Mkoa wa Kigoma Wastani wa wanawake wajawazito 48 hufariki Kila
Mwaka wilayani kasulu ,kutokana na tatizo
la uzazi pingamizi wakati wa kujifungua.
Akithibitisha hilo
Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali ya wilaya ya Kasulu Mageni Mpondamali alisema
sababu hiyo inachangiwa na ukosefu wa vifaa na dawa za kutosha katika vituo vya
Afya na hospitali zilizopo wilayani humo.
“ pamoja na baadhi ya akina mama wajawazito kuchelewa kufika katika
vituo vya afya na hosptali jambo ambalo linasababisha wanawake hao wanapofika
katika vituo hivyo kuwa na hali mbaya ambayo inahatarisha usalama wa maisha yao”
alisema Mpondamali.
Aidha amesema kuwa licha ya kuwahimizi kufika maeneo ya
kupatia huduma muhimu pamoja na kujifungua bado jamii imekuwa na tabia ya
kuendekeza mila na desturi na hivyo wengine kujifungulia kwa wakungawa Jadi.
Alisema kuwa tatizo hilo katika wilaya ya kasulu imekuwa
ikiongezeka kila kukicha licha ya kuwapatia elimu mbalimbali akinamama hao
pamoja na wakunga wanaowazalisha kuwapatia elimu ili wakipata mama mjamzito
wamfikishe katika vituo vya afya na hospitali.
Akipokea msaada kutoka katika kikundi cha pretty mother cha
akinamama wilaya ya Kasulu Afisa Muuguzi katika hosptali ya wilaya ya Kasulu Bi
Janet Gabriel ametoa shukrani kwa kikundi hicho ambapo ameeleza
kuwa itasaidia kupunguza matatizo mbalimbali yanayojitokeza katika hospitali hiyo.
Amesema kuwa sambamba na hilo bado kunatatizo la elimu ya uzazi salama kwa akinamama wajawazito
na wenzawao kutohudhuria kliniki pamoja na wengine kuamini tiba mbadala za asili
ambapo ni miongoni mwa sababu zinazochangia kuongezeka kwa vifo hivyo.
Akikabidhi msaada huo mwenyekiti wa kikundi hicho bi Edita Nsila
amesema kuwa lengo la kikundi ni kuisaidia jamii iliyopo katika Makundi maalumu
yakiwemo ya walemavu, wagonjwa, na watu wengine wenye mahitaji maalum.
No comments:
Post a Comment