Makamu
wa Rais mwandamizi katika shughuli za kibiashara wa shirika la ndege la
FlyDubai ,Bwa.Sudhir Sreedharan akizungumza mbele ya wageni waalikwa
mbalimbali wakiwemo wana habari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo
pichani) katika hafla fupi ya uzinduzi wa njia mbili mpya za shirika la
ndege hiyo kutoka Dubai kuja jijini Dar es salaam na Zanzibara (nchini
Tanzania). Bwa.Sudhir amesema kuwa shirika hilo la Flydubai liliingia
katika soko la kibiashara kuanzia mnamo mwaka 12009,ambapo mpaka sasa
wamefanikiwa kuongeza njia mpya sita (six new routes ) .
Mgeni
rasmi,Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano,Mh Samia Suluhu
akizungumza mapema leo katika uzinduzi wa njia mbili mpya za ndege ya
FlyDubai aina ya Boieng 737-800,uliofanyika katika uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere,jijini Dar.
Wakiwa
katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo wa njia mpya ya
shirika la ndege la Flydubai lenye makao yake makuu Dubai..
Wageni waalikwa wakishangilia jambo.
Sehemu ya wageni waalikwa wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tukio hilo .
No comments:
Post a Comment