Pages

KAPIPI TV

Sunday, October 26, 2014

MAJAMBAZI WAFANYA UHALIFU ZIWA TANGANYIKA....KIGOMA,

MAJAMBAZI ZIWA TANGANYIKA
Na Magreth  Magosso,Kigoma

Watu watatu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wakiwa  na silaha tano za moto wamefanya uhalifu katika ziwa Tanganyika Mkoa wa Kigoma,( leo) na kupora injini mbili za Mitumbwi ,solar na Betri zenye thamani  ya zaidi ya   sh. milioni 2.8.
 
Akielezea  tukio hilo Katibu wa Wavuvi  mkoani  Kigoma  Mohamed Kasambwe alisema  mnamo Octoba ,26,mwaka huu  majira  ya saa 6.00 usiku ,mwalo wa Kalalangabo  kaskazini  mwa wilaya ya kigoma  wavuvi walivamiwa na majambazi  hao na kuiba vitu mbalimbali.

“ mtumbwi wao ulikuwa namba 15 HP,  usaliti miongoni mwetu na walikuwa wakiongea kibembe shida ipo katika idara ya polisi,uhamiaji na wamiliki wa mitumbwi miongoni mwetu  chachu ya kushindwa kuthibiti uhalifu ziwani” alisema Mohamed.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa mwalo wa Kibirizi Sendwe Ibrahimu alishauri serikali iweke ulinzi wa jeshi la wananchi  JWTZ katika maeneo tete hasa kijiji cha Kazinga ambapo wahalifu hutumia mwalo kujificha.

Alisema kwa upande wa Lubengela wahalifu wanaogopa kutumia mwalo huo kutokana na ulinzi kuimarishwa hatimaye kutumia vijiji vilivyopo kata ya Kagongo Jimbo la kigoma Kaskazini.

Waathirika wa tukio hilo Kasia Hamimu na Juma Mtusi kwa nyakati tofauti wamekili kuibiwa injini ,mafuta ya petrol lita 50 na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya  sh.milioni 3 .

Mdau wa uvuvi  Salum  Shaban alisema  wavuvi walifika umbali wa mita 20 kutoka mwalo kalalangabo ,majambazi walivamia wavuvi Huku akishauri kuwepo na operesheni shirikishi  ya wadau husika ili kutokomeza uvamizi ziwani.

Kamanda  wa Polisi  mkoa wa Kigoma Jafari Mohamed alipoulizwa  kuhusu hilo tukio  hilo ,alisema yupo katika shughuli ya kusimikwa kwa askofu  wa kanisa  Katoliki na atalijibia baada ya sherehe hiyo kumalizika.

No comments: