TUME iliyoundwa na
Mkuu wa Mkoa Kigoma Luten kanali Mstaafu Issa Machibya kufuatilia zana za uvuvi
zilizoibiwa na kupelekwa nchi ya kidemocrasia ya Congo haijafanikiwa kurudi na
zana hizo kutokana na kuwepo kwa utata baina ya viongozi wa serikali hiyo.
Akizungumzia hilo mwakilishi wa wavivu Salumu Shabani ambaye
alikuwa katika tume hiyo alisema kuwa jitihada za mkuu wa mkoa wa kigoma
ni kubwa lakini kutokana na mfumo uliopo katika nchi ya Congo imekuwa ngumu
kuweze kutimiza yale ambayo analenga kuwasaidia wavuvi mkoani hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana kigoma ujiji, Shabani alisema licha ya kuwepo kwa mikataba
ya ujirani mwema baina ya nchi hizo kwa lengo la kuwepo na mahusiano baina yao na
viongozi kuhakikisha zana zinazoibiwa na kupatikana katika nchi hizo zirudishwe
bila masharti magumu wala urasimu wowote bado mkataba wa ujirani mwema unakiukwa na n
chi hiyo.
Aidha mara
kadhaa uongozi wa mkoa wa kigoma umekuwa ukituma wawakilishi kufuatilia zana hizo
bila mafanikio ambapo fedha za serikali zimekuwa zikitumika kuhakikisha wavuvi
wanapatiwa zana zao na wanafanya shughuli za uvuvi kwa amani na utulivu katika
ziwa Tanganyika.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Mwenyekiti wa wavuvi Ramadhani
Kanyongo na Makamu wake Sendwe Ibrahimu walisema kuwa hadi ifikapo 2025 uvuvi
wa mkoa wa Kigoma utakuwa ni ule wa kusonza kwa mitubwi na sio uvuvi uliopo
kipindi hiki sambamba na mapato ya mkoa na Halmashauri kuporomoka kwa kasi na
uchumi kushuka.
Walisema kuwa kutokana na kukidhiri kwa wizi katika mwambao wa
ziwa Tanganyika bei ya mazao ya samaki na dagaa imepanda kutokana na wavuvi na
wamiliki kuhofia kuingiza vyombo vyao ziwani na wavuvi kuhofia usalama wa
maisha yao.
Walisema kuwa awali mwaka 2003 kulikuwa na mitubwi 168 katika
mwalo wa kibirizi ambapo kwa sasa imebaki 45, huku mwalo wa katonga kulikuwa na
mitumbwi 200 na sasa ipo 168 hali inayokatisha tama kuendelea kufanya shughuli
za uvuvi katika ziwa hilo.
Hivi karibuni
Mkuu wa mkoa akizungumza na wavuvi alisema kwa kushirikiana na wananchi, wavuvi
na vyombo vya ulinzi na usalama tatizo hilo litapatiwa ufumbuzi ikiwa ni pamoja
na kuendesha msako wa kuwakamata wahamiaji wanaoishi kinyume cha sheria na
kuwarudisha katika nchi zao.
Akijibia hilo ubalozi mdogo wa Nchi ya Congo Kigoma Balozi Riky
Molema akiri mfumo wa uendeshaji wa serikali ya Tanzania na
serikali ya Congo uko tofauti na hivyo kuwa vigumu kupata zana hizo kwa wakati
muafaka na kuwataka wavuvi kuwa wavumilivu .
Alisema kuwa ili kuondoa tatizo la wizi katika mwambao wa
ziwa ni lazima dhati ya kuthubutu kwa viongozi husika wa serikali zote mbili kuunda ulinzi shirikisha ndani ya ziwa hilo
kwa kufanya doria ya pamoja na kuhakikisha wimbi la wizi katika ziwa hilo
unatokomea.
No comments:
Post a Comment