Pages

KAPIPI TV

Saturday, March 29, 2014

SINGPRESS YAPATA KATIBU MTENDAJI MPYA


DSC07415
Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari (Singpress) mkoa wa Singida, Seif Takaza akifungua mkutano mkuu wa kawaida wa klabu hiyo uliofanyika mjini Manyoni mwishoni mwa wiki.Kulia ni makamu mwenyekiti Damiano Mkumbo na kulia ni kaimu katibu mtendaji,Emmanuel Michael.(Picha na Nathaniel Limu).
DSC07419
Baadhi ya wanachama wa klabu ya waandishi wa habari (Singpress) mkoa wa Singida,wakifuatilia mkutano mkuu wa kawaida wa (mwaka 2013) klabu hiyo uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kanisa Katoliki mjini Manyoni.

Na Nathaniel Limu, Manyoni
KLABU ya waandishi wa habari (Singpress) mkoa wa Singida imemchagua kwa kishindo Pascal Tantau (32),kuwa katibu wake mtendaji kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Abby Nkungu ambaye anadai kwa sasa afya yake ina mgogoro.

Pascal kijana aliyemaliza chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) alipata kura 15 za ndio,mbili zilimkataa na moja iliharibika.

Pascal atakuwa madarakani hadi mwishoni mwakwani (2015) uchaguzi mkuu utakapofanyika kwa mujibu wa katiba ya klabu hiyo.

Pascal aliwashukuru wanachama wenzake kwa kumwamini na kumkabidhi nafasi hiyo nyeti. Ameahidi kwamba atawatumikia kwa nguvu zake zote na kwa maarifa lengo kuu ikiwa ni  klabu hiyo iweze kupaa kimaendeleo katika kipindi chake cha uongozi.

“Niwaahidi pia kwamba katika uongozi wangu nitatumia mbinu shirikishi ili kila mwananchama aweze kutoa mchango wake mbalimbali kuendeleza klabu na kuboresha ustawi wa wananchama.Nitajitahidipia kuhakikisha klabu inakuwa na mahusiano mazuri na wadau wake mbalimbali”, alisema kwa kujiamini.

Abby Nkungu amelazimika kujiuzulu nafasi ya ukatibu mtendaji wa Singpress,kwa madai kwamba ameagizwa na daktari wake aishiye nchini Kenya, kuwa asifanye kazi yo yote ambayo atalazimika kutumia akili nyingi.

Ilielezwa mbele ya mkutano huo mkuu, kwamba Nkungu aliweza kuombwa na kamati tendaji kusaidia kuandaa maandalizi ya mkutano mkuu,alikataa kata kata.

Hata alipoitwa tena na kamati tendaji ili aweze kufafanua zaidi juu kutakiwa na daktari wake awe kwenye mapumziko yasiyo na bughudha yo yote…yaani ‘total rest’,wakati anaendelea na kazi kama kawaida zikiwemo za safari ndefu pia alitupilia mbali wito huo.

Kutokana na hali hiyo mkutano mkuu huo umeazimia Nkungu asigombee tena uongozi wowote katika klabu ya Singpress kwa muda wote wa maisha yake yaliyobaki.Pia amesimamishwa uanachama kwa kipindi cha miezi tisa.

Hii ni mara ya pili,Nkungu kusimamishwa uanachama wa klabu ya Singpress.

MWALIMU AMVUNJA MGUU DENTI KISA MAPENZI - KIGOMA


Na Magreth Magosso,Kigoma

Mwanafunzi wa Darasa la saba katika Shule ya Msingi Bangwe Kata ya Bangwe kwenye Manispaa ya kigoma Ujiji mkoani hapo  amepigwa na mwalimu wake katika maeneo mbalimbali ya mwili wake na kumvunja mguu wa kulia baada ya kumkatalia kumpa penzi.


Akizungumza na mwandishi wetu  jana wodi namba 5 katika hospitali ya Rufaa ya Maweni mwanafunzi huyo aliyetambuliwa kwa jina la Zubeda Athuman (14)  alisema chanzo cha mwalimu huyo kumchukia na hatimaye kufikia hatua ya kumpiga na kumvunja mguu  ni wivu wa kukataliwa kupewa penzi ,hali iliyomfanya mwalimu huyo kumpa  adhabu za hapa na pale kila aendapo shule.


Hali hiyo ilimfanya  mwanafunzi huyo kuwadokeza wazazi wake ambapo walimwambia avumilie,ndipo jumatano ya wiki hii mwalimu alimpa adhabu ya kuchimba shimo na alikataa kufanya hivyo baada ya kuona hana kosa la msingi la kumpa adhabu hiyo.


Mwalimu huyo alifikia hatua ya kumfuata nyumbani kwao  machi,22,2014 saa 12.30 jioni hali iliyowashtua wazazi na kumuhoji mtoto juu ya hilo ndipo binti alipokwenda shule Machi,24,2014  alimuliza mwalimu huyo sababu ya kumfuta kwao, hali hiyo ilimchefua mwalimu na kutoa maneno ya kashfa  na kumpiga  vibao vya uso na kusababisha maumivu mbalimbali ya mwili wake ikiwemo kuvunjika kwa mguu.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Maweni Macris Yakayeshi akiri mwanafunzi huyo kuvunjika mguu wa kulia sambamba na kuvimba uso na kupelekea mdomo kwenda upande na wiki ijayo anatarajia kumwekea `P.O.P’.


Dr.Yakayeshi alibainisha kuwa kutokana na tatizo alilonalo itamlazimu kukaa na mhogo si chini ya wiki sita ili mguu utengamae sambamba na kuitaka jamii ibadilike na matukio ya udhalilishaji wa kijijnsia huku akidai alifikishwa hapo kifua kikiwa wazi ili hali binti ni rika la balehe na kuomba sheria ichukue mkondo wake.


Mwenyekiti wa Mtaa wa Kamala katani humo Curthbert Kusongwa alisema, kwa maelezo aliyoyapata kutoka kwa walimu wa shule hiyo walidai binti alikataa adhabu aliyopewa na kumpiga kofi mwalimu na ndipo mwalimu akamwambia akamlete mzazi wake,wazazi walipofika alidai alimvamia mwalimu na kuanza kumpiga hali iliyolazimu jeshi la polisi kuingilia  hekaheka kiyo.


Akizungumzia tukio hilo Athumani Moshi ambaye ni baba wa Zubeda alisema  alishangaa kumuona mwanae amerudishwa shule huku akiwa amevimba uso na mdomo ndipo akadai kuitwa na mwalimu husika,alipofika shule na kuonana na mwalimu husika hakuwa muungwana kutokana na kauli chafu na kebehi.


Moshi alisema baada ya kauli hizo  ghafla mwalimu akamkata mtama mwanae na kuanguka chini ndipo wakapigana,huku akikiri awali alipata kuelezwa juu ya adha ya mwalimu huyo kwa binti yake hadi kufikia hatua ya kumfuata usiku siku za mapumziko sanjari na kumpa adhabu zisizostahili kwa kisa alikataa kuwa nae kimapenzi.


Kamanda wa Polisi mkoani hapa Zedekia Makunja alipoulizwa kama analifahamu hili akadai naam ila wataitwa machi,31,mwaka huu.


Kwa nyakati tofauti Mariamu Issa na Winyfrida Bwire walisema sheria ya mwanafunzi juu ya adhabu inajulikana ,walimu hawana budi kulea watoto kwa kuwafundisha adabu ,huku wakidai kuna namna kati ya mwanafunzi na mwalimu haiwezekani kukataa kwa adhabu amvunje mguu.

Thursday, March 27, 2014

SIRI YA CCM KUNG'ANG'ANIA SERIKALI MBILI KIKATIBA


katuni 83f0e
Katika maisha ya kawaida, binadamu ana msimamo wake na hata uamuzi asiopenda ubadilike.
Katika medani ya siasa nchini msimamo wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) kuhusu Muungano na muundo unafahamika. Ni muundo wa kutaka Serikali mbili ambao chama hicho unakipigania kwa udi na uvumba.(Hudugu Ng'amilo)

Hata hivyo, msimamo huo ni kinyume na mapendekezo au matakwa ya wengi kama ilivyoainishwa kwenye Rasimu ya Pili ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Tume hiyo iliyokuwa chini ya Jaji Joseph Warioba ilikusanya maoni ya wananchi na ilipendekeza muundo wa Muungano wa Serikali tatu.

Hivi karibuni akifungua Bunge Maalumu la Katiba, Rais Jakaya Kikwete akaunga mkono msimamo wa chama chake, jambo lililoibua mjadala unaoendelea hadi sasa.
Hoja ya Serikali mbili

Kwanini CCM wanataka Serikali mbili na siyo tatu au moja kama ilivyo maoni ya wananchi walio wengi kwa mujibu wa maelezo ya Tume ya Warioba? Makala haya yanachambua hoja hiyo.

Profesa Bakar Mohammed ni Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Siasa na Utawala ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, anayesema msimamo wa CCM wa kudai Serikali mbili unatokana na hofu ya uhafidhina wa kuogopa mabadiliko.

Anasema viongozi wengi wa CCM wanasumbuliwa na hofu na woga wa mabadiliko na kwamba wanakuwa wagumu kuyakubali yanapotaka kutokea.

"Kama mtu unaangalia madaraka zaidi, lazima kunakuwa na woga, na hii ni hulka ya binadamu kuwa na woga wa kuacha kile ulichokizoea... Lakini ukiangalia masilahi ya nchi na kuacha yale yanayokusukuma kusingekuwa na wasiwasi huu unaoonekana sasa," anasema.

Anasema CCM inachofanya ni kuhakikisha haking'oki madarakani, huku viongozi wake wakiamini kuwa wana sifa za kuongoza na siyo wengineo.

Profesa Bakari anailinganisha hofu ya sasa ya CCM na ile waliyokuwa nayo viongozi wa chama hicho miaka ya 1990 zilipoanza vuguvugu za mabadiliko ya siasa za vyama vingi. Anasema CCM kiliendesha propaganda kuwa mfumo wa vyama vingi haukuwa na tija na ungeleta vita.0
inShare

Hofu hiyo anasema ndiyo inayokifanya chama hicho kikongwe kuhofia kung'olewa madarakani.
"Woga huo bado upo, wanaogopa pengine mfumo ukiwa wa Serikali tatu uwezekano wa wao kubaki madarakani utakuwa mdogo," anafafanua.

Anaongeza kusema kuwa hofu ya CCM siyo kwa ajili ya masilahi ya nchi, badala yake inaonekana chama kinaangalia masilahi yake.
Ingekuwa vyema anasema kwa CCM kueleza madhara yanayoweza kulikumba taifa ikiwa muundo wa Serikali tatu utapita.

"Wanatoa hoja kuwa mfumo wa Serikali tatu unaweza kusambaratisha nchi, lakini hakuna uhakika kama mfumo huu uliopo nchi hauwezi kusambaratika," anasema.
 
Hofu ya kuyumba na kuanguka
Mhadhiri mwingine wa chuo hicho, Dk. Benson Bana anasema siri ya CCM kung'ang'ania Serikali mbili inatokana na hofu ya kuyumba na kuanguka.

Anasema CCM kimekuwa madarakani na mfumo huo kwa miaka 50 na kwamba hofu yao ni kuwa ukiondoa Serikali mbili kinaweza kuyumba na kuachia madaraka.

Anasema misingi ya wanasiasa ni madaraka, na kwamba ukishayapata, huwezi kuyaachia kirahisi.
"Misingi ya wanasiasa ni madaraka... Kuyalinda, kuyahifadhi na kuyatumia madaraka yale kwa namna yoyote...Huwezi kuyaachia madaraka kirahisi. Utafanya ujanja, utatumia mbinu chafu ili tu kuhakikisha unabaki madarakani, na hiki ndicho wanachofanya CCM," anasema.

Dk. Bana anasema CCM kingeeleweka na kingekuwa na mwonekano mzuri zaidi endapo wangepigania kuwapo kwa Serikali moja.

"Wangekuwa wanataka muungano imara, endelevu na uliokomaa wangeelekeza katika Serikali moja...Lakini hawataki kwa sababu wanajua moja inaweza ikawanyima uongozi," anasema.Dk. Bana anasema ni vyema wananchi wakaelimishwa huu muungano una faida gani na wanafunzi shuleni katika elimu ya uraia waelezwe faida zake.

"Ingekuwa wazi tungejua nani anafaidika na nini, mikopo misaada, nani anachangia nini...Je zile sababu za waasisi za kuungana bado zipo sasa miaka 50 ya Muungano, ule woga kuwa Zanzibar itamezwa bado upo leo?" Anahoji.

Anaongeza kuwa ni vyema kwa watawala kutazama mazingira ya sasa ya siasa zetu kwa kile anachoeleza kuwa hata Katiba ikipita ikakubali kuwapo wa Serikali mbili, bado wananchi watahoji mantiki ya muundo huo.

Msomi mwingine wa siasa, Dk. Alexander Makuliko anasema hofu ya CCM ni kuwa ndio iliyouasisi Muungano wa Serikali mbili, hivyo isingependa hali hiyo ibadilike.

Anaendelea kusema kuwa CCM imezoea mfumo huu na kuwa ikiukosa itaathirika, kwakuwa ni sera yake na imekuwa ikiitekeleza, lakini msimamo wa wananchi ndiyo kitu cha msingi kuzingatiwa. Hoja zijengwe na zisikilizwe, ubabe hautakiwi, busara inahitajika zaidi.

Anasema pamoja na suala la Serikali mbili kuwa ni pimajoto ya uhai wa CCM, hata hivyo hoja zinazotolewa katika kutetea msimamo wao ni nzuri tu na zinazoeleweka vyema.

"Sioni kama wanang'ang'ania, lakini ukweli ni kuwa kila chama kina sera yake, na CCM kimeweka sera yake katika suala la Muungano wao wanasema ni Serikali mbili, na siyo tatu...kwamba tatu zitaongeza gharama na mengineyo, ni sababu za msingi kabisa," anasema.

Anaongeza kuwa hoja zinazotolewa na chama tawala ni kubwa na siyo za kupuuzwa, lakini vilevile kero zinazotajwa kuhusu mfumo wa Muungano uliopo nazo zipo na zinaweza kutatuliwa katika mfumo uliopo.

"Unajua hivi vyama kila kimoja kinataka kuvutia kwake, hata bila rasimu ya Warioba...Ninashauri walete hoja, kisha watu wazipime hizo hoja, kwanini serikali mbili, na wale wa tatu tayari wameleta hoja na ushahidi, watu waachwe wapime," anasema na kuongeza:

''Jambo la msingi kuzingatiwa ni kuwa mawazo ya wananchi wengi yataonekana wakati wa kura za maoni. Angalizo ni kuhakikisha kuwa kura hiyo isije ikachakachuliwa.''
CHANZO MWANANCHI

Wednesday, March 26, 2014

MITAMBO YA TELEVISHENI KWA MFUMO WA ANALOJIA KUZIMWA TABORA NA SINGIDA MARCHI 31 2014

Naibu mkurugenzi wa Idara ya Utangazaji Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Bw.Frederick Ntobi akizungumza na waandishi wa habari Tabora kuhusu kuzima mitambo ya Analojia mikoa ya Tabora na Singida ifikapo tarehe 31 marchi mwaka 2014.
Meneja wa kanda ya kati TCRA Bi.Maria Sasabo akizungumzia ubora wa matangazo ya kupitia mfumo wa Dijitali nafaida zake.
Moja kati ya Antena za King'amuzi cha Startimes ambacho waandishi wa habari walielekezwa matumizi yake sahihi na namna kinavyoweza kukupatia picha zenye ung'avu.





DC IGUNGA AHAMASISHA WANANCHI KUJIUNGA NA MFUKO WA CHF

Mkuu wa wilaya ya Igunga Bw.Elibariki Kingu akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Matinje wakati akihamasisha Mfuko wa Afya ya Jamii CHF katika vijiji zaidi ya 52 wilayani Igunga.
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Matinje wakinyoosha mikoni juu ishara ya kuukubali Mfuko huo wa Afya ya Jamii Tiba kwa Kadi maarufu TIKA baada ya kumsikiliza mkuu wa wilaya ya Igunga Bw.Kingu ambaye alikuwa akihamasisha mfuko huo.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nzega Bw.Amos Kanuda akitoa msaada wa kuwalipia  kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii  Wazee wa Kijiji cha Matinje wilayani Igunga.
Mkuu wa wilaya ya Igunga Bw.Elibariki Kingu akionesha Kadi yake ya Bima ya Afya ikiwa ni hatua ya kuwahamasisha  wakazi wa Kijiji cha Matinje kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii wilayani Igunga.





TUME YA MACHIBYA YARUDI KICHWA CHINI-KIGOMA

Na Magreth Magosso, Kigoma.

TUME  iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa Kigoma Luten kanali Mstaafu Issa Machibya kufuatilia zana za uvuvi zilizoibiwa na kupelekwa nchi ya kidemocrasia ya Congo haijafanikiwa kurudi na zana hizo kutokana na kuwepo kwa utata baina ya viongozi wa serikali hiyo.
 
Akizungumzia hilo mwakilishi wa wavivu Salumu Shabani ambaye alikuwa katika tume hiyo alisema kuwa jitihada za mkuu wa mkoa wa kigoma  ni kubwa lakini kutokana na mfumo uliopo katika nchi ya Congo imekuwa ngumu kuweze kutimiza yale ambayo analenga kuwasaidia wavuvi mkoani hapa.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jana kigoma ujiji, Shabani alisema licha ya kuwepo kwa mikataba ya ujirani mwema baina ya nchi hizo kwa lengo la kuwepo na mahusiano baina yao na viongozi kuhakikisha zana zinazoibiwa na kupatikana katika nchi hizo zirudishwe bila masharti magumu wala urasimu wowote bado mkataba wa ujirani mwema unakiukwa na n chi hiyo.
 
Alisema kuwa, wizi unaofanywa na watu wa nchi hiyo umekuwa ukurudisha nyuma maendeleo ya wavuvi kwa kuwatia umaskini ambapo asilimia 80 ya wakazi wa mkoa huo  wanategemea shughuli za uvuvi ili kulea familia zao na kumudu hali ya maisha.
 
Aidha  mara kadhaa uongozi wa mkoa wa kigoma umekuwa ukituma wawakilishi kufuatilia zana hizo bila mafanikio ambapo fedha za serikali zimekuwa zikitumika kuhakikisha wavuvi wanapatiwa zana zao na wanafanya shughuli za uvuvi kwa amani na utulivu katika ziwa Tanganyika.
 
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Mwenyekiti wa wavuvi Ramadhani Kanyongo na Makamu wake Sendwe Ibrahimu walisema kuwa hadi ifikapo 2025 uvuvi wa mkoa wa Kigoma utakuwa ni ule wa kusonza kwa mitubwi na sio uvuvi uliopo kipindi hiki sambamba na mapato ya mkoa na Halmashauri kuporomoka kwa kasi na uchumi kushuka.
 
Walisema kuwa kutokana na kukidhiri kwa wizi katika mwambao wa ziwa Tanganyika bei ya mazao ya samaki na dagaa imepanda kutokana na wavuvi na wamiliki kuhofia kuingiza vyombo vyao ziwani na wavuvi kuhofia usalama wa maisha yao.
 
Walisema kuwa awali mwaka 2003 kulikuwa na mitubwi 168 katika mwalo wa kibirizi ambapo kwa sasa imebaki 45, huku mwalo wa katonga kulikuwa na mitumbwi 200 na sasa ipo 168 hali inayokatisha tama kuendelea kufanya shughuli za uvuvi katika ziwa hilo.
 
Hivi karibuni Mkuu wa mkoa akizungumza na wavuvi alisema kwa kushirikiana na wananchi, wavuvi na vyombo vya ulinzi na usalama tatizo hilo litapatiwa ufumbuzi ikiwa ni pamoja na kuendesha msako wa kuwakamata wahamiaji wanaoishi kinyume cha sheria na kuwarudisha katika nchi zao.
                                                               
Akijibia hilo ubalozi mdogo wa Nchi ya Congo  Kigoma Balozi Riky Molema   akiri mfumo wa uendeshaji wa serikali ya Tanzania na serikali ya Congo uko tofauti na hivyo kuwa vigumu kupata zana hizo kwa wakati muafaka na kuwataka wavuvi kuwa wavumilivu .
 
Alisema kuwa ili kuondoa tatizo la wizi katika mwambao wa ziwa ni lazima dhati ya kuthubutu kwa viongozi husika wa serikali zote mbili kuunda ulinzi shirikisha ndani ya ziwa hilo kwa kufanya doria ya pamoja na kuhakikisha wimbi la wizi katika ziwa hilo unatokomea.

Tuesday, March 25, 2014

NAMPE AMNADI RIDHIWANI, ATAKA WANACHALINZE KUMCHAGUA KUWA MBUNGE WA JIMBO LAO


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Mkoko wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni za kumnadi kumgombea Ubunge jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete ambapo wananchi hao walielezwa kitendo cha kuzuiwa kupiga kura ni sawa na ubakaji wa Demokrasia na CCM itakula sambamba na wabakaji wa Demokrasia.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambaye pia ndiye Mratibu wa kampeni za mgombea wa CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete akionyesha kadi Chadema  iliyorudishwa na Ndugu Subira Mrisho ambaye alikuwa mhamasishaji wa Chadema katika kijiji cha Mkoko,pia katika kata ya Msata Katibu Kata wa Chadema amerejea CCM anaitwa Mrisho Issa pamoja na mwananchama mwingine anayejulikana Kassim Msakamali wamerejea CCM
Katibu wa CCM mkoa wa Mtwara Ndugu Shaibu Akwilombe akihutubia wakazi wa kijiji cha Mkoko kwenye mkutano wa kumnadi mgombea wa CCM Ndugu Ridhwani Kikwete.
Mtela Mwampamba akihutubia wakazi wa kijiji cha Mkoko na kuwasihi wananchi hao kutambua mahusiano ya Tanzania na Chama Cha Mapinduzi.
Diwani wa Kata ya Msata akiwahutubia wananchi wa kiji cha Mkoko wakati wa kumtano wa kampeni wa kumnadi mgombea wa CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete.
Katibu wa CCM Wilaya ya Kisarawe Ndugu Zena Mgaya akiwa na Shumia Sharif mjumbe wa mkutano mkuu Taifa kutoka wilaya ya Bagamoyo na pia kiongozi wa kampeni kata ya Msata wakiwa kwenye mkutano wa kampeni za CCM kijiji cha Mkoko jimbo la Chalinze.
Wananchi wa kijiji cha Mkoko wakionyesha picha za mgombea wao wa Ubunge Ndugu Ridhiwani Kikwete wakati wa mkutano wa kampeni ulofanyika kijjini Mkoko.
Mapokezi ya katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye katika kijiji cha Mkoko.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahtubia wakazi wa kitongoji cha Madesa wakati wa kupiga kampeni za Ubunge.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahtubia wakazi wa kitongoji cha Madesa wakati wa kupiga kampeni za Ubunge ambapo aliwaambia uongozi si kitu cha kujaribiwa hivyo wananchi wakapige kura kwenye chama kilichokuwa na uzoefu wa siasa na maendeleo kwa jumla.
Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Kihangaiko wakati wa kampeni za kumnadi mgombea wa CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete.
Kikundi cha Upendo kikitumbuiza wakati wa mkutano wa kampeni za CCM

"WATOTO WAWILI FAMILIA MOJA WATEKETEA KWA MOTO-TABORA MJINI"

Miili ya watoto wawili wa familia moja Daniel Paul(8)na mdogo wake Emmanuel Paul(3) ambao wamepoteza maisha baada ya nyumba waliokuwa wakiishi kuteketea kwa moto huku wakiwa wamelala ndani majira ya saa moja asubuhi huko eneo la mtaa wa Rufita Mwanzaroad Tabora mjini.
Chumba ambacho watoto hao walipokuwa wamelala na kuteketea kwa moto ambao chanzo chake inadhaniwa kuwa ni hitilafu za umeme.
Majonzi makubwa kuhusiana na kifo cha watoto hao ambao walikuwa wamelala peke yao ndani
Kamanda wa Polisi wilaya ya Tabora  OCD  Samwel Mwampashe akizungumza na wananchi wakati wa tukio hilo la kusikitisha lililotokea na kupoteza maisha ya watoto hao.
Katikati alijishika kichwani ni Paul Daniel ambaye baba wa watoto hao walipoteza maisha akiangalia maiti za watoto wake hao wawili muda mfupi mara baada ya kufika eneo la tukio ambapo maswali mengi yalizuka baba huyo alikuwa wapi wakati watoto wanateketea kwa moto ndani ya nyumba.
Baadhi ya wananchi wakichungulia dirishani wakiangalia namna watoto walivyoteketea kwa moto
Mkuu wa wilaya ya Tabora Bw.Suleiman Kumchaya alifika eneo la tukio mapema wakati Kikosi cha Zimamoto kikimalizia uzimaji wa moto na kuwatoa watoto hao ambao tayari walikuwa wamekwisha kufa.

Huyu mama na mtoto walisalimika  katika tukio hilo la moto ambao walikuwa kwenye vyumba vingine
Baadhi ya Samani ziliteketea vibaya kwa moto huo.


Monday, March 24, 2014

WAJAWAZITO HATARINI MKOANI KIGOMA

Mkoa wa Kigoma Wastani wa wanawake wajawazito 48 hufariki Kila Mwaka wilayani  kasulu ,kutokana na tatizo la uzazi pingamizi wakati wa kujifungua.
 
Akithibitisha  hilo Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali ya wilaya ya Kasulu Mageni Mpondamali alisema sababu hiyo inachangiwa na ukosefu wa vifaa na dawa za kutosha katika vituo vya Afya na hospitali zilizopo wilayani humo.
 
“ pamoja na baadhi ya akina mama wajawazito kuchelewa kufika katika vituo vya afya na hosptali jambo ambalo linasababisha wanawake hao wanapofika katika vituo hivyo kuwa na hali mbaya ambayo inahatarisha usalama wa maisha yao” alisema Mpondamali.
 
Aidha amesema kuwa licha ya kuwahimizi kufika maeneo ya kupatia huduma muhimu pamoja na kujifungua bado jamii imekuwa na tabia ya kuendekeza mila na desturi na hivyo wengine kujifungulia kwa wakungawa Jadi.
 
 
Alisema kuwa tatizo hilo katika wilaya ya kasulu imekuwa ikiongezeka kila kukicha licha ya kuwapatia elimu mbalimbali akinamama hao pamoja na wakunga wanaowazalisha kuwapatia elimu ili wakipata mama mjamzito wamfikishe katika vituo vya afya na hospitali.
 
 
Akipokea msaada kutoka katika kikundi cha pretty mother cha akinamama wilaya ya Kasulu Afisa Muuguzi katika hosptali ya wilaya ya Kasulu Bi Janet Gabriel   ametoa shukrani kwa kikundi hicho ambapo ameeleza kuwa itasaidia kupunguza matatizo mbalimbali yanayojitokeza katika hospitali hiyo.
 
Amesema kuwa sambamba na hilo bado kunatatizo la  elimu ya uzazi salama kwa akinamama wajawazito na wenzawao kutohudhuria kliniki pamoja na wengine kuamini tiba mbadala za asili ambapo ni miongoni mwa sababu zinazochangia kuongezeka kwa vifo hivyo.
 
Akikabidhi msaada huo mwenyekiti wa kikundi hicho bi Edita Nsila amesema kuwa lengo la kikundi ni kuisaidia jamii iliyopo katika Makundi maalumu yakiwemo ya walemavu, wagonjwa, na watu wengine wenye mahitaji maalum.

Sunday, March 23, 2014

"KASEJA AMPENDA MTOTO TABORA"

Goli kipa maarufu nchini Juma Kaseja aliamua kupiga picha na mshabiki wa Yanga wakati mchezo kati ya Rhino na Yanga ambapo Rhino alipata kichapo cha bao tatu kwa sifuli katika uwanja wa Aly Hassan Mwinyi mjini Tabora.

LHRC YAZINDUA KAMPENI YA UELEWA WA RASIMU YA PILI YA KATIBA KANDA YA MAGHARIBI.

Na Magreth  Magosso, Kigoma


Mkuu wa wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma ataka  Wamiliki wa Vyombo vya Habari na Wandishi wa habari nchini wasitumike kuandika habari zenye kuligawa Taifa,badala yake wandike habari zenye uhalisia mzima wa mchakato wa katiba unaoendelea Bungeni Mjini Dodoma.


Akithibitisha kauli hiyo  Mgeni rasmi Khadija Nyembo jana kigoma ujiji kwenye uzinduzi wa kampeni kwa kanda Magharibi ya Azaki ya kusambaza uelewa wa Rasimu ya pili ya katiba ya Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania kwa lengo la kunyambulisha  ibara na vifungu vya sheria  katika rasimu hiyo katika wilaya sita za kigoma ,Uvinza ,Kakonko ,Kibondo na Kasulu katika kata tatu kwa kila wilaya hizo


“yaliyomo kwenye rasimu ya katiba ni chanzo na chachu ya utawala wa serikali kuwajibika kwa raia wake,itumieni vyema mijadala hiyo ili kubaini maslai yenu kwa kizazi cha leo na kesho,jitokezeni katika kata teule” alisema Nyembo.


Kwa upande wa Kaimu Mwenyekiti wa Kituo cha Sheria na haki za Binadamu Ezekieli Massanja (LHRC) alisema dhima ya kuwaelimisha wananchi wabaini mapungufu yaliyopo kwenye rasimu kwenye makundi maalum,vijana,watoto na wanawake ili sheria zibainishe  na watawala wawajibike  kutatua changamoto za wanannchi.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi  wa hapo Sofia Patriki na Rasdida Ramadhani walisema kuwa katika katiba hiyo iainishwe sheria maalumu ya umiliki wa miradhi kwa wanawake wajane ambao wananyimwa haki zao,  sanjari na kutungwa sheria ambayo itatoa adhabu kwa wale wenye tabia ya kushiriki tendo ya ndoa ya jinsia moja jambo ambalo ni kinyume cha utaratibu wa mila na desturi za Kitanzania.

Aidha Kashindi Maulidi alisema kuwa miongoni mwa mambo ya kuzingatiwa ni pamoja na umiliki wa ardhi kwa wananchi ili iwe na manufaa kwao, pamoja na kuongeza kifungu cha wananchi kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii jambo litakalo wawezesha kupata pesheni ya uzee na wao waweze kumudu hali ya maisha.  

"MIMI NA CHAMA CHANGU CHA CCM,NITAFIA HUKU HUKU!!!

Mmoja kati ya wakereketwa wa Chama cha Mapinduzi kata ya Isevya manispaa ya Tabora akionesha uzalendo kwa Chama chake.

Friday, March 21, 2014

BILIONI 5 ZAPOTEA KIGOMA

Na Magreth Magosso,Kigoma.
 
IMEFAHAMIKA kuwa,Mradi wa Mtandao wa maji unaojengwa katika Manispaa ya Kigoma Ujiji huenda usiwe na tija kwa wananchi wa hapo,endapo serikali haitawapa fidia  ya fedha mapema  kaya zitakazoathiriwa na mradi huo.
 
Mradi umetengewa  sh. Bilioni 32 ,kwa ufadhili wa jumuiya ya ulaya,serikali ya ujerumani (KFW)na serikali ya nchi hii, katika ujenzi wa matanki ya maji eneo la vamia,mlole,gungu,mji mwema,mnarani,kigoma sekondari sambamba na usambazaji wa mabomba makuu kwa urefu wa km16.9 na ya usambazaji maji km 122.8 .
 
Akifafanua hilo kwenye madhimisho ya kilele cha wiki ya maji  kigoma ujiji,Mkurugenzi wa KUWASA Josephat  Rwegasira alisema serikali ikiondoa changamoto ya fidia kwa wahanga wa mradi  mapema kwa lengo la mkandarasi afanye kazi  kwa wakati ,ili ifikapo machi ,17,2015 akabidhi mradi kwa wahusika kwa mujibu wa mkataba wa mkandarasi ‘Specon service Ltd .
 
Kwa upande wa Mgeni rasmi ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa kigoma Eng.John Ndunguru alisema pamoja na hilo mamlaka inawajibu wa kutoa huduma bora kwa wadau wake ili kuondoa dhulma dhidi ya wananchi husika.
 
“madiwani ,wananchi wanadai huduma mbovu ya maji na mnawatoza sh.20,000 kwa mwezi, maji kutoka mara mbili kwa mwezi dhulma zaidi hawana kisoma maji(meter)sasa mwishoni mwa machi nisisikie kaya hazina mita” alibainisha Eng.Ndunguru.
 
Aliongeza kwa kusema kuwa, amegundua KUWASA haishirikishi vya kutosha wandishi wa habari ,hali inayochangia jamii kukosa  taarifa muhimu, kutoka kwa mamlaka  sanjari na mikakati yao  ili kuondoa dhana hasi kwa wadau dhidi yao.
 
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wa kigoma ujiji Mariamu Issa na Sophia Steven  walisema , madhimisho ya wiki ya maji haina tija, kutokana na adha ya upatikanaji wa maji na kuishauri mamlaka kuwa madhimisho yawe wazi ili kubaini changamoto baina yao.