Naibu Waziri
wa Elimu na Ufundi
Jenista Muhagama ashauri Uongozi wa shule ya Sekondari ya Mwilamvya ifungue
kitengo cha ushauri nasaha shuleni hapo, ili kukabiliana na changamoto
ya ukosefu wa maadili kwa wanafunzi
husika.
Kauli hiyo
imetokana na risala iliyosomwa jana na Mkuu wa shule Emmanuel King katika
mahafali ya Darasa la saba na kidato cha Nnne yaliyofanyika shuleni hapo ambayo ipo katika kata ya murusi wilayani Kasulu Mkoa wa Kigoma.
“mawasiliano
ni muhimu , wekeni taratibu,kanuni na sheria itasaidia kudhibiti wanafunzi kumiliki
simu za mkononi holela,mnaweza mkawa na simu moja ambayo mzazi ataongea na
kijana ” alisema Mlelwa.
Ampongeza
mtendaji wa shule Elias Maliyatabu kwa kitendo cha kutumia rasilimali mali na
akili katika kuwekeza elimu mkoani
kigoma , ni mtendaji wa kwanza wa hapo mwenye tija ya kufuta ujinga kwa wakazi
husika.
Wigo mpana wa
kushirikisha na ushawishi kwa wadau ni
chachu ya kuboresha vitendea kazi hasa mabara ya kisasa ni moja ya sifa ya wanafunzi kufuta alama ya sifuri katika mtihani wa taifa na kanda tangu
ianzishwe 2005.
Akijibia
hilo Mkurugenzi Maliyatabu alisema mafaniko yanatokana na wazazi ambao wanaufahamu
wa tija ya elimu kwa mtoto ,ambapo ni
urithi bora wa kushinda adui ujinga na umaskini siku za usoni.
Baadhi ya wanafunzi
wahitimu Elimina Segenya na Inocent Batholomeo kwa nyakati tofauti walisema umiliki
wa simu kwa wanafunzi chanzo cha kukosa umakini katika masomo.
Waomba wazazi
wasiwape simu vijana na kutaka uongozi wa shule uweke utaratibu wa kuweka watoa huduma ya chakula zaidi ya mmoja ili kuboresha uwajibikaji.
Pia Zaidi ya
Milioni Tatu zimetumika katika ununuzi wa ng`ombe jike moja la maziwa na
dume,vitenge doti 10,debe moja la dagaa wa hapa na Lita 20 mafuta ya mawese.
No comments:
Post a Comment