujikumbushe kidogo wazanzibari kulalamika kwamba serikali ya bara
inawabana au Tanganyika kujificha ndani ya Muungano haikuanza leo yaani
piga ua huo ndio ukweli malalamiko ya watu wa visiwani kuhusu muundo wa
muungano yalianza tangu mzee karume watu wanasema na baadaye Aboud
Jumbe ambaye alitiwa ndani kabisa kwa kile wanachosema watu kuchafuka
kwa hali ya hewa 1984.
Kwa
hiyo swala la muundo na kero za muungano lipo kitambo Zanzibar inataka
mamlaka yake kamili na ndiyo maana hivi karibuni 2010 waliandika katiba
yao na kutamka bayana kwamba Zanzibar ni nchi ndiyo ambayo kimsingi
inasigana na katiba ya Muungano nani anabisha?
Sasa
kinachofanya wasiseme ukweli kwamba jamani serikali tatu ndio suluhisho
la kudumu la kero za muungano ni kipi? Basi kuanzia sasa kama hawawezi
na tumpe rungu Jakaya kikwete ya kuwalazimisha kubadili katiba yao na
Zanzibar si nchi tena mbali ni sehemu ya Muungano ndiyo kwa hapo nami
namuunga mkono Rais Jakaya Kikwete kwa hilo.
Hata
kama rasimu ya katiba ya Jaji warioba inasema serikali tatu ndio maoni
ya wananchi lakini kwa sababu wenyewe Zanzibar wameridhika na muundo wa
sasa hakuna shida kazi ni moja kwa chama tawala kuhakikisha Rais wa SMZ
Ali Mohammed Shein anabadilisha vipengele kadhaa kwenye katiba yao ya
2010 ili twende sawa ndiyo.
Watasema
sana lakini huo ndiyo ukweli waache malumbano yasiyokwisha huko
mjengoni kama vilabu vya pombe ya kibuku na mnazi kama uwanja wa fisi!
Naomba kuwasilisha
Kutoka MO Blog
No comments:
Post a Comment