Pages

KAPIPI TV

Tuesday, April 15, 2014

SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS LAPOKELEWA VYEMA NA WATANZANIA MIKOA YA MWANZA NA DODOMA

  
Na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Dodoma

Watanzania wa Mikoa ya Mwanza na Dodoma wameipongeza kampuni ya Proin Promotions Limited kupitia shindano lao la Kusaka vipaji vya Kuigiza Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents kwa kuamua kuanzisha shindano hilo ambalo limeanza kuonyesha matumaini kwa vijana wenye vipaji vya kuigiza ambao walisahaulika katika tasnia hiyo ya filamu nchini.

Shindano hili la Tanzania Movie Talents linawawezesha watanzania wote wenye vipaji vya kuigiza kuweza kujitokeza ili kuweza kuonyesha vipaji vyao na kuvikuza kwa kutumia fursa hii iliyoanzishwa na kampuni ya Proin Promotions Limited


Wakiongelea kuhusu shindano hili la Tanzania Movie Talents, wakazi wa Mkoa wa Dodoma walisema" tunafurahishwa sana na shindano hili kuweza kuanzishwa Tanzania na Afrika Mashariki na Kati kwani sasa tunaweza kupata nafasi katika tasnia ya filamu baada ya kuanza kuonyesha vipaji vyetu vya kuigiza"

"Tanzania Movie Talents inamgusa kila mtanzania mwenye vipaji vya kuigiza kwani ni nafasi kwa vijana na watanzania wote wenye vipaji vya kuigiza kuweza kujitokeza kwaajili ya kuonyesha uwezo na vipaji vyao vya kuigiza, Shindano la Tanzania Movie Talents ni mkombozi wa Vijana na watanzania ambao wana vipaji vya kuigiza ambapo kupitia shindano hili vijana wanaweza kupata nafasi za ajira kupitia tasnia ya filamu nchini ambapo washiriki watakuwa wameweza kuonekana na hatimaye kuitwa kwaajili ya kufanya kazi.


Kwa upande wake baadhi ya wafanyakazi wa timu ya Tanzania Movie Talents walithibitisha kuwa 'Tanzania Movie Talents imepokelewa vizuri na watanzania wa Mikoa ya Mwanza na Dodoma  kwani tumeona ongezeko la washiriki waliojitokeza kwaajili ya usaili wa kushiriki katika Shindano hili kubwa na la kwanza Afrika Mashariki na Kati.

 Hii nikutokana na ukweli kwamba washiriki wote wanaofika kwaajili ya Usaili hawatozwi kiasi chochote cha pesa kutoka timu ya Tanzania Movie Talents na pia kufurahishwa na uamuzi wa Majaji wa Timu ya Tanzania Movie Talents,  niwazi kabisa kuwa kutotozwa kwa kiasi chochote cha pesa kwa washiriki kumekuwa ni kivutio kikubwa kabisa hivyo kuongeza idadi ya washiriki katika kila Kanda tunayoenda"alisema Stephen Mapunda Mkazi wa Mkoa wa Dodoma

No comments: