Na Magreth Magosso,Kigoma.
IMEFAHAMIKA kuwa,Mradi wa Mtandao wa maji unaojengwa katika
Manispaa ya Kigoma Ujiji huenda usiwe na
tija kwa wananchi wa hapo,endapo serikali haitawapa fidia ya fedha mapema kaya zitakazoathiriwa na mradi huo.
Mradi umetengewa sh. Bilioni
32 ,kwa ufadhili wa jumuiya ya ulaya,serikali ya ujerumani (KFW)na serikali ya
nchi hii, katika ujenzi wa matanki ya maji eneo la vamia,mlole,gungu,mji
mwema,mnarani,kigoma sekondari sambamba na usambazaji wa mabomba makuu kwa
urefu wa km16.9 na ya usambazaji maji km 122.8 .
Akifafanua hilo kwenye madhimisho ya kilele cha wiki ya maji kigoma ujiji,Mkurugenzi wa KUWASA Josephat Rwegasira alisema serikali ikiondoa changamoto
ya fidia kwa wahanga wa mradi mapema kwa
lengo la mkandarasi afanye kazi kwa
wakati ,ili ifikapo machi ,17,2015 akabidhi mradi kwa wahusika kwa mujibu wa
mkataba wa mkandarasi ‘Specon service Ltd .
Kwa upande wa Mgeni rasmi ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa
kigoma Eng.John Ndunguru alisema pamoja na hilo mamlaka inawajibu wa kutoa
huduma bora kwa wadau wake ili kuondoa dhulma dhidi ya wananchi husika.
“madiwani ,wananchi wanadai huduma mbovu ya maji na mnawatoza
sh.20,000 kwa mwezi, maji kutoka mara mbili kwa mwezi dhulma zaidi hawana
kisoma maji(meter)sasa mwishoni mwa machi nisisikie kaya hazina mita”
alibainisha Eng.Ndunguru.
Aliongeza kwa kusema kuwa, amegundua KUWASA haishirikishi vya
kutosha wandishi wa habari ,hali inayochangia jamii kukosa taarifa muhimu, kutoka kwa mamlaka sanjari na mikakati yao ili kuondoa dhana hasi kwa wadau dhidi yao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wa kigoma ujiji
Mariamu Issa na Sophia Steven walisema ,
madhimisho ya wiki ya maji haina tija, kutokana na adha ya upatikanaji wa maji
na kuishauri mamlaka kuwa madhimisho yawe wazi ili kubaini changamoto baina
yao.
No comments:
Post a Comment