Na Allan Ntana, Sikonge
WANAFUNZI wapatao 60 wa shule za sekondari wasiojiweza na wale
wanaoishi katika mazingira hatarishi katika wilaya ya Sikonge mkoani
Tabora wamepatiwa msaada wa vifaa mbalimbali vya shule vyenye thamani
ya zaidi sh milioni 12.
Hayo yalibainishwa na Afisa Maendeleo ya Jamii ambaye pia ni Mratibu
wa Kudhibiti Ukimwi katika halmashauri ya wilaya ya Sikonge Nicholous
Magoha alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake
.
Alisema msaada uliotolewa kwa wanafunzi hao kutoka shule za sekondari
Ngulu, Kamagi, Mole, Tutuo, Pangale, Igigwa, Mibono, Langwa, Chabutwa,
Ugunda, Msuva, Kiwere, Kiloli, Kiombo na Usunga ni wa sare za shule na
madaftari.
Magoha alisema halmashauri imetoa msaada huo kwa lengola kuwahamasisha
wanafunzi hao ili waweze kusoma kwa utulivu sambamba na kuwapunguzia
changamoto za kiuchumi ambazo zimekuwa zikiwarudisha nyuma hasa
ikizingatiwa kuwa wengi wa wazazi na walezi wa vijana hao hawana
uwezo.
Aliongeza kuwa msaada huo umetolewa na halmashauri hiyo kupitia
uwezeshaji wa mfuko wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi hapa nchini
(TACAIDS.
Ili kuhakikisha wanafunzi hao wanakuwa kama wenzao wawapo shuleni,
Magoha alibainisha kuwa katika mwaka huu wa fedha wanakusudia kutoa
msaada mwingine wa sare za viatu kwa vijana hao.
Aidha katika harakati za kuhakikisha wale wote wanaoishi na maambukizi
ya Virus vya Ukimwi wanawezeshwa kiuchumi, halmashauri hiyo imeendelea
kutoa mafunzo mbalimbali ya ujasiriamali kwa vikundi vya watu wote
wanaoishi na VVU ambao tayari wameshapatiwa msaada wa kifedha kupitia
mfuko huo.
Aidha alisema katika harakati za kupambana na maambukizi mapya ya
ukimwi halmashauri hiyo imeendesha semina maalumu kwa wajasiriamali
iliyoambatana na uonyeshaji sinema na upimaji bure wa ukimwi ambapo
wajasiriamali zaidi ya 200 walijitokeza kupima afya zao na 3 kati yao
walibainika kuambukizwa 1 akiwa mwanaume na 2 wanawake.
Magoha aliwapongeza Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo
Shadrack Mhagama, Mkuu wa wilaya Hanifa Selengu na kamati nzima ya
kudhibiti ukimwi iliyo chini ya Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo
Hamis Mayilla kwa jitihada zao kubwa zilizofanikisha kutolewa msaada
huo na semina iliyoendeshwa.

No comments:
Post a Comment