Pages

KAPIPI TV

Sunday, October 26, 2014

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU UKATAJI WA MITI NCHINI HATA KAMA IKIWA MTU AMEPANDA NYUMBANI KWAKE


MISITU NA MALIASILI TANZANIAWaziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akimsalimia mmoja wa wagonwa waliofuata huduma katikazahanati ya Ngarenanyuki wilayani Arumeru ,juzi  alipoitembelea baada ya Mbunge wa jimbo hilo kumlalamikia kuhusu tozo ya ushuru wa magari na wagionjwa wanaopita katik Hifadhi ya Taifa ta Arusha ili kupata huduma katika hospitali hiyo. Waziri Nyalandu aliamuru wananchi wanaohitaji kupata tiba katika zahanati hiyo kupita bure hifadhini. unnamed1Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akimtaarifu Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu juu ya adha wanayopata wananchi wa jimbo klake wakati wakiiingia katika Zahanati ya tiba za Asili cha Ngarenanyuki mkoani Arusha juzi , kutokana  na tozo la pesa kupitia hifadhi ya Taifa ya Arusha. Waziri Nyalandu aliamuru wananchi wanaohitaji kupata tiba katika zahanati hiyo kupita bure hifadhini. unnamed2Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiwa na Mbunge wa Siha ambaye ni Naibu waziri wa Serikali za Mitaa, Aggrey Mwanri wakikagua kitalu cha miti katika shamba la mitiulioko wilayani humo juzi. Waziri Nyalandu aliruhusu nguzo nza umeme kupita katika msitu huo ili kuwezesha wananchi wa wilaya hiyo kupata umeme n akuondoa mgogoro uliozuia mradi huo kwa muda mrefu.
unnamed3Naibu waziri wa Serikali za Mitaa, Aggrey Mwanri akiwa na wataalamu na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu wakikagua msitu wa Siha mkoani Kilimanjaoro alipotembelea juzi . Waziri Nyalandu aliruhusu nguzo nza umeme kupita katika msitu huo ili kuwezesha wananchi wa wilaya hiyo kupata umeme.
……………………………………………………………..
Serikali imepiga marufuku ukataji wa miti nchini hata kama ikiwa mtu amepanda nyumbani kwake anatakiwa kuomba kibali kwajili ya kukata mti huo.

Akizungumza wilayani Siha juzi ,Waziri wa Maliasili na Utalii , Lazaro Nyalandu amesema kwamba Tanzania inawez a kuwa jangwa baada ya miaka 15 kutokana na uvunaji mbaya wa bidhaa za miti unaofanyika nchini .

“Tukiendelea kukata miti kma hivi tutakuwa tunatengeneza janga la kitaifa kwa hiyo kwa sasa naomba niseme rasmi kuwa hakuna mtu anaruhusiwa kukata miti au mti hata kama ameupanda nyumbani kwake, ni lazima aombe kibali kwa maafisa wa misitu. Tunatakiwa kushiriki kwa pamoja katika kutunza mazingira yetu” alisema

Nyalandu alisema kasi ya ukataji miti nchini imekuwa kuubwa kwa sasa kutokana na kuongezeka kw aidadi ya watu na kuwa kwa mwaka mmoja pekee hekta 350,000 hukatwa huku kikiwa hakuna jitihada za kurejesha iliyoondolewa.

“Kwa kaddri siku zinavyozidi kwenda na watu kuongezeka baada ya miaka kumi misitu itakuwa inavunwa kw azaidi ya hekta 850,000 nchini kwa mwaka, hii ni hatari kubwa, lazima tufanye jitihada zaidi kukomesha tatizo hili”.

Aliwaagiza wakuu wa wilaya za Arusha na kilimanjaro kuunda timu ili kuandaa  hadidu za rejea kwa ajili ya kupatia kikosi kazi ambacho kitaandaas andiko kw ajili ya kuanzisha mfuko huo.

Mtendaji Mkuu wa wakala wa misditu (TFS) Juma Mgoo alisema kwamba misitu ilianza kutunzwa mtokea enzi za wakoloni lakini tatizio kubwa linalotokea kw asasa ni watu wengi kuivamia kutokana na mahitaji ya nishati na uchomaji wa misitu.

Alisema kwamba kwa msitu wa asili kawaida huwa na mita 30 za ujazo wakati kwa upande wa misitu ya kuoandwea huwa wna ujazo wa zaidi ya mira za ujazo 400 hadi 600 kitu ambacho alishauri  umuhimu w akupanda miti zaidi ili iweze kukabiliana na ongezeko la mahitaji na kuokoa misitu iliyopo.

Waziri Nyalandu alitoa maagizo ya kuruhusu nguzio za umeme kupita katika msitu wa wilayani Siha ili kufanywa wananchi waweze kupata nishati ya umeme ili kuokoa matumizi ya kuni kama nishati na kulinda misitu.

“Umemem ni nishati mbadala badala ya kuni na mkaa kwa hiyo napenda kuwaeleza kwamba ni bora miti michache ikatwe ili pupisha nguzi za umeme ili wananchi wakipata nishati hiyo waache kutumia kuni na kuharibu misitu na kutumia umeme kama nishati mbadala” alisema.

MBWEMBWE ZA STAND UNITED

STAND UNITED YA SHINYANGA
Stand United wakiingia uwanjani na katapila tayari kucheza na Yanga, mwenye shati la kitenge hapo mlagoni ni Mbunge wa Shinyanga mjini Mheshimiwa Stephen Masele ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini amekuwa bega kwa bega na timu ya Stand United.

MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA KICHWA KIKUBWA NA MGONGO WAZI DUNIANI YAFANYIKA JIJINI DAR-ES-SALAAM


MTOTO WA KICHWA KIKUBWAMkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dkt. Othmani Kiloloma akiwaeleza waandishi wa habari(hawapo pichani) majukumu wanayotekeleza katika kuhakikisha wanakabiliana na tatizo la Mgongo wazi na Vichwa vikubwa ikiwamo kutoa elimu bora kwa madaktari wanaosomea somo hilo, kwenda mikoani kutoa tiba kwa watoto wenye matatizo hayo,wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na na Mgongo wazi duniani  Jijini Dar es salaam. Kushoto ni mwenyekiti wa chama cha wazazi wenye watoto wa kichwa kikubwa na mgongo wazi(ASBHAT) Bw. Abdulhakim Bayakub.PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
3Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dkt. Othmani Kiloloma akimkabidhi Mama Dorcas Membe kitabu cha Mpango shirikishi wa Mtoto wa kichwa kikubwa na Mgongo Wazi jana na kumuomba kuwa Mlezi wa chama cha Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) ambapo ameahidi kushirikiana na chama hicho katika harakati za kukabiliana na Tatizo la Kichwa Kikubwa na Mgongo wazi. kulia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Abdulhakim Bayakub.
4Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Bw. Abdulhakim Bayakub akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dkt. Othmani Kiloloma cheti shukrani kwa mchango wanaoendelea kuutoa cha chama hicho ikiwamo kutoa matibabu kwa Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi.
6Baadhi ya wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi waliojitokeza katika sherehe hizo za Maadhimisho ya ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na na Mgongo wazi duniani yaliyofanyika Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) leo Jijini Dar es Salaam. 6BBaadhi ya wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi waliojitokeza katika sherehe hizo za Maadhimisho ya ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na na Mgongo wazi duniani yaliyofanyika Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) jana Jijini Dar es Salaam. 7Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Bi. Germana Gasper akitoa maaelezo kwa wananchi waliojitokeza katika banda wakati wa sherehe na kuwaasa wazazi hasa wakike waliokatika umri wa kubeba mimba kutumia vyakula vyenye vitamin ya Foliki kama maembe, Mchicha, Mihogo,machungwa, maharage, mahindi,mayai, ndizi, parachichi, papai, maini na kabichi, ili kukabiliana na tatizo la Kichwa kikubwa na Mgongo wazi kwa watoto wanaozaliwa
10Mlezi wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Mama Dorcas Membe, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dkt. Othmani Kiloloma(Kulia), Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Bw. Abdulhakim Bayakub(mwenye T-shirt nyeupe) na Moja ya mtoto mwenye tatizo la Kichwa Kikubwa wakikata keki katika sherehe za Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na Mgongo wazi duniani jana Jijini Dar es salaam.
11Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dkt. Othmani Kiloloma akimlisha keki Moja ya mtoto mwenye tatizo la Kichwa Kikubwa wakikata keki katika sherehe za Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na Mgongo wazi duniani jana Jijini Dar es salaam.
12Mlezi wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Mama Dorcas Membe akimlisha keki Moja ya mtoto mwenye tatizo la Kichwa Kikubwa wakikata keki katika sherehe za Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na Mgongo wazi duniani jana Jijini Dar es salaam
13Mlezi wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Mama Dorcas Membe akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Bw. Abdulhakim Bayakub.
14Mlezi wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Mama Dorcas Membe akiwapa msaada kinamama wenye watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi.
15 16

MAJAMBAZI WAFANYA UHALIFU ZIWA TANGANYIKA....KIGOMA,

MAJAMBAZI ZIWA TANGANYIKA
Na Magreth  Magosso,Kigoma

Watu watatu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wakiwa  na silaha tano za moto wamefanya uhalifu katika ziwa Tanganyika Mkoa wa Kigoma,( leo) na kupora injini mbili za Mitumbwi ,solar na Betri zenye thamani  ya zaidi ya   sh. milioni 2.8.
 
Akielezea  tukio hilo Katibu wa Wavuvi  mkoani  Kigoma  Mohamed Kasambwe alisema  mnamo Octoba ,26,mwaka huu  majira  ya saa 6.00 usiku ,mwalo wa Kalalangabo  kaskazini  mwa wilaya ya kigoma  wavuvi walivamiwa na majambazi  hao na kuiba vitu mbalimbali.

“ mtumbwi wao ulikuwa namba 15 HP,  usaliti miongoni mwetu na walikuwa wakiongea kibembe shida ipo katika idara ya polisi,uhamiaji na wamiliki wa mitumbwi miongoni mwetu  chachu ya kushindwa kuthibiti uhalifu ziwani” alisema Mohamed.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa mwalo wa Kibirizi Sendwe Ibrahimu alishauri serikali iweke ulinzi wa jeshi la wananchi  JWTZ katika maeneo tete hasa kijiji cha Kazinga ambapo wahalifu hutumia mwalo kujificha.

Alisema kwa upande wa Lubengela wahalifu wanaogopa kutumia mwalo huo kutokana na ulinzi kuimarishwa hatimaye kutumia vijiji vilivyopo kata ya Kagongo Jimbo la kigoma Kaskazini.

Waathirika wa tukio hilo Kasia Hamimu na Juma Mtusi kwa nyakati tofauti wamekili kuibiwa injini ,mafuta ya petrol lita 50 na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya  sh.milioni 3 .

Mdau wa uvuvi  Salum  Shaban alisema  wavuvi walifika umbali wa mita 20 kutoka mwalo kalalangabo ,majambazi walivamia wavuvi Huku akishauri kuwepo na operesheni shirikishi  ya wadau husika ili kutokomeza uvamizi ziwani.

Kamanda  wa Polisi  mkoa wa Kigoma Jafari Mohamed alipoulizwa  kuhusu hilo tukio  hilo ,alisema yupo katika shughuli ya kusimikwa kwa askofu  wa kanisa  Katoliki na atalijibia baada ya sherehe hiyo kumalizika.

Saturday, October 25, 2014

MKE WA RAIS WA CHINA AIPA MSAADA SHULE YA SEKONDARI YA WAMA-NAKAYA


IMG_4094

Na Anna Nkinda – Beijing, China Mke wa Rais wa China Mama Peng Liyuan ameahidi kutoa vifaa vya shule vikiwemo vya maabara pamoja na vitabu kwa ajili ya shule ya Sekondari ya WAMA-Nakayama ili  wanafunzi hao waweze kusoma vizuri masomo ya sayansi.
 
Mama Liyuan aliitoa ahadi hiyo  jana wakati akiongea na  mke wa Rais Mama Salma Kikwete katika ukumbi maarufu wa watu (Great hall of the People) uliopo mjini Beijing.

“Nina mapenzi na Taasisi ya  WAMA, nakupongeza kwa kazi unayoifanya ukiwa Mke wa Rais ya kuwainua wanawake kiuchumi na kuwasaidia  watoto wa kike ambao ni yatima na wanaotoka katika mazingira hatarishi ambao nao wanapata elimu sawa na watoto wengine”.

Najua kitaaluma wewe ni mwalimu na unapenda shule mwaka huu nitakuunga  mkono zaidi katika masuala ya shule,  hii itawasaidia wanafunzi kusoma vizuri. Pia nitakuwa na ushirikiano  endelevu na Taasisi ya WAMA”, alisema Mama Liyuan.

Kwa upande wake Mama Kikwete alishukuru kwa msaada huo na kusema kila kwenye maendeleo changamoto hazikosekani alizitaja changamoto zinazoikabili sekta ya elimu ambazo ni  upungufu wa maabara, kutokuwepo kwa wataalamu wa maabara na walimu wa masomo ya sayansi wa kutosha.

Mama Kikwete  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema  katika upande wa elimu Serikali kwa kushirikiana na wananchi wamejitahidi kujenga shule nyingi za  Sekondari lakini  bado kuna  upungufu wa walimu wa masomo ya  sayansi , kutokuwa na maabara za kutosha, kutokuwa na vifaa vya maabara na  upungufu wa wataalamu wa maabara .

“Ninaomba  kuwe na ubadilishanaji wa ujuzi wa kazi (Exchange Program) kwa walimu wetu wa nchi hizi mbili hii itawasaidia kupata  utaalamu zaidi katika fani zao na kutoa mfano wa wataalamu wa maabara ambao wakija nchini watasaidia kwa kiasi kikubwa kuwafundisha wanafunzi masomo ya sayansi kwa njia ya vitendo”, alisema Mama Kikwete.

Shule hiyo ambayo inamilikiwa na Taasisi ya WAMA wanafunzi  wake ni watoto wa kike  ambao ni yatima na wanaotoka  katika mazingira hatarishi  kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani iko  kijiji cha Nyamisati wilaya ya Rufiji mkoani Pwani.

Hii ni mara ya pili kwa Mama Liyuan kuiunga mkono Taasisi ya WAMA ambapo mwaka 2013 alipotembelea nchini  alitoa Yuan milioni moja  sawasawa na shilingi milioni  250 za kitanzania na mabegi ya shule 100 kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya WAMA-Nakayama na vyerehani 20 kwa ajili ya Umoja wa Vikundi vya WAMA  (UVIMA).

Mama Kikwete  ameambatana na mumewe Rais Prof. Jakaya Mrisho Kikwete nchini China kwa ziara ya kikazi ya siku sita.

DR.SLAA AKIWASILISHA MADA KATIKA MKUTANO ULIOANDALIWA NA TCD


Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Willibrod Slaa akiwasilisha mada juu ya ushiriki wa vyama vya siasa katika mageuzi Afrika katika mkutano wa siku nne wa kubadilishana uzoefu kwa vyama vya siasa ulioandaliwa na kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) na kufadhiliwa na Taasisi ya Demokrasia ya vyama vingi ya Uholanzi (NIMD). Mkutano huo unahudhuriwa na vyama kutoka Malawi, Ghana, Uganda na wenyeji Tanzania na kufanyika Zanzibar

BENKI YA EXIM YASAINI MKATABA WA MWAKA MMOJA NA STAND UNITED FC


unnamed
Mkuu wa matawi wa Benki ya Exim Kanda ya Ziwa, Bw. Justus Mukurasi (wapili kushoto) akibadilishana mkataba na Mwenyekiti wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Stand United, Bw. Amani Vicent (wapili kulia) wakati wa hafla fupi iliyofanyika mkoani Shinyanga jana. Mkataba huo utaiwezesha benki kuidhamini timu hiyo katika ligi kuu ya mpira wa miguu ya Vodacom (VPL) katika msimu wa 2014/2015. Wakishuhudia wa kwanza kushoto ni Meneja Msaidizi Tawi la Shinyanga, Bw. Hatunga Nicodemus na Katibu wa kamati ya Fedha, Bw. Bakari Salum (Wa kwanza kulia). Picha na mpiga picha wetu.  
unnamed3  Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
 
Benki ya Exim imesaini makubaliano ya kuifadhili timu ya mpira wa miguu ya Stand United FC ya mkoani Shinyanga. Hii ni timu ya kwanza kupata ufadhili toka Benki ya Exim. Ufadhili huo wa mwaka mmoja utaisaidia timu hiyo kushiriki katika ligi kuu soka Tanzania bara kwa msimu wa 2014/2015.
 
“Makubaliano haya yanaikutanisha Benki ya Exim na mchezo mkubwa kuliko yote Tanzania,” alisema mkuu wa matawi ya Benki ya Exim kanda ya ziwa, Bw. Justus Mukurasi jana katika hafla fupi iliyofanyika mkoani Shinyanga. Aliongeza kuwa hakuna mchezo wenye watazamaji, wafuatiliaji na mashabiki wengi zaidi nchini kama mpira wa miguu.
 
“Timu ya Stand United inanguvu kubwa ya kuunganisha mashabiki  wa kanda ya ziwa. Hivyo ni jambo stahiki kwa Benki ya Exim kuisaidia timu hii ambayo mashabiki wake ni miongoni mwa wateja wa Benki ya Exim,” alisema Bw. Mukurasi.
 
Mukurasi aliongeza kuwa pande hizo mbili zilifanikiwa kuingia katika makubaliano ambayo yataiwezesha benki hiyo kuifadhili timu ya Stand United toka Ligi Kuu Tanzania bara ilipoanza.
 
“Kwetu sisi udhamini tuliofanya sio tu wa nembo, nbali ni ufadhili wa muda mrefu utakaozinufaisha pande zote mbili,” alisema Mukurasi.
 
”Tunatumai kuwa kila mmoja wetu ataweza kujifunza kutoka kwa mwenzake ili kupata matokeo mazuri kwa pamoja. Exim itasaidia kukuza na kuundeleza mchezo wa soka na hivyo kuiwezesha benki yetu karibu zaidi na wateja wake,” alisema Bw. Mukurasi.
 
Naye, Mwenyekiti wa Stand United FC, Bw. Aman Vicent alisema kuwa timu yake inayofuraha kubwa kuingia katika makubaliano na Benki ya Exim. “Tunadhamiria kuimarisha uhusiano huu ili kuhakikisha timu yetu inafanya vizuri katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu,” alisema Bw. Vicent.
 
“Kwa niaba ya Stand United FC, ningependa kuishukuru Benki ya Exim kwa jitiada zao za kusaidia wachezaji wetu na timu kwa ujumla. Tunafanya kazi kubwa kuhakikisha tunainua vipaji vya wachezaji wetu ili na wao waweze kufika mbali zaidi,” aliongeza Bw. Vicent.

PROFESA TIBAIJUKA AONGOZA MAADHIMISHO YA MIAKA 69 YA UMOJA WA MATAIFA (UN)

 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka,ambaye alimwakilisha Rais Jakaya Kikwete, akihutubia Dar es Salaam, katika Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa kutimiza miaka 69 tangu kuundwa kwake. Maadhimisho hayo yamefanyika Viwanja vya Karimjee. 
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Tanzania na Mratibu Mkazi wa UNDP Tanzania, Alvero Rodriquez, akihutubia kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Tanzania na Mratibu Mkazi wa UNDP Tanzania, Alvero Rodriquez (kushoto) akiwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, wakifuatilia matukio mbalimbali ya hafla hiyo.
Gwaride maalumu la maadhimisho hao.
Waziri Tibaijuka akihojiwa na wanahabri kuhusu 
maadhimisho hayo.
Wawakilishi wa mashirika ya kimataifa wakiwa 
kwenye maadhimisho hayo.
Wageni waalikwa wakisubiri kuondoka baada ya kumalizika kwa maadhimisho hayo.
Wanafunzi wakiwa kwenye sherehe hiyo.
Gwaride maalumu la watoto la bendera likitoa 
heshima kwa mgeni rasmi.
Wapiga picha kutoka vyombo mbalimbali vya habari 
wakichukua tukio hilo.
Wanahabari wakichukua taarifa mbalimbali za maadhimisho hayo.
Wanafunzi wa Shule ya Viziwi ya Buguruni 
wakitoa burudani kwenye maadhimisho hayo.
Burudani zikiendelea
………………………………………………………………………………………………..
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka amehimiza nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuunganisha nguvu katika kukabiliana na changamoto za Mabadiliko ya Tabia Nchi miongoni mwao.
 Tibaijuka alitoa wito huo  katika sherehe za kuazimisha miaka 69 ya Umoja wa Mataifa zilizofanyika katika viwanja vya ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa mgeni rasmi.
Waziri Tibaijuka, aliyemwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika maazimisho hayo alibainisha kuwa mabadiliko ya Tabia Nchi yameendelea kuwa tishio kubwa kwa binadamu katika siku za leo duniani kote.
Kutokana na hali hiyo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliitisha mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Septemba 23, mwaka huu ambapo watu, nchi, mabara na wafanyabiashara walitoa tamko la kuungana pamoja kwa kila mmoja kuinusuru dunia.
Prof. Tibaijuka alisema kuwa akiwakilisha bara la Afrika, Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete aliwasilisha mpango unaoonyesha juhudi za pamoja zinazofanywa na bara hilo kukabiliana na mabadiliko hayo.
“Katika mkutano huo, Tanzania imeahidi kuimarisha juhudi zake katika kutunza misitu na matumizi ya nishati kama upepo, sola na gesi asilia,” Waziri Tibaijuka alisema.
Hivyo Prof. Tibaijuka alihimisa nchi wahisani kutimiza ahadi zao kwa wakati hususani kutoa fedha kiasi cha dola za Kimarekani billion 100 kila mwaka hadi 2020 zitakazosaidia katika juhudi za kupambana na changamotio hizo.
Waziri aliwaambia wageni waalikwa katika sherehe hizo pia kuwa Tanzania inaendelea kutekeleza malengo ya changamoto za mileniamu na kuhakikisha kuwa nchi inaendelea kuimarisha amani, utawala wa sheria na kudimisha haki za binadamu.

KAMPUNI YA KARIATI YAKABIDHI WAKULIMA MATREKTA MANNE LEO, JIJINI DAR ES SALAAM


Kampuni ya Kariati Matracktor Diwani wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, Omary Kariati, leo imekabidhi matrekta manne kwa wakulima wa wilaya ya Kondoa (matrekta matatu) na Mbarali (trekta moja), katika hafla iliyofanyika leo asubuhi, kwenye Ofisi za Kariati Matrektor, Kinondoni, Dar es Salaam. Zinazofuatia ni picha za hafla hiyo. Picha/Maelezo na Bashir Nkoromo
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kariati Matractor, Omary Kariati akimkabidhi fungua za trekta Mwakilishi wa wkulima wa Kondoa, Karoli Lubuva, katika hafla ya makabidhiano hayo, iliyofanyika leo.
Kariati akikata uatepe kuzindua makabidhiano ya trekta hizo
 Kariati akiwapa maelezo kuhusu trekta husika kabla ya kuzikabidhi kwa wawakilishi wa wakulima hao leo
Kariati akilijaribu moja ya matrekta hayo akiwa na mwakilishi wa wakulima kutoka Kondoa Karoli Lubuva.

NAIBU WAZIRI ELIMU NA MAFUNZO JENISTA MHAGAMA ANENA - KIGOMA

JENISTA MHAGAMA -KIGOMANa Magreth Magosso,Kigoma

Naibu Waziri wa  Elimu  na  Ufundi Jenista Muhagama ashauri Uongozi wa  shule ya Sekondari ya Mwilamvya ifungue kitengo cha ushauri nasaha shuleni hapo, ili kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa maadili  kwa wanafunzi husika.
 
Kauli hiyo imetokana na risala iliyosomwa jana na Mkuu wa shule Emmanuel  King  katika mahafali ya Darasa la saba na kidato cha Nnne yaliyofanyika  shuleni hapo ambayo ipo katika  kata ya murusi wilayani Kasulu Mkoa wa Kigoma.
 
Akifafanua hilo kwa niaba ya Naibu  husika,Mkaguzi wa shule Kanda magharibi Adriani Mlelwa alisema   utandawazi ni chanzo cha madili kwenda mlama , shida ipo katika mapokeo huku ashauri wafungue kitengo hicho,  ili kudhibiti maadili  na nidhamu kwa wanafunzi.
 
“mawasiliano ni muhimu , wekeni taratibu,kanuni na sheria itasaidia kudhibiti wanafunzi kumiliki simu za mkononi holela,mnaweza mkawa na simu moja ambayo mzazi ataongea na kijana  ” alisema Mlelwa.
Ampongeza mtendaji wa shule Elias Maliyatabu kwa kitendo cha kutumia rasilimali mali na akili katika kuwekeza  elimu mkoani kigoma , ni mtendaji wa kwanza wa hapo mwenye tija ya kufuta ujinga kwa wakazi husika.

Wigo mpana wa kushirikisha  na ushawishi kwa wadau ni chachu ya kuboresha  vitendea kazi  hasa mabara ya kisasa  ni moja ya sifa ya wanafunzi kufuta  alama ya sifuri katika  mtihani wa taifa na kanda  tangu ianzishwe  2005.

Akijibia hilo Mkurugenzi Maliyatabu alisema mafaniko yanatokana na wazazi ambao wanaufahamu  wa tija ya elimu kwa mtoto ,ambapo ni urithi bora wa kushinda adui ujinga na umaskini siku za usoni.
Baadhi ya wanafunzi wahitimu Elimina Segenya na Inocent Batholomeo kwa nyakati tofauti walisema umiliki wa simu kwa wanafunzi chanzo cha kukosa umakini katika masomo.

Waomba wazazi wasiwape simu vijana na kutaka uongozi wa shule uweke utaratibu wa kuweka  watoa huduma ya chakula  zaidi ya mmoja  ili kuboresha uwajibikaji.

Pia Zaidi ya Milioni  Tatu zimetumika katika  ununuzi wa ng`ombe jike moja la maziwa na dume,vitenge doti 10,debe moja la dagaa wa hapa na Lita 20 mafuta ya mawese.

Friday, October 24, 2014

PROF.TIBAIJUKA:MAGONJWA YA MLIPUKO YATEKELEZWE KIMATAIFA


Picha-na-3

Na Anita Jonas-MAELEZO
Umoja wa Mataifa umeshauri  kuchukua  hatua za haraka kwa magongwa ya mlipuko yanayotokea Afrika kama Ebola kwani yanadhiri uchumi wa mataifa husika.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka wakati wa Maadhimisho ya Miaka 69 ya Umoja wa Kimataifa leo Jijini Dar es Salaam.

Prof. Tibaijuka alisema kuwa Umoja wa Mataifa wanatakiwa kuchukua tahadhari ya milipuko ya magonjwa hatarishi na kuyachukulia kama ni magonjwa ya Kidunia kwani yanaathiri mifumo yote ya kimaendeleo.

“Mataifa yaliyoendelea yasingepuuzia mlipuko wa  ugonjwa wa Ebola ulipojitokeza  Afrika  hali  isingekuwa  hatarishi kama ilivyo sasa, hivyo ni rai yangu kwa Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na mataifa husika kuchukua  tahadhari wakati wote ”Alisema Prof. Tibaijuka.

Aidha, Prof. Tibaijuka alisema kuwa kutokana na tatizo la mabadiliko ya tabia nchi kuwa tishio miongoni mwa wengi duniani, wahisani wa maendeleo hawanabudi kusaidia Mataifa mengine ikiwamo utekelezaji wa Mfuko wa Kijani wa Hali ya hewa.

Akizungumzia kuhusu hatua ya Rais Dkt. Jakaya Kikwete kutoa uraia kwa wakimbizi 162,000 kutoka Burundi, Prof. Tibaijuka alisema kuwa Tanzania imeonyesha ulimwengu kuwa suala la mapambano dhidi ya ukimbizi linaweza kufanyiwa kazi na kuwafanya wakimbizi kuishi maisha kama binadamu wengine.

Naye Mratibu muwakilishi wa makazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bw. Alvaro Rodriguez alisema kuwa shirika hilo kwa kushirikiana na serikali na wadau wengine,  wamepanga kusaidia na kuboresha miundombinu ya kiusalama ili kuendeleza amani Duniani kwani bila amani maendeleo ni vigumu kupatikana.

Pia Bw. Rodriguez aliipongeza Tanzania katika kutekeleza Malengo ya Millenia katika sekta ya afya kwa ambapo asilimia 96 ya vituo vyote vya afya nchini vinatoa huduma ya afya ya uzazi kwa mama na mtoto.

Sherehe hizo zimebebwa na kauli mbiu ya “Leave no One Behind” ikiwa na mlengo wa kuleta maendeleo yenye usawa duniani.

UBORESHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA KUANZA KATIKATI YA NOVEMBA 2014


IMG_8833
Makamu Mwenyekiti wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), pia  na Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Hamid   Mahamoud Hamid(kushoto)  akitoa ufafanuzi baada kusoma taarifa kuhusu kuanza kwa shughuli za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dares Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa NEC.Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Julias Malaba.
…………………………………………………………..
Na Magreth Kinabo,Maelezo
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) imesema kwamba  zoezi la majaribio ya  Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linatarajia kuanza rasmi katikati mwa mwezi  Novemba mwaka huu.
 
Aidha  NEC imefafanu kwamba zoezi hilo, litafanyika kwa kutumia mfumo mpya wa ‘Biometric Voter Registration’(BVR) katika majimbo matatu ya uchaguzi ambayo ni Kawe katika Manispaa ya Kinondoni, Kilombero, Halimashauri ya Mji wa Kilombero na Mlele, Halimashauri ya Mlele, ambapo vituo vya uandikishaji vimewekwa katika kata zilizomo katika majimbo husika.
 
Hayo yalisemwa  na Makamu Mwenyekiti wa NEC  pia  na Jaji  Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Hamid   Mahamoud  Hamid,wakati  akisoma taarifa kuhusu kuanza kwa shughuli za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura  katika  mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dares Salaam.
 
“Tume tayari imekwishapokea baadhi ya vifaa muhimu vya uandikishaji zikiwemo fomu za unadikishaji, hivyo kinachosubiriwa ni kupokea BVR kits 250 zinazotarajiwa kupokelewa wakati wowote kuanzia leo. Zoezi la Uandikishaji litakapoanza, vituo vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni, vyama vya siasa vinaruhusiwa  kuweka mawakala wao katika kituo ili kushuhudia jinsi uandikishaji utakavyokuwa unafanyika,” alisema  Hamid.
 
 Makamu Mwenyekiti huyo alisema baada ya zoezi hilo kukamilika zoezi hilo litaanza katika maeneo mengine.
 
“ Tunatarajia Uboreshaji  wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utafanyika kwa wakati mmoja katika mikoa yote nchini isipokuwa mkoa wa Dares Salaam na Zanzibar.Uandikishaji katika mikao ya Dares Salaam na Zanzibar utafanyika baada ya uandikishaji katika mikoa yote utakapokamilika.Muda wa uandikishaji  utakuwa ni siku saba katika kila kituo,” alisema.
Aliongeza kwamba uandikishaji katika mikoa yote umepangwa kufanyika kuanzia mwanzoni mwa mwezi Januari, mwaka huu hadi katikati ya   Februari mwaka huu, wakati katika mikoa ya Dares Salaam na Zanzibar utafanyika mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu.
 
 Alisema uandikishaji katika mikoa yote utafanyika katika awamu nne kwenye kila halimashauri ili kutoa fursa ya kuhamisha vifaa vya uandikishaji   kutoka eneo moja kwenda eneo lingine.
 
“Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utahusisha  wapiga kura wote wapya na wa zamani. Wapiga kura wa zamani yaani wale ambao walikuwa wamejiandikisha katika Daftari la Zamani, watatakiwa kwenda katika vituo vya kujiandikisha vilivyoko karibu na maeneo wanayoishi ili kuchukuliwa taarifa zao hasa alama za vidole, picha na saini zao kuiongizwa katika mfumo Biometric Voter Registration na hatimaye watapewa vitambulisho vipya.” Alisisitiza.
 
Alisema wapiga kura ambao watakuwa na kadi zao za kupiga kura za zamani watatakiwa kwenda na kadi zao katika kituo cha kujiandikisha ili kurahisisha zoezi la kuhamisha taarifa zao za awali katika mfumo mpya wa BVR.
 
Aidha alifafanua kwamba  kwa wapiga kura waliopoteza kadi au wale ambao kadi zao zimeharibika watatakiwa kwenta kituoni ili kujiandikisha na kupewa kadi mpya.
 
 Hamid alisema kwa wapiga kura wenye vitambulisho vya taifa Dares Salaam na Zanzibar watakuja na kadi zao ambazo ni taarifa zao zitasomwa na vifaa maalum ili kupunguza muda utakaotumika katika zoezi hilo, pia watapewa kadi mpya ya mpiga kura.
 
 Alisema kwa wapiga kura wanaoishi na ulemavu na wale ambao hawajui kusoma na kuandika wanaruhusiwa kwenda kituoni na mtu mmoja katika familia wanayemuamini ili kusaidia katika uandikishaji.
 
“Uboreshaji huu unahusisha pia kuandikisha wapiga kura wote waliotimiza umri wa miaka 18 au zaidi na wale ambao ifikapo siku ya upigaji  kura ya maoni na uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 watakuwa wametimiza umri wa miaka 18. Pia wale wote ambao kwa sababu mbalimbali hawakuwahi kujiandikisha katika Daftari la  Kudumu  la Wapiga Kura katika mazoezi yote uandikishaji yaliyopita,” alisisitiza.
 
Hivyo jumla ya watu wenye umri wa miaka 18 na zaidi wapatao milioni 23.09 wanatarajiwa kujiandikisha.
 
Hamid aliongeza kwamba mpiga kura atakayejiandikisha katika daftari hilo la sasa pekee na kupewa kadi ndiye atakayeruhusiwa kupiga kura.
 
“Wakati wa uandikishaji, kipaumbele kitatolewa  kwa watu wanaoishi na ulemavu, wazee, wagonjwa wakinamama wajawazito na wenye watoto wachanga. Hivyo hawatalazimika kusimama kwenye mstari.
 
Naye Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka  NEC, Julias Malaba alisema tayari kiasi cha fedha cha Sh. bilioni 15 zimeshatolewa kwa ajili ya zoezi hilo.Huku Makamu Mwenyekiti wa NEC  akisema bajeti halisi litafafanuliwa baadae.
 
Kwa upande wake, Sisti  Cariah ambaye ni Mkuu wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na Naibu Katibu NEC, alisema daftari hilo litakamilika  Aprili 14,mwaka huu na litawekwa  wazi   kwa muda wa siku tano katika maeneo husika  ili kumwezesha kila mtu aliyejiandikisha  aende  kukagua na kujiridhisha kwa taarifa zake zimeandikwa  kwa usahihi.
 
 Tume hiyo inatoa wito kwa wananchi wote wenye sifa za kujiandikisha kujitokeza kwa wingi katika vituo vyote vya uandikishaji kwa ajili ya kujiandikisha katika daftari hilo.
Akizungumzia  kuhusu mfumo wa BVR alisema unasaidia kupunguza ujiandikisha mara mbili na kuwa na taarifa sahihi.