Pamoja
na kutekeleza mpango wa kusogeza huduma karibu na wanachama na wadau
kwa maana ya kufungua ofisi mikoani, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
umeanzisha mpango wa kupeleka huduma za Madaktari Bingwa mikoani.
Mpango huu unawahusisha Madaktari Bingwa ambao ki-ukweli ni wachache kutoka katika hospitali zifuatazo:-
- Hospitali ya Taifa ya Muhimbili;
- Taasisi ya Mifupa MOI;
- Hospitali ya Bugando.
Madaktari Bingwa hao wanafanya kazi katika hospitali za mikoa kwa kushirikiana na madaktari waliopo huko mikoani.
Madaktari hao ni mabingwa wa:-
- Magonjwa ya Moyo
- Magonjwa ya Wanawake
- Magonjwa ya Watoto
- Upasuaji na
- Mabingwa wa Dawa za Usingizi.
- LENGO LA KUANZISHA MPANGO HUO:
Lengo la kuanzisha mpango huo ni:-
- Kuwapeleka Madaktari Bingwa katika mikoa yenye uhaba mkubwa wa madaktari bingwa na kuwatumia wataalamu hao wachache kitaifa;
- Kuwapunguzia wananchi gharama za usafiri kufuata huduma za madaktari bingwa katika miji mikubwa;
- Kurahisisha utaratibu wa kumwona daktari bingwa ambao wanaonwa kwa ahadi maalum;
- Kuwapa fursa ya kujifunza na kuwajengea uwezo wa kiutendaji madaktari walioko kwenye hospitali za mikoa hiyo.
4.0 MAFANIKIO YA MPANGO HUO:
Mpango
wa kupeleka Madaktari Bingwa mikoani umekuwa na mafanikio makubwa kwa
maana ya kuwafikia walengwa ambao wana mahitaji makubwa ya huduma za
madaktari hao. Maisha ya watanzania yameokolewa kwa huduma zitolewazo na
Madaktari Bingwa unaofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Mikoa
ya Lindi, kigoma, Katavi na Rukwa imeshafikiwa na mpango huo na idadi
ya wananchi waliopata huduma hiyo ya madakatari bingwa ni kama
ifuatavyo:-
SN | MKOA | WAGONJWA WALIOONWA | WALIOFANYIWA OPERESHENI |
1 | Lindi | 258 | 6 |
2 | Kigoma | 754 | 37 |
3 | Katavi | 1276 | 37 |
4 | Rukwa | 1410 | 18 |
Jumla | 3,698 | 98 |
Mpango
huu umepokelewa kwa mtizamo chanya na wadau wetu wakiwemo wanachama na
wananchi wa mikoa husika kwa kuwa wengi wao hawana uwezo wa kufuata
huduma hizo katika hospitali kubwa ambazo nyingi ziko mbali na maeneo
wanayoishi.
5.0 RATIBA YA MIKOA INAYOFUATA
Mikoa inayofuatiwa kupelekewa huduma hii ya madaktari bingwa ni Mara,Tabora, Manyara na Mtwara.
MKOA | TAREHE | MAHALI HUDUMA ZITAKAPOTOLEWA |
Mara | 3/11/2014-8/11/2014 | Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara |
Tabora | Mipango ya maandalizi inaendelea (wanachi watajulishwa) | |
Manyara | Mipango ya maandalizi inaendelea (wanachi watajulishwa) | |
Mtwara | Mipango ya maandalizi inaendelea (wanachi watajulishwa) |
- CHANGAMOTO ZA MPANGO WA KUPELEKA MADAKTARI BINGWA MIKOANI:
Pamoja
na nia njema ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuwapeleka madaktari
Bingwa karibu zaidi ya wananchi wengi wenye mahitaji ya huduma zao, bado
zoezi hilo linakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo:
- Idadi ndogo ya Madaktari Bingwa ikilinganishwa na wananchi wanaohitaji huduma hizo.
- Uhaba wa vifaa tiba vya kisasa, kama vile vipimo katika hospitali za mikoa ya pembezoni na
- Uhaba wa vitendea kazi na madawa ili kufanikisha zoezi hili.
Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya unaamini kuwa mpango huu utaokoa maisha ya
Watanzania wengi ambao walikwishakata tamaa ya kupata tiba kutokana na
gharama kubwa za kufuata matibabu hayo katika hospitali walizopewa
rufaa.
6.0 MIPANGO YA BAADAYE YA MFUKO.
Mfuko
utaendelea kupeleka Madaktari Bingwa katika maeneo mbalimbali ya nchi
baada ya kufanya upembuzi wa mahitaji ya huduma na utaalamu katika
maeneo husika.
Kauli mbiu yetu ni “ Afya Bora Ndiyo Mambo Yote.”
No comments:
Post a Comment