Watoa huduma ya kisheria kutoka wilaya ya Kilolo wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi ,wakufunzi na uongozi wa LASWA |
Na Francis Godwin Blog
WANANCHI waliokuwa wakipoteza
haki zao kwa kukosa msaada wa kisheria katika wilaya ya Iringa na
Kilolo mkoani Iringa watafutiwa ufumbuzi wa kudumu wa kisheria kwa
kusogezewa wataalam watakao wapa msaada wa kisheria bila malipo
Akizungumza jana mjini Ilula wilaya ya Kilolo wakati wa kuhitimisha mafunzo ya kisheria kwa wahitimu hao katibu mtendaji wa asasi isiyo ya kiserikali ya Legal Aid and Social welfare association( LASWA) mkoani Iringa Oscary Waya alisema kuwa jumla ya vijana zaidi ya 50 wamepewa mafunzo ya kisheria ili kuisaidia jamii ambayo imekuwa ikipoteza haki kwa kukosa msaada wa kisheria.
Alisema kuwa asasi yake imeamua
kutoa mafunzo ya kisheria kwa vijana hao ambao kutoka kata za wilaya
za Kilolo na Iringa Vijijini ili kuisaidia jamii ya maeneo hayo kupata
huduma ya bure ya msaada wa kisheria wa bure .
Bw Waya alisema kuwa kutokana
na uvunjifu wa amani na kushindwa kutimizwa kwa sheria kwa wananchi wa
vijijini, LASWA waliamua kuwaandaa vijana hao na kuwapa mafunzo
ambayo yataendelea kuwa msaada kwa wananchi na kuepuka kupoteza muda
kwa kukimbilia mahakamani ama katika mabaraza ya kata.
Alisema kuwa wahitimu wa
mafunzo ambayo yamefanyika kwa miaka mitatu kwa nyakati tofauti
yamewezesha watu 27 kutoka wilaya ya Kilolo na wengine 24 kutoka wilaya
ya Iringa Vijijini kuhitimu ambapo kwa miaka mitatu jumla ya milioni
179,990,000 zimetumika katika kutoa mafunzo ili vijana hao ili kuisaidia
jamii kuondokana na kero mbalimbali zinazowakandamiza kwa kutojua
sheria .
Baadhi ya wahitimu
wakizungumzia mafunzo hayo Bw. Ramadhan Mhehe, Bi. Rukia Kihwele, Bw.
Mkude Mng’ong’o na Lucas Kidungu walisema kuwa kero ambazo wamekuwa
wakikumbana nazo katika maeneo ya vijiji, kata na tarafa ambazo wananchi
wanakabiliana nazo ni pamoja na kero za migogoro ya ardhi, ndoa,
mirathi, unyanyaswaji wa kijinsia kwa wanawake na wanaume ambapo kero
nyingi chanzo chake zinatokana na mfumo dume uliopo katika jamii ya watu
wanamoishi.
Hata hivyo alisema kuwa kwa kuwa vijana hao wataendelea kutoa huduma ya bure ambayo itawasaidia wananchi kutoa msaada wa kisheria ni vema serikali ama wahisani kujitokeza ili kuwasaidia vijana hao ambao wataendelea kufanya kazi hiyo kwa kujitolea bila malipo tofauti na mabaraza ya kata . Bw waya alisema kwa sasa vijana hao mbali ya kuifanya kazi hiyo ya huduma ya kisheria bado wameanzishiwa asasi zao mbili moja ikiwepo Ilula na nyingine Mseke na kwa sasa wana miradi ya kiuchumi ukiwemo wa upandaji miti.
Kwa upande wake mgeni
rasmi katika ufungaji wa mafunzo hayo ,mwanasheria wa Halmashauri ya
wilaya ya Kilolo Bw. Abdul Manga aliwataka wahitimu hao kwenda kutoa
msaada wa kisherika katika kila kata katika wilaya za Kilolo na Iringa
Vijijini kwa uhakika bila kuwatoza pesa wananchi kama ilivyo
mabaraza ya kata ambayo yamekuwa yakilazimisha kesi ili kupata pesa .
Manga alisema kuwa mabaraza ya
kata yanayoshughulikia kuamua kesi na kero mbalimbali za wananchi
kutokana na kuhitaji malipo ya fedha ili waweze kufanya maamuzi ya
kusimamia sheria katika maeneo yao yamesababisha watu wengi kujiweka
kando na mabaraza hayo na badala yake wamekuwa wakiendelea kuteseka
kutokana na kushindwa kupatiwa haki kwa kukosa pesa.
“Malengo ya LASWA ya kutoa
mafunzo kwa ninyi watu 51 ili kila kata za Iringa Vijijini na Kilolo
watu wapate msaada wa kisheria ni makubwa na yamezingatia ubinadamu na
hali nzima ya utu kwa watu wote kwa kuwa juhudi zao za kutoa mafunzo
unalenga kuitatulia kero mbalimbali za kijamii wananchi wote wa
vijijini, hivyo mtatakiwa mkawajibike kikamilifu kwa jamii na kuwashauri
wananchi kutopenda kesi kwa jambo ambalo linawezekana kupatiwa
ufumbuzi ”,
Lakini pia ninaiomba serikali
ili sisi wanasheria tuweze kutoa mafunzo na elimu kwa mabaraza yetu yote
ya kata ambayo yanasimamia haki na sheria kwa wananchi wetu ili kila
wakati sheria ambazo zinatakiwa kuamuliwa zitende haki kwa wananchi mara
kwa mara ndani ya jamii endapo mabaraza ya kata yatapatiwa elimu
mbadala yataweza kutenda haki sahihi kwa wananchi wetu.
Alisema kuwa uwepo wa gharama
kubwa za kufuatilia kesi katika maeneo ya vijijini pamoja na
kuwasafirisha mashahidi na kuupata ukweli kwa walalamikaji ambao umekuwa
ukitendewa ndivy sivyo ambapo alisema kuwa itakuwa ni faraja kubwa
endapo mafunzo hayo yataleta faida kubwa kwa wananchi ambao wanatakiwa
wakombolewe kupitia watu waliojifunza mafunzo ya sheria.
|
No comments:
Post a Comment