Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya
Fahamu (MOI) Dkt. Othmani Kiloloma akiwaeleza waandishi wa
habari(hawapo pichani) majukumu wanayotekeleza katika kuhakikisha
wanakabiliana na tatizo la Mgongo wazi na Vichwa vikubwa ikiwamo kutoa
elimu bora kwa madaktari wanaosomea somo hilo, kwenda mikoani kutoa tiba
kwa watoto wenye matatizo hayo,wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto
wa kichwa kikubwa na na Mgongo wazi duniani Jijini Dar es salaam.
Kushoto ni mwenyekiti wa chama cha wazazi wenye watoto wa kichwa kikubwa
na mgongo wazi(ASBHAT) Bw. Abdulhakim Bayakub.PICHA NA HASSAN
SILAYO-MAELEZO
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya
Fahamu (MOI) Dkt. Othmani Kiloloma akimkabidhi Mama Dorcas Membe kitabu
cha Mpango shirikishi wa Mtoto wa kichwa kikubwa na Mgongo Wazi jana na
kumuomba kuwa Mlezi wa chama cha Chama cha Wazazi wenye Watoto wa
Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) ambapo ameahidi kushirikiana na
chama hicho katika harakati za kukabiliana na Tatizo la Kichwa Kikubwa
na Mgongo wazi. kulia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Abdulhakim
Bayakub.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi
(ASBHAT) Bw. Abdulhakim Bayakub akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI)
Dkt. Othmani Kiloloma cheti shukrani kwa mchango wanaoendelea kuutoa
cha chama hicho ikiwamo kutoa matibabu kwa Watoto wa Kichwa Kikubwa na
Mgongo Wazi.
Baadhi
ya wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi waliojitokeza
katika sherehe hizo za Maadhimisho ya ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa
na na Mgongo wazi duniani yaliyofanyika Taasisi ya Tiba ya Mifupa,
Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) leo Jijini Dar es Salaam. Baadhi
ya wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi waliojitokeza
katika sherehe hizo za Maadhimisho ya ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa
na na Mgongo wazi duniani yaliyofanyika Taasisi ya Tiba ya Mifupa,
Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) jana Jijini Dar es Salaam. Afisa
Muuguzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya
Fahamu (MOI) Bi. Germana Gasper akitoa maaelezo kwa wananchi
waliojitokeza katika banda wakati wa sherehe na kuwaasa wazazi hasa
wakike waliokatika umri wa kubeba mimba kutumia vyakula vyenye vitamin
ya Foliki kama maembe, Mchicha, Mihogo,machungwa, maharage,
mahindi,mayai, ndizi, parachichi, papai, maini na kabichi, ili
kukabiliana na tatizo la Kichwa kikubwa na Mgongo wazi kwa watoto
wanaozaliwa
Mlezi
wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi
(ASBHAT) Mama Dorcas Membe, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya
Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dkt. Othmani
Kiloloma(Kulia), Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa
Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Bw. Abdulhakim Bayakub(mwenye T-shirt
nyeupe) na Moja ya mtoto mwenye tatizo la Kichwa Kikubwa wakikata keki
katika sherehe za Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na
Mgongo wazi duniani jana Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya
Fahamu (MOI) Dkt. Othmani Kiloloma akimlisha keki Moja ya mtoto mwenye
tatizo la Kichwa Kikubwa wakikata keki katika sherehe za Maadhimisho ya
siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na Mgongo wazi duniani jana Jijini Dar
es salaam.
Mlezi
wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi
(ASBHAT) Mama Dorcas Membe akimlisha keki Moja ya mtoto mwenye tatizo la
Kichwa Kikubwa wakikata keki katika sherehe za Maadhimisho ya siku ya
mtoto wa kichwa kikubwa na Mgongo wazi duniani jana Jijini Dar es salaam
Mlezi
wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi
(ASBHAT) Mama Dorcas Membe akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa
Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo
Wazi (ASBHAT) Bw. Abdulhakim Bayakub.
Mlezi
wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi
(ASBHAT) Mama Dorcas Membe akiwapa msaada kinamama wenye watoto wa
Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi.
No comments:
Post a Comment