Pages

KAPIPI TV

Tuesday, April 15, 2014

POLISI WAPEWA ELIMU YA UKATILI WA KIJINSIA KIGOMA

Na Magreth Magosso Kigoma.

POLISI  Mkoa wa Kigoma wametakiwa wawe makini katika upokeaji wa elimu sahihi ya ukatili wa kijinsia kwa lengo la kudhibiti na kutatua changamoto hiyo kwa wananchi ambayo inachagia kuzorotesha  uchumi wa  jamii zetu.

Akifafanua hilo kwenye uzinduzi wa mafunzo ya siku Nne kwa wakaguzi wa madawati ya jinsia na maofisa polisi wa Kigoma na Tabora wakilenga kuwapa elimu  ya utambuzi juu ya ukatili wa kijinsia  kuwa ni  kosa la jinai kwa tija ya kupunguza vitendo hivyo na kulinda utu wa wahanga.

Pia Naibu Kamishna mkuu wa Polisi Dawati la jinsia na watoto Taifa Adolphina Chialo alisema, miongoni mwao hushindwa kuwasaidia wahanga waliofanyiwa vitendo  vya ukatili kutokana na mfumo dume ulioathiri jamii kuona wanaume kupiga wake zao ni sehemu ya upendo na mwanamke akichukua hatua anatengwa na familia hali inayozidisha unyonge kwa wanawake .

“badilikeni, ukatili unaathiri mfumo wa maisha ya wahanga kisaikolojia na kimwili,sasa mafunzo haya chachu kwenu kuwajibika,hatuna bajeti ya madawati toka serikalini lakini tuonyeshe nia yetu kwa pamoja tutengewe fungu la kuendesha  na semina kwa wadau na umma” alisema Chialo.

Akifungua mafunzo hayo mgeni rasmi ambaye pia ni Ofisa ustawi jamii Manispaa ya Kigoma Ujiji Agnes Punjila alishauri askari polisi waongeze udadisi kwa kufuatilia vyombo vya habari na matukio kadhaa katika mikoa mingine na nje ya nchi ili kujiimarisha katika kukabiliana na sheria tata za kuwashtaki watendaji wa matukio husika.

Kwa upande wa Mkaguzi mkuu wa dawati la jinsia kigoma Amina Kihando alisema changamoto ya  kutofanikisha kukamata wahalifu wasifikishwe kwenye vyombo vya sheria inatokana  na wahanga kutiwa hofu na jamii kwa mujibu wa mila,tamaduni na imani za kidini pasipo kubaini athari zake pia ni chachu kwa familia kuwa sehemu ya ukatili kutokana na kumaliza kesi kinyemela.

Alisema watu wa ukanda wa ziwa ni miongoni mwa wahanga wa matukio hayo,lakini wanashindwa kuwapeleka wahusika mahakamani kutokana na changamoto ya usafiri na kipato cha kugharamia kesi husika,Huku akiri matukio ya ubakaji ni mengi pamoja na walezi wa familia huyafumbia macho kwa hofu ya kujenga uhasama baina ya mtenda na mtendewa.

Naye Kamanda wa Polisi Fresser Kashai  na wakili wa Halmashauri ya wilaya ya kigoma Idd Ndabhona kwa nyakati tofauti walisema mafunzo hayo ni tija kwa jamii husika kutokana na kushamiri vitendo vya kutelekeza watoto,ubakaji na lugha chafu  ambapo jamii huona ni kawaida ilihali  kisheria ni kosa la jinai,mtendewa ana haki za msingi kushtaki.
 

Mtandao huu umebaini kuwa  ,kitaifa madawati  ya kijinsia yapo 417 ambapo madawati 8 yana ofisi zake,sanjari na watendaji wake hawana upeo mpana wa sheria na namna ya kukabiliana na kesi za aina hizo hali inayochangia ukatili kusimika mizizi katika familia na viongozi kwa ujumla hasa kwa kutojitambua,kuthamini, kujali na kuwajibika.

Hivyo kuchangia  kizazi kisichojali ambapo Aprili,2014 dawati hilo mkoa limepokea kesi 20  kutoka wilaya sita za mkoani haopa,huku kesi 6 zipo mahakamani ni moja ya kiashiria cha elimu finyu kwa umma, kukosekana kwa sheria maalum juu ya ukatili ili  kusaidia wahanga  kesi zimalizwe mapema kwa mujibu wa sheria husika  tija kuboresha maisha ya umma kwa kuzingatia usawa na haki.

No comments: