Pages

KAPIPI TV

Thursday, October 23, 2014

ADHA YA MAJI YAENDELEA KUWATESA WAKAZI WA KIJIJI CHA SONGAMBELE HALMASHAURI YA NSIMBO WILAYANI MLELE


MAAMUZI MADIWAN
Madiwani na watalaam wa Halmashauri ya Nsimbo wakijadili mstakabali wa maendeleo ya Halmashauri yao Nsimbo,pamoja na kujadili masuala ya elimu, Afya, Miundo mbinu ya barabara,utawala,na maengineyo lakini suala la maji lilichukua nafasi ya kipekee katika kikao hicho cha baraza la madiwani kilichomalizika mwishoni mwa wiki iiliyo
(Picha zote Kibada Kibada -Nsimbo Mlele Katavi).
???????????????????????????????
Mama akisukuma maji kwenye kisima kifupi kilichopo hapo huku akina mama wengine na watoto wakisubiri zamu yao ifike ili waweze kuchota maji  ambayo yanatoka kidogokidogo kwenye kisima hicho hapo madumu yanaonekana hayana maji,  dumu  moja kujaa inawachukua zaidi ya saa, hivyo kuwafanya watumie muda mwingi kutafuta   maji badala ya kufanya shughuli nyingine za maendeleo.
……………………………………………….
 
Na Kibada Kibada –Nsimbo Mlele
Wakazi wa Songambele Halmashauri ya Nsimbo Wilayani Mlele wanakabiliwa na Changamoto ya uhaba wa maji kufuatia visima vifupi vilivyopo kutokuwa maji ya kutosha.
 
Hali  hiyo ya uhaba wa maji kwa baadhi ya Vijiji vya Kata ya Nsimbo na maeneo mengine ya Halmashauri hiyo  inayowafanya akina mama na watoto kuamka  kila siku alfajiri  majira saa kumi usiku kwenda kutafuta maji kwa au  kusubiria  maji  kwenye visim vifupi vilivyopo ambavyo navyo havitoi maji ya kutosha hivyo kutumia muda mrefu kutafuta na kukosa muda wa kufanya shughuli nyingine za maendeleo.
 
Akizungumzia  hali ilivyotete  kuhusu upatikanaji wa maji katika Kijiji  cha Songambele  na Kata ya Nsimbo kwa ujumla Afisa Mtendaji wa Kata ya Nsimbo Wilbroad Milala anasema kwa kweli hapo maji ni shida kubwa kwa wakazi wa hapo.
 
Milala anasema hata visima vilivyopo havitoi maji ya kutosha wakati mwingine kama msimu huu wa kiangazi maji hukata hata miezi miwili bila kutoa maji hali inayofanya wakazi hao hasa akina mama na watoto kufuata maji kwenye mbuga umbali wa takribani kilometa tatu hadi nne maji amabyo siyo safi wala salama.
 
Kufuatia kuwepo kwa changamoto hiyo ya Maji wawakilishi wa wananchi ambao ni madiwani kupitia kwenye vikao vya baraza la madiwani suala la maji lilionekana kuchukua nafasi ya kipekee kuzungumzia ikiwa ni pamoja na kutafuta mbinu za kulipatia ufumbuzi.
 
Akiongea katika kikao cha Baraza la madiwani kwa nyakati tofauti Mjini Nsimbo Diwani wa Kata ya NsimboMichael Kasanga, Diwani wa Kata ya Mtapenda Eliezer Fyula,walieleza kuwa lazima hatua zichukuliwe kwa haraka ili kulipatia ufumbuzi suala la upatikanaji wa maji kwa wakazi wa Halamshauri hiyo hasa maeneo yale yenye visima vifupi vichimbwe visima virefu.
 
Wakaeleza kuwa pia visima vinapoharibika taarifa iwe inatolewa mapema kwenye Idara ya Maji ili kuona namna ya kuweza kulipatia ufumbuzi pale panapo wezeakana kama kununua vifaa vya ukarabati wa pump.
 
Awali Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu na Maji  Raphael Kalinga akiwasilisha taarifa ya Kamati yake alieleza mikakati inayochukuliwa na halmashauri ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa maji ikiwa ni pamoja na kutenga fedha kupitia bajeti zake na fedha kutoka kwenye mifuko ya maji ili kusaidia upatikanaji wa maji ikiwa pia na kuomba ufadhili kutoka kwa wahisani mbalimbali kusaidia suala la maji.
 
Aidha aliwashauri madiwani kuwahamasisha wananchi kuanzisha kamati za mifuko ya maji ili fedha inayopatikana iwe inasaidia katika matengenezo madogo madogo pindi pump za visima vya maji vinapo haribika fedha hizo zitasaidia ukarabati mdogo mdogo.
 
Katika hatua nyingine Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Nsimbo limemwagiza Kaimu Mhandisi wa Mji katika Halmashauri  Enock Msengi kuhakikisha anapoondoka awe anakaimisha ofisi kwa mwenzake anayekuwa ofisini kuliko kuacha amefunga ofisi na pia mali za ofisi inatakiwa awe anacha ofisi ikiwa wazi na awe anaandika barua ya kukabidhi ofisi kuliko kijiondokea kama anavyofanya kwa kuwa ofisi siyo mali yake bali ni mali ya Serikalai.

No comments: