Pages

KAPIPI TV

Thursday, October 23, 2014

ADHA YA MAJI YAENDELEA KUWATESA WAKAZI WA KIJIJI CHA SONGAMBELE HALMASHAURI YA NSIMBO WILAYANI MLELE


MAAMUZI MADIWAN
Madiwani na watalaam wa Halmashauri ya Nsimbo wakijadili mstakabali wa maendeleo ya Halmashauri yao Nsimbo,pamoja na kujadili masuala ya elimu, Afya, Miundo mbinu ya barabara,utawala,na maengineyo lakini suala la maji lilichukua nafasi ya kipekee katika kikao hicho cha baraza la madiwani kilichomalizika mwishoni mwa wiki iiliyo
(Picha zote Kibada Kibada -Nsimbo Mlele Katavi).
???????????????????????????????
Mama akisukuma maji kwenye kisima kifupi kilichopo hapo huku akina mama wengine na watoto wakisubiri zamu yao ifike ili waweze kuchota maji  ambayo yanatoka kidogokidogo kwenye kisima hicho hapo madumu yanaonekana hayana maji,  dumu  moja kujaa inawachukua zaidi ya saa, hivyo kuwafanya watumie muda mwingi kutafuta   maji badala ya kufanya shughuli nyingine za maendeleo.
……………………………………………….
 
Na Kibada Kibada –Nsimbo Mlele
Wakazi wa Songambele Halmashauri ya Nsimbo Wilayani Mlele wanakabiliwa na Changamoto ya uhaba wa maji kufuatia visima vifupi vilivyopo kutokuwa maji ya kutosha.
 
Hali  hiyo ya uhaba wa maji kwa baadhi ya Vijiji vya Kata ya Nsimbo na maeneo mengine ya Halmashauri hiyo  inayowafanya akina mama na watoto kuamka  kila siku alfajiri  majira saa kumi usiku kwenda kutafuta maji kwa au  kusubiria  maji  kwenye visim vifupi vilivyopo ambavyo navyo havitoi maji ya kutosha hivyo kutumia muda mrefu kutafuta na kukosa muda wa kufanya shughuli nyingine za maendeleo.
 
Akizungumzia  hali ilivyotete  kuhusu upatikanaji wa maji katika Kijiji  cha Songambele  na Kata ya Nsimbo kwa ujumla Afisa Mtendaji wa Kata ya Nsimbo Wilbroad Milala anasema kwa kweli hapo maji ni shida kubwa kwa wakazi wa hapo.
 
Milala anasema hata visima vilivyopo havitoi maji ya kutosha wakati mwingine kama msimu huu wa kiangazi maji hukata hata miezi miwili bila kutoa maji hali inayofanya wakazi hao hasa akina mama na watoto kufuata maji kwenye mbuga umbali wa takribani kilometa tatu hadi nne maji amabyo siyo safi wala salama.
 
Kufuatia kuwepo kwa changamoto hiyo ya Maji wawakilishi wa wananchi ambao ni madiwani kupitia kwenye vikao vya baraza la madiwani suala la maji lilionekana kuchukua nafasi ya kipekee kuzungumzia ikiwa ni pamoja na kutafuta mbinu za kulipatia ufumbuzi.
 
Akiongea katika kikao cha Baraza la madiwani kwa nyakati tofauti Mjini Nsimbo Diwani wa Kata ya NsimboMichael Kasanga, Diwani wa Kata ya Mtapenda Eliezer Fyula,walieleza kuwa lazima hatua zichukuliwe kwa haraka ili kulipatia ufumbuzi suala la upatikanaji wa maji kwa wakazi wa Halamshauri hiyo hasa maeneo yale yenye visima vifupi vichimbwe visima virefu.
 
Wakaeleza kuwa pia visima vinapoharibika taarifa iwe inatolewa mapema kwenye Idara ya Maji ili kuona namna ya kuweza kulipatia ufumbuzi pale panapo wezeakana kama kununua vifaa vya ukarabati wa pump.
 
Awali Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu na Maji  Raphael Kalinga akiwasilisha taarifa ya Kamati yake alieleza mikakati inayochukuliwa na halmashauri ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa maji ikiwa ni pamoja na kutenga fedha kupitia bajeti zake na fedha kutoka kwenye mifuko ya maji ili kusaidia upatikanaji wa maji ikiwa pia na kuomba ufadhili kutoka kwa wahisani mbalimbali kusaidia suala la maji.
 
Aidha aliwashauri madiwani kuwahamasisha wananchi kuanzisha kamati za mifuko ya maji ili fedha inayopatikana iwe inasaidia katika matengenezo madogo madogo pindi pump za visima vya maji vinapo haribika fedha hizo zitasaidia ukarabati mdogo mdogo.
 
Katika hatua nyingine Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Nsimbo limemwagiza Kaimu Mhandisi wa Mji katika Halmashauri  Enock Msengi kuhakikisha anapoondoka awe anakaimisha ofisi kwa mwenzake anayekuwa ofisini kuliko kuacha amefunga ofisi na pia mali za ofisi inatakiwa awe anacha ofisi ikiwa wazi na awe anaandika barua ya kukabidhi ofisi kuliko kijiondokea kama anavyofanya kwa kuwa ofisi siyo mali yake bali ni mali ya Serikalai.

Wednesday, October 22, 2014

SIKONGE YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MIL.12 KWA WANAFUNZI WASIOJIWEZA

NHIF NA MPANGO WA KUPELEKA MADAKTARI BINGWA MIKOANI

MAOFISA WA UN WAHAMASISHA WANAFUNZI WA JANGWANI KUTEKELEZA AJENDA ZA UMOJA WA MATAIFA

MAOFISA WA UNAfisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama, akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Jangwani akiwa ameambatana na maafisa wenzake wa mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiwa ni shamrashamra ya maadhimisho ya miaka 69 toka Umoja wa Mataifa unazishwe. Kushoto kwa Bi Ledama ni Albert Okal (ILO).

Shamrashamra za maadhimisho ya miaka 69 toka Umoja wa Mataifa uanzishwe zimeanza nchini, na leo jumatano maofisa waandamizi wa UN walitembelea shule ya sekondari ya Jangwani na kuwahabarisha wanafunzi hao juu ya shughuli za Umoja wa Mataifa hapa nchini.

Mjadala kati ya maofisa hao Phillemon Mutashubirwa, Programme Manager wa UN Habitat, Usia Nkhoma Ledama, Afisa habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa(UNIC), Albert Okal (ILO),Greta Sayungi (UNICEF), ulijikita katika masuala ya HIV/AIDS, EBOLA, Usafi na umuhimu wakuosha mikono ili kujikinga na maradhi, elimu ya ujasiriamali, ajira kwa vijana, kazi za kujitolea, malengo ya Milenia na malengo ya Umoja wa Mataifa kwa ujumla wake.

Ijumaa wiki hii Umoja wa Mataifa utaadhimisha mkiaka 69 toka uanzishwe na kilele cha maadhimisho hayo yatafanyika katika viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.
DSC_0106
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama akifafanua jambo wakati akizungumza na wanafunzi wa shule yasekondari Jangwani jijini Dar. Kutoka kushoto ni Phillemon Mutashubirwa (UN Habitat), Greta Sayungi (UNICEF) pamoja na Dr Bwijo Bijo (UNDP)
DSC_0094Pichani juu na chini ni Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Jangwani wakiwasiliza maafisa wa Umoja wa Mataifa waliowatembelea shuleni hapo.
DSC_0083

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MABALOZI WA AFRIKA NCHINI CHINA


unnamedRais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mabalozi wa Afrika wanaoziwakilkisha nchi zao nchini China wakati alipokutana nao jijini Beijing China leo asubuhi.Rais Kikwete yupo nchini China kwa ziara ya kiserikali(picha na Freddy Maro)unnamed3

SHIRIKA LA NDEGE LA FLY DUBAI LAZINDUA NJIA MBILI MPYA ZA NDEGE


Makamu wa Rais mwandamizi katika shughuli za kibiashara wa shirika la ndege la FlyDubai ,Bwa.Sudhir Sreedharan akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo wana habari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani) katika hafla fupi ya uzinduzi wa njia mbili mpya za shirika la ndege hiyo kutoka Dubai kuja jijini Dar es salaam na Zanzibara (nchini Tanzania). Bwa.Sudhir amesema kuwa shirika hilo la Flydubai liliingia katika soko la kibiashara kuanzia mnamo mwaka 12009,ambapo mpaka sasa wamefanikiwa kuongeza njia mpya sita (six new routes ) .
Mgeni rasmi,Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano,Mh Samia Suluhu akizungumza mapema leo katika uzinduzi wa njia mbili mpya za ndege ya FlyDubai aina ya Boieng 737-800,uliofanyika katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jijini Dar.

Wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo wa njia mpya ya shirika la ndege la Flydubai lenye makao yake makuu Dubai..

 Wageni waalikwa wakishangilia jambo.
Sehemu ya wageni waalikwa wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tukio hilo .

MAHAKAMA YA TANZANIA IMEDHAMIRIA KUTEKELEZA DIRA YAKE YA HAKI SAWA KWA WOTE


Kaimu Mkurugenzi, Kurugenzi ya Usimamizi na Uendeshaji wa Mashauri kutoka Mahakama ya Tanzania Bw. John Kahyoza akiwaeleza waandishi wa (hawapo pichani) mikakati iliyoweka iliyowekwa na Mahakama ya Tanzania ili kutekeleza dira yake ya haki sawa kwa wote na kwa wakati kwa vitendo, kwa kuhakikisha inapunguza muda wa mashauri kukaa mahakamani, wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari wa Mahakama ya Tanzania Bi. Mary Gwera. Picha na Hassan silayo-maelezo
………………………………………………………………………………..

Na Georgina Misama-MAELEZO.
Mahakama ya Tanzania imedhamiria kutekeleza dira yake ya haki sawa kwa wote ili kuhakikisha inapunguza muda wa mashauri na rufaa kukaa Mahakamani kwa muda mrefu. Hayo yamesemwa na Afisa Habari wa Mahakama ya Tanzania Bi Mary Gwera wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
 
Akizitaja hatua zilizochukuliwa na Mahakama Bi Mary alisema, kuboresha bajeti ya kushughulikia mashauri kupitia mfuko wa mahakama toka bilioni 57 kwa mwaka 2012/13 mpaka bilioni 88 mwaka 2014/15, Idadi ya vikao vya Mahakama ya Rufani vimeongezeka kutoka 26 mwaka 2012 hadi 34 mwaka 2013/14.
 
Aidha, Bi Mary alisema kuwa hatua nyingine ni pamoja na kuanzisha kitengo cha Mahakama Kuu Dar es Salaam kitakachoshughulikia masuala ya utatuzi wa mashauri kwa njia ya suluhu muafaka, pia uundwaji wa kamati ya kanuni za Mahakama itakayosaidia kutunga au kurekebisha kanuni ili kuhakikisha kuwa kanuni zinazotumika Mahakamani si chanzo cha kuchelewa mashauri Mahakamami
 
Naye, Kaimu Mkurugenzi, Kurugenzi ya Usimamizi na Uendeshaji wa Mashauri kutoka Mahakama ya Tanzania Bw. John Kahyoza alisema kuwa Mahakama imeanza kuchukua hatua za kuimarisha ukaguzi wa shughuli za Mahakama na maadili ya watumishi kwa kuanzisha kurugenzi ya ukaguzi na maadili.
 
Aidha, Bw Kahyoza alivitaja viwango ambavyo kila hakimu au Jaji anatakiwa kuvitimiza kwa mwaka na muda ambao mashauri yanatakiwa kuwa Mahakamani kuwa ni Mh. Jaji wa Mahakama Kuu analenga kumaliza kesi 220, Mahakimu wa Mahakama za Wilaya na Hakimu Mkazi kesi 250 na Mahakimu wa Mahakama za mwanzo kesi 260
 
Mahakama Kuu inatoa rai kwa Watanzania kufika Mahakamani kwa Tarehe zinazopangwa ili kuisaidia Mahakama kuhakikisha inapunguza muda wa mashauri kukaa Mahakamani.

"MADIWANI SIMAMIENI VIZURI MAPATO NA MIRADI YA MAENDELEO"; KAMOGA

Na Allan Ntana, Sikonge

MADIWANI wa halmashauri ya wilaya ya Sikonge mkoani Tabora wametakiwa
kusimamia kwa nguvu zote ukusanyaji wa mapato ya ndani na kufuatilia
kwa karibu zaidi utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kufanikisha
shughuli zote za uendeshaji wa halmashauri hiyo kwa kiwango
kinachotakiwa.

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Robert
Kamoga katika hotuba yake ya ufunguzi wa kikao cha baraza la madiwani
wa halmashauri hiyo kilichofanyika jana katika ukumbi wa Chuo cha
Maendeleo ya Jamii (FDC) mjini Sikonge.

Alisema ili halmashauri hiyo iweze kufanikisha utekelezaji wa mipango
yake ya kimaendeleo kwa mwaka wa fedha 2014/2015 kama ilivyopangwa
wanapaswa kuongeza juhudi katika suala zima la ukusanyaji mapato
kutoka katika vyanzo vyake vya ndani sambamba na kuwa na usimamaizi
mzuri wa mapato hayo.

Akielezea jitihada zilizowezesha halmashauri hiyo kuvuka lengo la
makusanyo katika kipindi cha msimu wa 2013/2014, alisema watendaji
wote walishikamana na kuwa kitu kimoja huku kila mmoja akitekeleza
wajibu wake ipasavyo, hivyo akawataka madiwani hao kusimamia kwa nguvu
zote ukusanyaji mapato na utekelezaji miradi ili kufanikisha malengo
ya halmashauri hiyo.

‘Waheshimiwa madiwani ili kufikia lengo la kukusanya kile
tulichojipangia hatuna budi kusimamia kwa nguvu zetu zote ili tuweze
kufanikisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa maabara
kwa kila shule na shughuli zote za uendeshaji wa halmashauri yetu’,
aliongeza.

Akizungumzia mafanikio ya miradi mbalimbali ya maendeleo, Kamoga
alisema huduma katika zahanati na vituo vya afya Kitunda na Mazinge
zimeendelea kuboreshwa kwa kuongeza majengo ya upasuaji na vifaa tiba
kupitia mapato ya halmashauri na michango ya wahisani.

Huduma nyingine ambazo zimeendelea kuboreshwa ni usambazaji wa maji
safi na salama sambamba na ukamilishaji ujenzi wa miradi ya maji
Majojoro na Mibono ikiwemo mradi wa usambazaji maji Sikonge mjini,
japokuwa changamoto kadhaa zimekuwa zikijitokeza ikiwemo uharibifu wa
miundo mbinu, ukosefu wa nishati ya kuendeshea mitambo na maji
kutowafikia wananchi wote.

Aidha Kamoga alisema sekta ya elimu pia imeendelea kuboreshwa kwa
kiwango kikubwa kwa kuongeza madawati mashuleni, ujenzi wa nyumba za
waalimu na vyumba vya madarasa sambamba na uboreshaji miundo mbinu ya
barabara kwa kufanya matengenezo ya mara kwa mara ya barabara zote za
vijijini na mjini.

Akitoa salaamu kwa niaba ya Mkuu wa wilaya hiyo Hanifa Selengu,
KatibuTawala wa halmashauri hiyo Geofrey Mtalemwa aliwataka watendaji
wote wa vijiji na kata kwa kushirikiana na madiwani kuhamasisha
kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika suala zima la kilimo
kwani msimu wa mvua ndio umeanza.

Pia aliwataka watendaji wote wa halmashauri, tarafa, kata na vijiji
kuhamasisha na kusimamia ipasavyo suala la elimu kwa kulipa uzito
unaostahili hasa ikizingatiwa kuwa taifa zima liko katika mchakato wa
ujenzi wa maabara katika kila shule, kwani maabara zinaendana na uwepo
wa wanafunzi, vinginevyo hatuwezi kufanikiwa.

WATU WATATU WAUAWA MKOANI MBEYA


WATATU WAUAWA MBEYA 

WATU WATATU WASIOFAHAMIKA MAJINA WALA MAKAZI YAO, JINSI ZA KIUME, UMRI KATI YA MIAKA 25 -29, WALIUAWA KWA KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI, FIMBO, MAWE KUTOKANA NA TUHUMA ZA UVUNJAJI.

TUKIO HILO USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 00:51 HUKO KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA MBEYA, KATA NA TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.

INADAIWA KUWA, WANANCHI HAO WAISHIO KATIKA ENEO LA FOREST MPYA NYUMA YA HOSPITALI YA MKOA WA MBEYA WALIWAKAMATA WATU HAO WAKIWA NA VIFAA VINAVYOTUMIKA KUVUNJIA VIKIWEMO NONDO, PLAIZI PAMOJA NA MISUMARI NA NDIPO WALIAMUA KUWASHAMBULIA KWA KUWAPIGA SEHEMU MBALIMBALI ZA MIILI.

WATU HAO WALIFARIKI DUNIA WAKIWA NJIANI KUPELEKWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA NA ASKARI WA KIKOSI CHA KUZUIA NA KUPAMBANA NA UJAMBAZI CHA WILAYA YA MBEYA, JUHUDI ZA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI ZINAENDELEA. 

MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA UCHUNGUZI WA KITABIBU NA UTAMBUZI.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.

KATIKA TUKIO LA PILI:
 MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA KANGAGA WILAYANI MBARALI AITWAYE FUNGO KIFANGA (50) ALIUAWA KWA KUPIGWA NA KITU KIZITO SEHEMU ZA KICHWANI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 21.10.2014 MAJIRA YA SAA 19:00 JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA KANGAGA, KATA YA MAWINDI, TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA.

INADAIWA KUWA, CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI UGOMVI WA ARDHI KATI YA MAREHEMU NA WATU HAO AMBAO BADO KUFAHAMIKA. AIDHA, WATU WATATU WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA MAHOJIANO ZAIDI KUHUSIANA NA TUKIO HILO AMBAO NI 1. CLEMENCE KIBIKI, (28) MKAZI WA KANGAGA 2. IMANI KIBIKI (23) MKAZI WA KANGAGA NA 3. FIDELIS KIBIKI (34) MKAZI WA KANGAGA. 

MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MBARALI KWA UCHUNGUZI WA KITABIBU.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUTATUA MIGOGORO YAO KWA NJIA YA AMANI NA UTULIVU ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA.

KATIKA TUKIO LA TATU:
MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA MBIGILI WILAYA YA RUNGWE AITWAYE AMANI LIKENEME MWAKYOMA (50) ALIUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU ZA KICHWANI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 20.10.2014 MAJIRA YA SAA 23:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA MBIGILI, KATA YA RWANGWA, TARAFA YA BUSOKELO, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA.

CHANZO CHA MAUAJI HAYO BADO HAKIJAFAHAMIKA, JUHUDI ZA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI ZINAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA RUNGWE.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO/WALIPO WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA. Imesainiwa na: [BARAKAEL N. MASAKI – ACP] KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

MAAMBUKIZI VVU KUTOKA KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO YAPUNGUA-EGPAF

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Mrisho  Kikwete akipata maelezo kwa Meneja wa Shirika la EGPAF Dr.Alphaxard Lwitakubi, wakati wa maonesho ya wiki ya vijana iliyofanyika kitaifa mkoani Tabora.
MAAMBUKIZI ya virusi vya Ukimwi (VVU), kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto yamepungua kwa asilimia 90. Imeelezwa.
Hayo yalisemwa na Meneja wa shirika la EGPAF Mkoa wa Tabora, Dk. Alphaxard Lwitakubi, mara baada ya Rais Jakaya Kikwete kukagua banda la shirika hilo katika maonyesho ya wiki ya vijana iliyoambatana na kilele cha kuzimwa kwa Mwenge wa Uhuru.
Lwitakubi, alisema lengo la EGPAF ni kufikia asilimia 98 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2015.
Alisema hatua hiyo itafikiwa endapo wanaume wataambatana na wake zao kwenda kwenye vituo vya afya kama inavyotakiwa, kwani hadi sasa zimefikiwa asilimia 48 kwa mwaka 2014 kutoka asilimia 5 mwaka 2010.
Dk. Lwitakubi, alisema Shirika la EGPAF limekuwa likijihusisha na kazi za kuzuia na kutokomeza maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU), kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Alisema EGPAF inafanya kazi zake katika mikoa ya Tabora, KilimanjaroArusha, Lindi, Shinyanga, Geita na Simiyu.
Aliongeza kuwa EGPAF pia imekuwa ikijihusisha na wagonjwa wa majumbani katika mikoa ya Pwani, Zanzibar na Mwanza huku likitoa huduma za uchunguzi wa
saratani ya shingo ya kizazi mikoa ya Tabora, Kilimanjaro,
Shinyanga, Arusha, Simiyu, Lindi na Geita.


Kwa upande wake, Mratibu wa Mawasiliano na Utetezi wa EGPAF, Mercy Nyanda, alisema katika huduma zao kumekuwa na mafanikio, kwani kwa sasa wajawazito wengi wanajifungulia vituoni tofauti hapo mwanzo.
Nyanda, alisema uelewa kwa jamii umeongezeka zaidi kuhusu hali halisi ya maamukizi ya VVU na jamii hiyo kuendelea kubadilika.