Pages

KAPIPI TV

Sunday, March 23, 2014

LHRC YAZINDUA KAMPENI YA UELEWA WA RASIMU YA PILI YA KATIBA KANDA YA MAGHARIBI.

Na Magreth  Magosso, Kigoma


Mkuu wa wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma ataka  Wamiliki wa Vyombo vya Habari na Wandishi wa habari nchini wasitumike kuandika habari zenye kuligawa Taifa,badala yake wandike habari zenye uhalisia mzima wa mchakato wa katiba unaoendelea Bungeni Mjini Dodoma.


Akithibitisha kauli hiyo  Mgeni rasmi Khadija Nyembo jana kigoma ujiji kwenye uzinduzi wa kampeni kwa kanda Magharibi ya Azaki ya kusambaza uelewa wa Rasimu ya pili ya katiba ya Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania kwa lengo la kunyambulisha  ibara na vifungu vya sheria  katika rasimu hiyo katika wilaya sita za kigoma ,Uvinza ,Kakonko ,Kibondo na Kasulu katika kata tatu kwa kila wilaya hizo


“yaliyomo kwenye rasimu ya katiba ni chanzo na chachu ya utawala wa serikali kuwajibika kwa raia wake,itumieni vyema mijadala hiyo ili kubaini maslai yenu kwa kizazi cha leo na kesho,jitokezeni katika kata teule” alisema Nyembo.


Kwa upande wa Kaimu Mwenyekiti wa Kituo cha Sheria na haki za Binadamu Ezekieli Massanja (LHRC) alisema dhima ya kuwaelimisha wananchi wabaini mapungufu yaliyopo kwenye rasimu kwenye makundi maalum,vijana,watoto na wanawake ili sheria zibainishe  na watawala wawajibike  kutatua changamoto za wanannchi.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi  wa hapo Sofia Patriki na Rasdida Ramadhani walisema kuwa katika katiba hiyo iainishwe sheria maalumu ya umiliki wa miradhi kwa wanawake wajane ambao wananyimwa haki zao,  sanjari na kutungwa sheria ambayo itatoa adhabu kwa wale wenye tabia ya kushiriki tendo ya ndoa ya jinsia moja jambo ambalo ni kinyume cha utaratibu wa mila na desturi za Kitanzania.

Aidha Kashindi Maulidi alisema kuwa miongoni mwa mambo ya kuzingatiwa ni pamoja na umiliki wa ardhi kwa wananchi ili iwe na manufaa kwao, pamoja na kuongeza kifungu cha wananchi kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii jambo litakalo wawezesha kupata pesheni ya uzee na wao waweze kumudu hali ya maisha.  

No comments: