Pages

KAPIPI TV

Saturday, March 29, 2014

MWALIMU AMVUNJA MGUU DENTI KISA MAPENZI - KIGOMA


Na Magreth Magosso,Kigoma

Mwanafunzi wa Darasa la saba katika Shule ya Msingi Bangwe Kata ya Bangwe kwenye Manispaa ya kigoma Ujiji mkoani hapo  amepigwa na mwalimu wake katika maeneo mbalimbali ya mwili wake na kumvunja mguu wa kulia baada ya kumkatalia kumpa penzi.


Akizungumza na mwandishi wetu  jana wodi namba 5 katika hospitali ya Rufaa ya Maweni mwanafunzi huyo aliyetambuliwa kwa jina la Zubeda Athuman (14)  alisema chanzo cha mwalimu huyo kumchukia na hatimaye kufikia hatua ya kumpiga na kumvunja mguu  ni wivu wa kukataliwa kupewa penzi ,hali iliyomfanya mwalimu huyo kumpa  adhabu za hapa na pale kila aendapo shule.


Hali hiyo ilimfanya  mwanafunzi huyo kuwadokeza wazazi wake ambapo walimwambia avumilie,ndipo jumatano ya wiki hii mwalimu alimpa adhabu ya kuchimba shimo na alikataa kufanya hivyo baada ya kuona hana kosa la msingi la kumpa adhabu hiyo.


Mwalimu huyo alifikia hatua ya kumfuata nyumbani kwao  machi,22,2014 saa 12.30 jioni hali iliyowashtua wazazi na kumuhoji mtoto juu ya hilo ndipo binti alipokwenda shule Machi,24,2014  alimuliza mwalimu huyo sababu ya kumfuta kwao, hali hiyo ilimchefua mwalimu na kutoa maneno ya kashfa  na kumpiga  vibao vya uso na kusababisha maumivu mbalimbali ya mwili wake ikiwemo kuvunjika kwa mguu.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Maweni Macris Yakayeshi akiri mwanafunzi huyo kuvunjika mguu wa kulia sambamba na kuvimba uso na kupelekea mdomo kwenda upande na wiki ijayo anatarajia kumwekea `P.O.P’.


Dr.Yakayeshi alibainisha kuwa kutokana na tatizo alilonalo itamlazimu kukaa na mhogo si chini ya wiki sita ili mguu utengamae sambamba na kuitaka jamii ibadilike na matukio ya udhalilishaji wa kijijnsia huku akidai alifikishwa hapo kifua kikiwa wazi ili hali binti ni rika la balehe na kuomba sheria ichukue mkondo wake.


Mwenyekiti wa Mtaa wa Kamala katani humo Curthbert Kusongwa alisema, kwa maelezo aliyoyapata kutoka kwa walimu wa shule hiyo walidai binti alikataa adhabu aliyopewa na kumpiga kofi mwalimu na ndipo mwalimu akamwambia akamlete mzazi wake,wazazi walipofika alidai alimvamia mwalimu na kuanza kumpiga hali iliyolazimu jeshi la polisi kuingilia  hekaheka kiyo.


Akizungumzia tukio hilo Athumani Moshi ambaye ni baba wa Zubeda alisema  alishangaa kumuona mwanae amerudishwa shule huku akiwa amevimba uso na mdomo ndipo akadai kuitwa na mwalimu husika,alipofika shule na kuonana na mwalimu husika hakuwa muungwana kutokana na kauli chafu na kebehi.


Moshi alisema baada ya kauli hizo  ghafla mwalimu akamkata mtama mwanae na kuanguka chini ndipo wakapigana,huku akikiri awali alipata kuelezwa juu ya adha ya mwalimu huyo kwa binti yake hadi kufikia hatua ya kumfuata usiku siku za mapumziko sanjari na kumpa adhabu zisizostahili kwa kisa alikataa kuwa nae kimapenzi.


Kamanda wa Polisi mkoani hapa Zedekia Makunja alipoulizwa kama analifahamu hili akadai naam ila wataitwa machi,31,mwaka huu.


Kwa nyakati tofauti Mariamu Issa na Winyfrida Bwire walisema sheria ya mwanafunzi juu ya adhabu inajulikana ,walimu hawana budi kulea watoto kwa kuwafundisha adabu ,huku wakidai kuna namna kati ya mwanafunzi na mwalimu haiwezekani kukataa kwa adhabu amvunje mguu.

No comments: