Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja(kulia) akichangia mjadala wakati wa kupitia mapendekezo ya Wafungwa wanaopendekezwa kuachiliwa na mpango wa Parole kabla ya kufungwa rasmi Kikao cha 25 cha Bodi hiyo leo Aprili 17, 2014 katika Ukumbi wa Hoteli ya Charity, Jijini Arusha(kushoto) ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mhe. Jaji Mstaafu Eusebia Munuo akifuatilia mjadala huo. Wajumbe wa Bodi ya Taifa ya Parole wakipitia makabrasha yenye mapendekezo ya Wafungwa watakaoachiliwa na mpango wa Parole kabla ya kufungwa rasmi kwa Kikao hicho lei Aprili 17, 2014 katika Ukumbi wa Hoteli ya Charity, Jijini Arusha. Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Jaji Mstaafu Eusebia Munuo(katikati) mapema leo kabla ya kufungwa rasmi kwa Kikao kilichofanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Hoteli ya Charity, Jijini Arusha(kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Jaji Mstaafu Eusebia Munuo(katikati aliyeketi) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi hiyo mara baada ya kufungwa rasmi kwa Kikao cha 25 cha Bodi hiyo kilichofanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Hoteli ya Charity iliyopo Jijini Arusha(kulia aliyeketi) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja ambaye pia ni Katibu wa Bodi ya Taifa ya Parole(kushoto aliyeketi) ni Mjumbe wa Bodi, Naibu Kamishna wa Magereza Mstaafu, John Nyoka.
No comments:
Post a Comment