Na Anita Jonas-MAELEZO
Umoja wa Mataifa umeshauri
kuchukua hatua za haraka kwa magongwa ya mlipuko yanayotokea Afrika
kama Ebola kwani yanadhiri uchumi wa mataifa husika.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka wakati wa Maadhimisho
ya Miaka 69 ya Umoja wa Kimataifa leo Jijini Dar es Salaam.
Prof. Tibaijuka alisema kuwa Umoja
wa Mataifa wanatakiwa kuchukua tahadhari ya milipuko ya magonjwa
hatarishi na kuyachukulia kama ni magonjwa ya Kidunia kwani yanaathiri
mifumo yote ya kimaendeleo.
“Mataifa yaliyoendelea
yasingepuuzia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola ulipojitokeza Afrika hali
isingekuwa hatarishi kama ilivyo sasa, hivyo ni rai yangu kwa Umoja wa
Mataifa kwa kushirikiana na mataifa husika kuchukua tahadhari wakati
wote ”Alisema Prof. Tibaijuka.
Aidha, Prof. Tibaijuka alisema
kuwa kutokana na tatizo la mabadiliko ya tabia nchi kuwa tishio miongoni
mwa wengi duniani, wahisani wa maendeleo hawanabudi kusaidia Mataifa
mengine ikiwamo utekelezaji wa Mfuko wa Kijani wa Hali ya hewa.
Akizungumzia kuhusu hatua ya Rais
Dkt. Jakaya Kikwete kutoa uraia kwa wakimbizi 162,000 kutoka Burundi,
Prof. Tibaijuka alisema kuwa Tanzania imeonyesha ulimwengu kuwa suala la
mapambano dhidi ya ukimbizi linaweza kufanyiwa kazi na kuwafanya
wakimbizi kuishi maisha kama binadamu wengine.
Naye Mratibu muwakilishi wa makazi
wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bw. Alvaro Rodriguez
alisema kuwa shirika hilo kwa kushirikiana na serikali na wadau
wengine, wamepanga kusaidia na kuboresha miundombinu ya kiusalama ili
kuendeleza amani Duniani kwani bila amani maendeleo ni vigumu
kupatikana.
Pia Bw. Rodriguez aliipongeza
Tanzania katika kutekeleza Malengo ya Millenia katika sekta ya afya kwa
ambapo asilimia 96 ya vituo vyote vya afya nchini vinatoa huduma ya afya
ya uzazi kwa mama na mtoto.
Sherehe hizo zimebebwa na kauli mbiu ya “Leave no One Behind” ikiwa na mlengo wa kuleta maendeleo yenye usawa duniani.
No comments:
Post a Comment