Mwenyekiti
wa klabu ya waandishi wa habari (Singpress) mkoa wa Singida, Seif
Takaza akifungua mkutano mkuu wa kawaida wa klabu hiyo uliofanyika mjini
Manyoni mwishoni mwa wiki.Kulia ni makamu mwenyekiti Damiano Mkumbo na
kulia ni kaimu katibu mtendaji,Emmanuel Michael.(Picha na Nathaniel
Limu).
Baadhi
ya wanachama wa klabu ya waandishi wa habari (Singpress) mkoa wa
Singida,wakifuatilia mkutano mkuu wa kawaida wa (mwaka 2013) klabu hiyo
uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kanisa Katoliki mjini Manyoni.
Na Nathaniel Limu, Manyoni
KLABU
ya waandishi wa habari (Singpress) mkoa wa Singida imemchagua kwa
kishindo Pascal Tantau (32),kuwa katibu wake mtendaji kuziba nafasi
iliyoachwa wazi na Abby Nkungu ambaye anadai kwa sasa afya yake ina
mgogoro.
Pascal kijana aliyemaliza chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) alipata kura 15 za ndio,mbili zilimkataa na moja iliharibika.
Pascal atakuwa madarakani hadi mwishoni mwakwani (2015) uchaguzi mkuu utakapofanyika kwa mujibu wa katiba ya klabu hiyo.
Pascal
aliwashukuru wanachama wenzake kwa kumwamini na kumkabidhi nafasi hiyo
nyeti. Ameahidi kwamba atawatumikia kwa nguvu zake zote na kwa maarifa
lengo kuu ikiwa ni klabu hiyo iweze kupaa kimaendeleo katika kipindi
chake cha uongozi.
“Niwaahidi
pia kwamba katika uongozi wangu nitatumia mbinu shirikishi ili kila
mwananchama aweze kutoa mchango wake mbalimbali kuendeleza klabu na
kuboresha ustawi wa wananchama.Nitajitahidipia kuhakikisha klabu inakuwa
na mahusiano mazuri na wadau wake mbalimbali”, alisema kwa kujiamini.
Abby
Nkungu amelazimika kujiuzulu nafasi ya ukatibu mtendaji wa
Singpress,kwa madai kwamba ameagizwa na daktari wake aishiye nchini
Kenya, kuwa asifanye kazi yo yote ambayo atalazimika kutumia akili
nyingi.
Ilielezwa
mbele ya mkutano huo mkuu, kwamba Nkungu aliweza kuombwa na kamati
tendaji kusaidia kuandaa maandalizi ya mkutano mkuu,alikataa kata kata.
Hata
alipoitwa tena na kamati tendaji ili aweze kufafanua zaidi juu kutakiwa
na daktari wake awe kwenye mapumziko yasiyo na bughudha yo yote…yaani
‘total rest’,wakati anaendelea na kazi kama kawaida zikiwemo za safari
ndefu pia alitupilia mbali wito huo.
Kutokana
na hali hiyo mkutano mkuu huo umeazimia Nkungu asigombee tena uongozi
wowote katika klabu ya Singpress kwa muda wote wa maisha yake
yaliyobaki.Pia amesimamishwa uanachama kwa kipindi cha miezi tisa.
Hii ni mara ya pili,Nkungu kusimamishwa uanachama wa klabu ya Singpress.
No comments:
Post a Comment