Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka,ambaye
alimwakilisha Rais Jakaya Kikwete, akihutubia Dar es Salaam, katika
Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa kutimiza miaka 69 tangu kuundwa
kwake. Maadhimisho hayo yamefanyika Viwanja vya Karimjee.
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Tanzania na Mratibu Mkazi wa UNDP Tanzania, Alvero Rodriquez, akihutubia kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Tanzania na Mratibu Mkazi wa UNDP Tanzania, Alvero Rodriquez (kushoto) akiwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, wakifuatilia matukio mbalimbali ya hafla hiyo.
Gwaride maalumu la maadhimisho hao.
Waziri Tibaijuka akihojiwa na wanahabri kuhusu
maadhimisho hayo.
Wawakilishi wa mashirika ya kimataifa wakiwa
kwenye maadhimisho hayo.
Wageni waalikwa wakisubiri kuondoka baada ya kumalizika kwa maadhimisho hayo.
Wanafunzi wakiwa kwenye sherehe hiyo.
Gwaride maalumu la watoto la bendera likitoa
heshima kwa mgeni rasmi.
Wapiga picha kutoka vyombo mbalimbali vya habari
wakichukua tukio hilo.
Wanahabari wakichukua taarifa mbalimbali za maadhimisho hayo.
Wanafunzi wa Shule ya Viziwi ya Buguruni
wakitoa burudani kwenye maadhimisho hayo.
Burudani zikiendelea
………………………………………………………………………………………………..
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka amehimiza nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuunganisha nguvu katika kukabiliana na changamoto za Mabadiliko ya Tabia Nchi miongoni mwao.
………………………………………………………………………………………………..
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka amehimiza nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuunganisha nguvu katika kukabiliana na changamoto za Mabadiliko ya Tabia Nchi miongoni mwao.
Tibaijuka
alitoa wito huo katika sherehe za kuazimisha miaka 69 ya Umoja wa
Mataifa zilizofanyika katika viwanja vya ukumbi wa Karimjee jijini Dar
es Salaam ambapo alikuwa mgeni rasmi.
Waziri
Tibaijuka, aliyemwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika maazimisho hayo
alibainisha kuwa mabadiliko ya Tabia Nchi yameendelea kuwa tishio kubwa
kwa binadamu katika siku za leo duniani kote.
Kutokana
na hali hiyo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliitisha mkutano wa
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Septemba 23, mwaka huu ambapo watu, nchi,
mabara na wafanyabiashara walitoa tamko la kuungana pamoja kwa kila
mmoja kuinusuru dunia.
Prof.
Tibaijuka alisema kuwa akiwakilisha bara la Afrika, Rais wa Tanzania
Jakaya Kikwete aliwasilisha mpango unaoonyesha juhudi za pamoja
zinazofanywa na bara hilo kukabiliana na mabadiliko hayo.
“Katika
mkutano huo, Tanzania imeahidi kuimarisha juhudi zake katika kutunza
misitu na matumizi ya nishati kama upepo, sola na gesi asilia,” Waziri
Tibaijuka alisema.
Hivyo
Prof. Tibaijuka alihimisa nchi wahisani kutimiza ahadi zao kwa wakati
hususani kutoa fedha kiasi cha dola za Kimarekani billion 100 kila mwaka
hadi 2020 zitakazosaidia katika juhudi za kupambana na changamotio
hizo.
Waziri
aliwaambia wageni waalikwa katika sherehe hizo pia kuwa Tanzania
inaendelea kutekeleza malengo ya changamoto za mileniamu na kuhakikisha
kuwa nchi inaendelea kuimarisha amani, utawala wa sheria na kudimisha
haki za binadamu.
No comments:
Post a Comment